Walinzi wa Uswiss,uchunguzi wa ndani kuhusu"mzozo"katika moja la lango la Vatican
Vatican News
"Kikosi cha Walinzi wa Kipapa cha Uswiss kimepokea ripoti kuhusu tukio lililotokea katika moja ya milango ya kuingia katika Jiji la Vatican, ambapo vipengele vilivyotafsiriwa kuwa na chuki dhidi ya Wayahudi viligunduliwa. Kulingana na uchunguzi mpya wa awali, ripoti hiyo inarejea kutokubaliana kuliotokea kuhusu ombi la picha katika kituo cha walinzi."
Hayo yalisemwa na Dk. Matteo Bruni, Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu tukio hilo, lililoripotiwa hivi karibuni na vyombo kadhaa vya habari, kuhusu madai ya maneno kutoka kwa Walinzi wa Uswisi yaliyoripotiwa na wanawake wawili wa Kiyahudi. "Jambo hilo," kwa mujibu wa Dk Bruni alieleza kuwa, "kwa sasa ni mada ya uchunguzi wa ndani, unaoamilishwa kulingana na taratibu zilizowekwa kwa ripoti zinazowahusisha wajume wa kikosi cha Walinzi. Utaratibu huu unafanywa kwa kufuata kanuni za usiri na muaaka, na kwa mujibu wa sheria za sasa."
"Kwa kuzingatia utamaduni wake wa karne nyingi ya huduma," Walinzi wa Uswisi - kama ilivyoelezwa katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican - "inathibitisha tena kujitolea kwake mara kwa mara kuhakikisha kwamba dhamira yake inatekelezwa kila wakati kwa heshima ya utu wa kila mtu na kanuni za msingi za usawa na kutobagua."