Askofu mkuu Andrés Carrascosa Coso ameteuliwa na Papa Leo XIV kuwa  Balozi mpya wa Vatican nchini Ureno., 2025 Askofu mkuu Andrés Carrascosa Coso ameteuliwa na Papa Leo XIV kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ureno., 2025  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Askofu Mkuu Andrès Carrascosa Coso Balozi wa Vatican Nchini Ureno

Askofu mkuu Andrés C. Coso amateuliwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Ureno. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Andrés Carrascosa Coso alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ecuador. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Andrés Carrascosa Coso alizaliwa tarehe 16 Desemba 1955 huko Cuenca, nchini Hispania. Baada ya malezi na masomo yake ya Kipadre, tarehe 2 Julai 1980 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre; tarehe 7 Oktoba 2004 akawekwa wakfu kuwa Askofu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 11 Desemba 2025 amemteua Askofu mkuu Andrés Carrascosa Coso kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Ureno. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Andrés Carrascosa Coso alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ecuador. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Andrés Carrascosa Coso alizaliwa tarehe 16 Desemba 1955 huko Cuenca, nchini Hispania. Baada ya malezi na masomo yake ya Kipadre, tarehe 2 Julai 1980 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 31 Julai 2004 akateuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa Balozi wa Vatican nchini Congo na hivyo kumpadisha hadhi kuwa Askofu mkuu.

Askofu mkuu Andrès Carrascosa Coso, Balozi wa Vatican nchini Ureno
Askofu mkuu Andrès Carrascosa Coso, Balozi wa Vatican nchini Ureno   (Vatican Media)

Tarehe 26 Agosti 2004 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Gabon na hatimaye, kuwekwa wakfu kuwa ni Askofu tarehe 7 Oktoba 2004. Ilipogota tarehe 12 Januari 2009, Baba Mtakatifu Benedikto XVI akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Panama. Ilikuwa ni tarehe 22 Juni 2017, Baba Mtakatifu Francisko alipomteuwa Askofu mkuu Andrés Carrascosa Coso kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ecuador na hatimaye tarehe 11 Desemba 2025 Baba Mtakatifu Leo XIV akamwamisha na kumpeleka nchini Ureno.

Uteuzi Ureno

 

18 Desemba 2025, 15:29