Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 17 Februari 2026 amemteuwa Mheshimiwa Sana Padre Amos Mabuti Masemola kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kroonstad, Afrika ya Kusini Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 17 Februari 2026 amemteuwa Mheshimiwa Sana Padre Amos Mabuti Masemola kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kroonstad, Afrika ya Kusini  (ANSA)

Askofu Amos Mabuti Maselo Jimbo Katoliki La Kroonstad, Afrika Ya Kusini

Padre Amos Mabuti Masemola ameteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Kroonstad, Afrika ya Kusini. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Amos Mabuti Masemola alikuwa ni Makamu Askofu wa Jimbo kuu la Pretoria na Paroko wa Parokia ya “St. Thomas More in Centurion.” Itakumbukwa kwamba alizaliwa tarehe 5 Machi 1978 huko Windterveld, Pretoria. Baada ya masomo, malezi na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 3 Juni 2007 akapewa Daraja Takattifu ya Upadre.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 17 Februari 2026 amemteuwa Mheshimiwa Padre Amos Mabuti Masemola wa Jimbo kuu la Pretoria, Afrika ya Kusini kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kroonstad, Afrika ya Kusini. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Amos Mabuti Masemola wa Jimbo Katoliki la Kroonstad alikuwa ni Makamu Askofu wa Jimbo kuu la Pretoria na Paroko wa Parokia ya “St. Thomas More in Centurion.” Itakumbukwa kwamba alizaliwa tarehe 5 Machi 1978 huko Windterveld, Pretoria. Baada ya masomo, malezi na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 3 Juni 2007 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Pretoria.

Askofu Amos Mabuti Masemola, Jimbo Katoliki la Kroonstad. A. Kusini
Askofu Amos Mabuti Masemola, Jimbo Katoliki la Kroonstad. A. Kusini   (ANSA)

Tangu wakati huo, kama Padre amewahi kuwa Paroko-usu, Paroko hadi mwaka 2016 alipotumwa na Jimbo kwenda kujiendeleza zaidi kwenye Chuo Kikuu cha Kikatoliki Afrika Mashariki (The Catholic University of Eastern Africa – CUEA, Nairobi, Kenya) na hapo akajipatia Shahada ya Uzamili kuhusiana na Tasaufi ya Kikristo. Tangu mwaka 2016 hadi mwaka 2020 aliteuliwa kuwa ni Msimamizi wa Kanisa kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Jimbo kuu la Pretoria; “Chancellor” tangu Mwaka 2016-2020; Mjumbe wa Baraza la Washauri wa Jimbo tangu mwaka 2026; Padre Mlezi wa Maisha ya kiroho tangu mwaka 2017 na Mwalimu, Seminari ya St. John Vianney, Jimbo kuu la Pretoria Mwaka 2018 Paroko wa Parokia ya “St. Thomas More in Centurion” kuanzia mwaka 2021, Askofu Msaidizi na Mchumi wa Jimbo kuu la Pretoria hadi kuteuliwa kwake tarehe 17 Februari 2026 kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kroonstad, Afrika ya Kusini.

Uteuzi Afrika ya Kusini
17 Februari 2026, 14:03