2025.03.18 Cupola di San Pietro

Jumuiya ya Mt.Pio X yakataa mazungumzo yaliyopendekezwa na Kiti Kitakatifu.Wathibitisha wakfu

Katika barua iliyoelekezwa kwa Kardinali Fernández,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kwa Mkuu wa Shirika la Pio X Padre Pagliarani anasema kwamba haoni uwezekano wa kuanzisha mazungumzo ya"Kitaalimungu,kama ilivyopendekezwa na Vatican,ikizingatiwa kwamba "maandiko ya Mtaguso hayawezi kusahihishwa,wala uhalali wa mageuzi ya kiliturujia unaotiliwa shaka."Kwa hivyo,uamuzi wa wakfu Maaskofu,Julai 1.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Kuna kukataa kwa pendekezo la Vatican la mazungumzo "mahususi ya kitaalimungu", kwa sababu kwa vyovyote vile, maandishi ya Mtaguso au uhalali wa mageuzi ya kiliturujia hayatawahi kutiliwa shaka. Ndiyo kwa ya kuwekwa wakfu kwa Maaskofu wapya uliopangwa kufanyika tarehe 1 Julai 2026. Jumuiya ya Mtakatifu Pio X ilijibu kwa barua kutoka kwa Mkuu wake, Padre Davide Pagliarani, kuilekeza kwa Kardinali Víctor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, kufuatia mkutano wa wanaume hao wawili mjini Vatican uliofanyika mnamo tarehe 12 Februari 2026. Katika taarifa iliyofuata, Kardinali Fernández alielezea mkutano huo kama "wa kirafiki" na "wa dhati," baada ya hapo akatangaza kwamba alikuwa amependekeza kwa wajumbe wa Jumuiya kwamba waanze "mazungumzo mahususi ya kitaalimungu” kwa "mbinu sahihi sana, kuhusu masuala ambayo bado hayajafafanuliwa vya kutosha."

Pendekezo hilo linaambatana na ombi la kusimamisha kuwekwa wakfu wa kiaskofu uliotangazwa tarehe 2 Februari,  kwa sababu hiyo  "ingemaanisha kuvunjika kwa ushirika wa kikanisa (utengano) na matokeo mabaya kwa Udugu kwa ujumla." Juma lililopita, Padre  Pagliarani alitangaza kwamba angewasilisha pendekezo la Vatican kwa wajumbe wa Baraza Kuu la Udugu na kuthibitisha kwamba "muda muhimu umechukuliwa kulitathmini." Tarehe 18  Februari 2026, Kardinali alipokea jibu lililosainiwa na wajumbe watano wa Baraza Kuu.


Pendekezo la Mazungumzo

Katika barua iliyotumwa kwa  Kardinali Fernández, Mkuu wa Shirika waitwao Lefebvrians ( jina la Askofu Marcel Lefebvre, ambaye alianzisha Shirika hilo miaka ya 1970 kupinga mageuzi ya Mtaguso wa  Pili wa Vatican) alisema anakaribisha, kwa upande mmoja, "uwazi mpya wa mazungumzo," kama "jibu chanya" kwa pendekezo la "mjadala" wa kimafundisho ambao yeye mwenyewe alikuwa tayari ameutoa Januari 2019, katika "wakati wa utulivu na amani, bila shinikizo au tishio la kutengwa." Kwa upande mwingine, Padre Pagliarani anakataa pendekezo la Vatican kwa sababu mchakato wa mazungumzo ya pamoja haungeweza "kufikia uamuzi wa pamoja wa kile ambacho kingekuwa 'kiwango cha chini kabisa kinachohitajika kwa ushirika kamili na Kanisa Katoliki,'" kwani "maandiko ya Mtaguso hayawezi kusahihishwa, wala uhalali wa mageuzi ya kiliturujia unaotiliwa shaka."

"Mtaguso," Pagliarani anasisitiza, "si mkusanyiko wa maandishi yanayoweza kutafsiriwa kwa uhuru: yamepokelewa, kuendelezwa, na kutumika kwa miaka sitini na Mapapa waliofuatana, kulingana na miongozo sahihi ya kimafundisho na ya kichungaji. Usomaji huu rasmi unaoneshwa, kwa mfano, katika maandishi muhimu kama vile Redemptor hominisUt unum sintEvangelii gaudium o Amoris lætitia. Na inajidhihirisha katika mageuzi ya kiliturujia, yanayoeleweka kwa kuzingatia kanuni zilizothibitishwa tena  Traditionis custodes. Nyaraka hizi zote zinaonesha kwamba mfumo wa mafundisho na kichungaji ambao Kiti Kitakatifu kinakusudia kuweka kila mjadala tayari umewekwa.

Kuweka wakfu wa kiaskofu wathibitishwa

"Kwa sababu hizo," Pagliarani anaongeza, "katika ufahamu wa pamoja kwamba hatuwezi kufikia makubaliano kuhusu mafundisho, inaonekana kwangu kwamba jambo pekee tunaloweza kukutana nalo ni lile la upendo kwa roho na kwa Kanisa." Kiongozi wa Jumuiya ya Papa PIO X (SSPX)ambaye anakataa kwa ufanisi uhalali wa ibada ya kiliturujia inayotokana na mageuzi ya kiliturujia, anasema kwamba hawezi kukubali "mtazamo na malengo ambayo Baraza la Kipapa linapendekeza kuanza tena kwa mazungumzo katika hatua hii; wala, wakati huo huo, kuahirishwa kwa tarehe 1 Julai." Kwa hivyo, kuwekwa wakfu kwa Maaskofu wapya kunathibitishwa kama "hitaji halisi la muda mfupi la kuendelea kuishi kwa Tamaduni.”

Kauli ya Kardinali Fernández

Kama inavyoweza kukumbuka, katika kauli yake ya  tarehe 12 Februari 2026, Kardinali Fernández alisema: "Kiti Kitakatifu kimesisitiza kwamba kuwekwa wakfu kwa Maaskofu bila idhini ya Baba Mtakatifu, ambaye ana mamlaka kuu ya kawaida, ambayo ni kamili, ya ulimwengu wote, ya moja kwa moja, (taz. Kanuni ya Sheria ya Kanisa,n 331; Katiba ya Kidogma Mchungaji Milele”pastor aeternus, sura ya I na III) kungemaanisha kuvunjika kwa uamuzi wa ushirika wa Kanisa (utengano), na matokeo mabaya kwa Jumuiya kwa ujumla (Yohane Paulo II, Barua ya Kitume Ecclesia Dei, Julai 2, 1988, n. 3 na 5c; Baraza la Kipapa la Maandiko ya Kisheria, Maandishi ya Maelezo, Agosti 24, 1966, n1)."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

20 Februari 2026, 09:48