Njia ya Msalaba ya kiutamaduni itafanyika tarehe 3 Aprili 2026. Njia ya Msalaba ya kiutamaduni itafanyika tarehe 3 Aprili 2026.  (ANSA)

Njia ya Msalaba Colosseum:Papa Leo XIV atabeba Msalaba katika kila kituo!

Siku ya Ijumaa,Aprili 3,Papa Leo XIV ataongoza ibada ya kukumbuka safari ya Yesu kwenda Golgotha katika Uwanja wa Maonesho wa Flavian,Ujulikanao Colosseum.Tafakari za njia ya Msalaba ziliandikwa na Padre Francesco Patton OFM.

Vatican News

Papa Leo XIV, atabeba Msalaba  kupitia vituo vyote 14 katika Colosseum, ikiwa ni kwa mara ya kwanza  kufanya Njia ya  Msalaba,  Ijumaa Kuu, tarehe 3 Aprili 2026, katika Uwanja wa Maonyesho wa Flavian, Roma. Padre Francesco Patton(OFM) aliyekuwa Msimamizi wa Nchi Takatifu kuanzia 2016 hadi 2025, ndiye aliyepewa jukumu la kuandika tafakari kuhusu safari ya Njia ya Msalaba ya Yesu kuelekea Golgotha.

Ofisi ya Habari ya Vatican, ilitangaza kuwa tafakari hiyo na itachapishwa Ijumaa,  karibia na saa 6.00 za mchana majira ya Ulaya. Ndugu Mdogo Mfransiskani kutoka Mlima Nebo, Yordan, amezungumza mara kwa mara kwa ajili ya mateso ya watu wa Mashariki ya Kati, hasa katika wakati huu mgumu.

Mwaka 2025, kama ilivyokuwa mwaka 2024, tafakari hizo za njia ya Msalaba ziliandikwa na Papa Francisko, ambaye alirudi Nyumba ya Mtakatifu Marta, mara  baada ya kukaa hospitalini kwa muda mrefu katika Hospitali ya Gemelli, Roma. Ibada ya Ijumaa Kuu, tarehe 18 Aprili 2025, iliongozwa na Kardinali Baldo Reina, Makamu wa Papa Jimbo Kuu la Roma, kwa ombi la Papa mwenyewe wa Argentina.

PAPA ATABEBA MSALABA IJUMAA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

31 Machi 2026, 16:55