Uzinduzi wa Vituo vipya vya njia ya Msalaba katika Basilika ya Mtakatifu Petro. Uzinduzi wa Vituo vipya vya njia ya Msalaba katika Basilika ya Mtakatifu Petro. 

Vituo vipya vya njia ya Msalaba vimezinduliwa katika Basilika ya Mtakatifu Petro

Ijumaa,Februari 20,saa tisa alasiri katika Basilika ya Mtakatifu Petro,mjini Vatican Vituo vipya vya Njia ya Msalaba vilizinduliwa.Kazi hiyo iliundwa na msanii kijana wa Uswiss Manuel Andreas Dürr, aliyechaguliwa baada ya shindano la kimataifa lililovutia zaidi ya watu elfu moja.Sherehe ya uzinduzi wa Vituo vya Msalaba ilifuata ibada ya Njia ya Msalaba saa 10.00 Jioni.

Vatican News

Kama sehemu ya mipango iliyotangazwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka Mia Nne ya Kuwekwa Wakfu kwa Basilika ya Vatican(1626–2026),(Fabbrica di San Pietro), yaani Karakana ya Mtakatifu Petro ilizindua Vituo vipya vya njia ya Msalaba ndani ya Basilika ya Mtakatifu Petro, Ijumaa tarehe 20 Februari 2026, saa Tisa alasiri.  Kazi hiyo imefanywa na msanii kijana kutoka Uswiss Manuel Andreas Dürr, aliyechaguliwa kufuatia shindano la kimataifa lililotangazwa mnamo Desemba 2023.

Njia ya Msalaba katika basilika ya Mtakatifu Petro
Njia ya Msalaba katika basilika ya Mtakatifu Petro

Shindano la Kimataifa

Shindano hilo, lililofunguliwa bila ubaguzi wa utaifa, jinsia, umri, au dini, lilivutia zaidi ya maombi elfu moja kutoka nchi themanini katika mabara matano. Tume hiyo, iliyojumuisha wanahistoria wa sanaa, wanaliturujia, na wawakilishi wa taasisi za Vatican, baada ya uteuzi wa awali kulingana na Wasifu wao(CV) na kwingineko za picha, iliwaalika wasanii kumi na wanne kuwasilisha michoro miwili, ikiwa ni pamoja na ile ya lazima iliyowekwa katika kituo cha kumi na mbili: Yesu anakufa msalabani.

Kijana wa uswiss aliyeshinda kutengeneza njia ya Picha ya Msalaba
Kijana wa uswiss aliyeshinda kutengeneza njia ya Picha ya Msalaba

Baada ya tathmini makini, pendekezo la Dürr lilichaguliwa kwa kauli moja kwa usawa wake wa utunzi na nguvu ya kuelezea ambayo inatafsiri Fumbo la Pasaka. Vituo kumi na vinne, vilivyotengenezwa na mafundi wa Karakana ya Mtakatifu Petro, vitakuwepo kando kando ya kuzunguka Ungamo kwa kipindi chote cha Kwaresima, vikihudumia maombi ya waamini na wageni.

Mshindi wa kutengeneza picha za njia ya Msalaba

Uzinduzi wa Njia ya Msalaba

Saa kumi 10.00 jioni mara tu baada ya uzinduzi mfupi, ibada ya Njia ya Msalaba ilifanyika ndani ya Basilika ya Mtakatifu Petro. Sherehe hiyo iliwaongoza washiriki kando ya vituo kumi na vinne, katika safari ya kutafakari Mateso ya Bwana, pamoja na masomo, sala, na wakati wa ukimya, katikati ya nafasi ya liturujia inayohifadhi kumbukumbu ya Mtume Petro.

Njia ya Msalaba
Njia ya Msalaba

Mazungmzo katia ya sanaa na liturujia kwa jumuiya ya Kanisa na mahujaji

Kwa njia hii mpya ya Msalaba, Basilika ya Mtakatifu Petro inasasisha mazungumzo kati ya sanaa na liturujia, ikiwapatia jumuiya ya Kanisa na mahujaji ishara inayoonekana ya jinsi uzuri unavyoendelea kuwa njia ya kupendelewa ya kutafakari fumbo la Msalaba.

Maelezo kutoka kwa Mons Pepe kuhusu Njia mpya ya Msalaba
VITUO VYA NJIA YA MSALABA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

20 Februari 2026, 19:34