Kardinali Parolin:Misa kwa ajili ya marehemu
Na Isabella H. de Carvalho
Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin alisisitiza mateso ya watu wa Ukraine waliokumbwa na vita wakati wa mahubiri yake katika Misa iliyoadhimishwa Alhamisi, tarehe 20Novemba 2025, katika Kanisa la Mtakatifu Andrea wa Valle jijini Roma. Kardinali Parolin alisema: "Nchini Ukraine, "Hakuna uhalali wa kulazimisha maelfu ya raia kuishi katika giza na baridi. Tunaathiriwa sana na habari za mashambulizi ya mifumo ya umeme katika miundo ya kiraia, ambayo imefanya maisha kuwa magumu zaidi kwa watu wengi".
Liturujia hiyo iliyoandaliwa na Ubalozi wa Kiukreni mjini Vatican na Serkali ya Malta, iliyoadhimishwa kuwakumbuka waathiriwa wa mauaji ya Kimabri ya Holodomor kati ya 1932-33, na njaa iliyosababishwa na serikali ya Kisoviet, baada ya watu wa Ukraine kupinga mfumo wa pamoja wa mali, ambao ulisababisha mamilioni ya vifo. Kila kitendo ambacho kinawanyima raia uwezekano wa kuishi kwa utu ni kosa dhidi ya ubinadamu na hasira dhidi ya Mungu, ambaye ni mwanga, uzima na huruma. Hatuwezi kubaki kutojali wale wanaoteseka kwa njaa, kutokuwa na uhakika, vita, baridi ya baridi, vifungo, na uhamisho," Kardinali alisema. Kardinali aidha alikumbuka maneno ya Papa Leo XIV kwa waandishi wa habari aliyesema siku Jumanne jioni, Novemba 18 kuwa: "Kwa bahati mbaya, kila siku, watu wanakufa. Ni lazima tusisitize amani, kuanzia na usitishaji huu wa mapigano, na kisha mazungumzo."
Hofu ya Holodomor
Katika mahubiri yake, Kardinali Parolin alisema Holodomor ilikuwa na njaa kali sana iliyosababishwa kwa makusudi na "chuki, ukosefu wa haki, kutojali, na matumizi mabaya ya mamlaka". Aliwakumbuka waliathirika kama watoto wanaopendwa na Mungu, kaka zetu na dada zetu ambao kuteseka kwao kunaendelea kutatiza dhamiri ya ulimwengu.” Katika Mwaka huu wa Jubilei, unaojikita na mada ya Matumaini, Katibu Mkuu alimwomba Mwenyezi Mungu "kulainisha mioyo migumu, kusimamisha mikono yenye jeuri, kufungua njia za mazungumzo na amani. " Pia alisema ni muhimu kufanya upya tumaini “kwa waathiriwa wa jana, wanaoteseka leo, kwa watu wanaotamani amani, uhuru, na wakati ujao wenye amani.”
"Leo, hii pamoja na watu wa Ukraine walio na majeraha ya kihistoria na maafa ya vita vinavyoendelea, tunaitwa kudumu katika sala na kutoa ushuhuda wa imani inayostahimili, inayotumaini, inayongoja kwa ukimya, lakini kama nguvu, kwa wokovu wa Bwana," akaongeza. Aliomba maombi kwa ajili ya wafungwa, kwa wale “waliobeba majeraha ya vita katika miili yao na roho”, kwa familia zilizogawanyika na watoto wanaoogopa, na kwa “mioyo ambayo imepoteza matumaini”. “Leo, mbele ya madhabahu ya Bwana, tunafanya upya imani yetu kwa Mungu wa uzima, tukiwakabidhi rehema zake za milele waathriwa wote wa njaa, chuki, na jeuri,” Kardinali huyo alimalizia, “nasi tunasihi kwa unyenyekevu na kwa uhakika kwamba mapambazuko ya amani, amani ya haki na ya kudumu, ipate kutokea hivi karibuni kwa Ukraine.”
Shukurani za Balozi
Balozi wa Ukraine anayewakilisha nchi yaji jijini Vatican, Andrii Yurash, alimshukuru Kardinali Parolin na wote waliohudhuria, wakiwemo wawakilishi kadhaa wa kisiasa wa Italia na zaidi ya mabalozi 50 kutoka miongoni mwa takriban misheni 80 zilizoko Roma. Yurash aliakisi hasa uwepo wa ujumbe wa vijana wanne wa Ukraine kati ya miaka 14 na 18 ambao, mwanzoni mwa vita, walipelekwa Urusi na sasa wamerudishwa kwa familia zao. Pia alisisitiza uwepo wa wanawake watatu, "mashujaa wa upinzani na heshima" ambao alisema, walionesha "nguvu na uamuzi wa ajabu". Mwishoni mwa Misa, pia kulikuwa na uzinduzi wa maonesho ya sanaa "Sala kwa Ukraine" na tamasha na utendaji wa Metropolitan String Quintet. Misa hiyo pia ilihudhuriwa na Naibu Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Ukraine, Iryna Vereshchuk.
Mpango wa amani
Baada ya Misa hiyo, akijibu maswali ya waandishi wa habari, Kardinali aliakisi mada ya vita hivyo, akitoa maoni yake kuhusu mpango wa amani wenye vipengele 28 uliopendekezwa na Rais wa Marekani Bwana Donald Trump. Matumaini yake, alisema, ni kwamba "njia za mazungumzo zitafunguliwa ambazo zitaruhusu janga hili kumalizika." "Itakuwa vigumu sana kupata maelewano kati ya mahitaji ya upande mmoja na matakwa ya upande mwingine. Kwa hivyo ninafikiri kwamba njia ya mazungumzo itakuwa vita kubwa," alisema..
Kwa maoni yake kadhalika alisema "Ulaya inapaswa kushiriki na kutoa sauti yake, sio kubaki kutengwa," sio kwa sababu "imeshiriki kikamilifu" nchini Ukraine hadi sasa. Kuhusu suala la kusitishwa kwa maeneo, "ni mapema" kulizungumzia, pia kwa sababu litakuwa ni matokeo ya mazungumzo." Kwa kusisitiza zaidi alisema "Amani itapatikana tu ikiwa pande zote mbili zitaridhika kwa kiasi fulani na maelewano, kwa sababu mwishowe mwafaka itabidi kufanywa."
Kazi ya Vatican
Kardinali huyo aliongeza kusema kwamba, Vatican bado imejitolea kurudi kwa watoto wafungwa wa Kiukreni waliopelekwa Urusi: "Tunaendelea kufanya kazi katika eneo hili, na inaonekana kwangu kwamba utaratibu kuhusu watoto sasa umefanywa upya. Tuko tayari kusaidia katika eneo hili kwa sababu tunaamini kwamba, zaidi ya kuwajali wale wanaoteseka, pia hutengeneza hali ambayo itasababisha amani," alisema.