Kard.Parolin:Tupokee Urithi wa Attanaso katika ulimwengu,wema ni muhimu zaidi kuliko vurugu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tupokee urithi wa Luca Attanasio, "kuendelea kujenga ulimwengu ambapo amani inatamaniwa zaidi kuliko vita, ambapo wema ni muhimu zaidi kuliko vurugu, ambapo mshikamano una ufanisi zaidi kuliko faida." Hivi ndivyo Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, alivyokumbuka ushuhuda wa Balozi wa Italia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, aliyeuawa miaka mitano iliyopita katika shambulio la kuvizia pamoja na Askari Mlinzi wake Vittorio Iacovacci na dereva wake Mustapha Milambo, wakati wa kumbukumbu katika makaburi ya Limbiate, katika jimbo la Monza na Brianza, asubuhi ya Dominika tarehe 22 Februari 2026
Kujitolea zaidi ya wito wa wajibu, kujenga ulimwengu bora
Mita chache kutoka kaburi la mwanadiplomasia huyo aliyeuawa akiwa na umri wa miaka 43, huku binafsi akifuatilia misheni ya kibinadamu ya Mpango wa Chakula Duniani, Kardinali Parolin alisema kuwa alitoa, maisha yake, "akikubali wito wa kujenga ulimwengu bora si tu kwa mawazo na dhana, bali kwa maneno na ishara halisi, za kweli, na za dhati." Na akitoa kwa familia yake, "kwa Zakia na binti zake, kwa wazazi wake, kwa dada yake, kwa marafiki ambao bado wanathamini ukaribu wake."
Luca na Uthabiti wa Upendo
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Vaticana, urithi wa Luca ni ule wa upendo unaoonekana, katika hamu ya kuwa karibu na wale wanaohitaji, katika "uthabiti wa upendo, kupitia ishara zinazoshuhudia "mawazo mengi yanayotolewa kwa maskini na kwa jumuiya za kimisionari alizokutana nazo katika kutekeleza majukumu yake ya kitaasisi." Maneno yake, pia, yale ya moja yaliyoundwa katika shule ya Neno la Mungu, yaliruhusu Attanasio, katika misheni zake za kidiplomasia, kueleweka, "kuleta ujumbe wa amani na faraja, pamoja na uwezo, alisisitiza Kardinali Parolin, katika kumbuka Mwandiplomasia huyo aliyeuwawa kikatili."
Mattarella: Italia inaitazama Afrika kwa hisia za ubinadamu
Katika kumbukumbu hiyo hiyo, ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, pia ulifika kwa Meya wa Limbiate na familia ya Balozi aliyeuawa nchini Congo mnamo tarehe 22 Februari 2021. "Katika mgogoro mkubwa unaoendelea kuikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo," Mkuu wa Nchi aliandika, "kumbukumbu ya Balozi Attanasio na dhamira yake inabaki kuwa ya mfano zaidi kuliko hapo awali." Rais Mattarella aliongeza, "kujitolea kwake kunawakilisha maadili mema ya Jamhuri ya Italia, ambayo yanaangalia bara la Afrika kwa roho ya ushirikiano na ubinadamu. Thamani ya kujitolea kwa kila siku kwa watumishi wa Jamhuri ya Italia ambao, kwa ujasiri na hisia ya wajibu, hufanya kazi katika maeneo yaliyo na ukosefu wa utulivu na hatari, inarudiwa katika mfano wa Luca Attanasio na wale waliokuwa pamoja naye."
Sala ya Kardinali Parolin katika Misa: Maisha ya Ushirikiano Miongoni mwa Watu
Baadaye, saa 5:30 asubuhi, Kardinali Parolin aliongoza ibada ya misa katika Kanisa la Mtakatifu George huko Limbiate. Katika mahubiri yake, Katibu Mkuu alisisitiza kwamba kumbukumbu ya Attanasio, katika jiji lake, "inaendelea kupinga dhamiri ya pamoja, kwa sababu kuna maisha ambayo, hata yakikatizwa kwa njia ya kusikitisha, yanabaki kama swali wazi kuhusu maana ya huduma, uwajibikaji, na kujitolea kwa manufaa ya wote." Alimkumbuka kwamba maisha yake, "yaliyotumika katika huduma kwa Serikali na katika kukuza ushirikiano miongoni mwa watu, yalikabiliwa na mazingira magumu, ambapo maslahi binafsi, ufahari, na nguvu wakati mwingine huonekana kutawala."
Kufanya chaguzi kulingana na mantiki ya huduma ya uaminifu
Na alihitimisha kwamba matokeo yake yanaendelea kuuliza swali gumu: "Ni mantiki gani inayoongoza chaguzi zetu za kibinafsi na za pamoja? Ile ya matumizi ya haraka au ile ya huduma ya uaminifu?" Jangwa ambalo Injili ya Dominika hii inatupeleka, pamoja na Yesu, basi "sio mahali mbali na historia, bali ni nafasi ya ndani ambayo tunaamua jinsi ya kuipitia." Kwetu sisi pia, jaribio halijumuishi kukosekana kwa njia mbadala, "bali katika hitaji la kupambanua kati ya kile kinachoonekana kuwa na ufanisi katika siku zijazo za karibu na kile kinachopatana na mapenzi ya Mungu."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here