Mons.Balestrero:Mfumo wa pande nyingi kwa sasa unapitia nyakati za misukosuko
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Askofu Mkuu Ettore Balestrero, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa alitoa hotuba yake, tarehe 18 Novemba 2025 huko Geneva Uswiss katika Kikao cha 355 cha Uongozi wa Shirika la Kani Ulimwenguni( ILO). Akianza hotuba yake Askofu Mkuu Balestrero alisema, Vatican ilipenda awali ya Yote kumshukuru Mkurugenzi Mkuu, Ofisi na washirika wote wa kijamii kwa kazi iliyofanywa kuhusu jambo hilo. Mfumo wa pande nyingi kwa sasa unakabiliwa na nyakati za misukosuko.
Katikati ya msukosuko huu, ni muhimu kurudi kwenye kanuni ambazo Shirika hili lilianzishwa. Imani kwamba "wanadamu wote [...] wana haki ya kufuata ustawi wao wa kimwili na maendeleo yao ya kiroho katika hali ya uhuru na utu" na wazo la "amani ya ulimwengu na ya kudumu, kulingana na haki ya kijamii" lazima ihakikishwe tena.
Umuhimu wa kudumisha uadilishu na uaminifu wa mfumo
Kila mageuzi lazima yaanzie hapo. Hii ni muhimu katika ngazi tatu. Kwanza, ni muhimu kwa kudumisha uadilifu na uaminifu wa mfumo mpana wa pande nyingi, ikizingatiwa kwamba ILO ndiyo shirika pekee la pande tatu lenye jukumu la kukuza haki ya kijamii na kazi nzuri. Pili, ni muhimu kwa uhai wa kitaasisi na ufanisi wa uendeshaji wa ILO. Mageuzi yanapaswa kuongozwa na hisia ya pamoja ya uwajibikaji ili kuhakikisha umuhimu wa Shirika katika ulimwengu unaobadilika, na si tu kwa vikwazo vya kifedha.
Kama Papa Leo XIV anavyosema, kuna haja ya "kutambua kwamba muhimu zaidi kuliko matatizo yetu au suluhisho la mwisho ni jinsi tunavyoyashughulikia, tukiongozwa na vigezo vya utambuzi, na kanuni nzuri za maadili." Tatu, kusudi kuu la kuimarisha ILO ni kuwanufaisha wafanyakazi, waajiri, na jamii kupitia mwongozo na programu za Shirika.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here