Kardinali Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican wakati wa kuheshimu masalia ya Mtakatifu Francis wa Assisi. Kardinali Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican wakati wa kuheshimu masalia ya Mtakatifu Francis wa Assisi. 

Kard.Parolin:Viongozi wa dunia wasikilize kilio cha wale wanaotaka ulimwengu mpya

Katibu Mkuu wa Vatican,katika mahojiano na Ndugu Giulio Cesareo,OFMConv,Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Conventi Takatifu ya Assisi,alikumbusha:“katika muktadha wenye wasiwasi wa nyakati hizi,kuna ishara za matumaini,za watu wanaotaka jumuiya mpya ambapo imani inatoa mwongozo halisi,hasa mada ya udugu."

Na Benedetta Capelli – Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, alijumuishwa katika Podikasti iitwayo: "Parole povere" kwenye chaneli ya YouTube "ya Mtakatifu Francis wa Assisi, iliyochapishwa tarehe 1 Aprili 2026 kuhusu mahojiano yaliyofanywa naNdugu  Giulio Cesareo,OFMConv. Akifanya mahojiano hayo Kardinali alionesha wasiwasi wa dunia ambao unahitaji ishara za matumaini:  “Ishara hizi za matumaini zimepungua lakini hata hivyo zipo katika ulimwengu mgumu, unaokumbwa na migogoro na vita, ambapo  kuna watu wengi wanaotoa sauti zao na ambapo imani hupinga jaribu rahisi la kuhisi kuzungukwa na maadui pekee, shukrani zaidi ya yote kwa upendo uliofundishwa na Yesu, ambaye anakuwa vitu vyote kwa watu wote na anatafuta kujenga uhalisia wa amani. Mahojiano hayo yalifanywa na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Conventi Takatifu ya Assisi, mnamo tarehe 15 Machi 2026, wakati Kardinali Parolin alipoongoza Misa katika Basilika ya Juu katika fursa ya maonesho maalum ya masalia ya Mtakatifu Francis kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 800 ya kifo chake.

Tumaini ni la wale ambao hawakati tamaa

Kardinali Pietro Parolin alizungumzia muktadha wenye wasiwasi, akimaanisha kinachotokea katika sehemu mbalimbali za dunia. "Tukiangalia huku na huko," alisema, "sote tuna wasiwasi wa kweli kuhusu kinachotokea. Lakini ishara za matumaini ziko kwa watu hasa. Hawakubali ukweli huu bila kujali na kusema kwamba ulimwengu mpya unawezekana, jamii mpya inawezekana, njia mpya ya kuishi na kuhusiana na wengine inawezekana," Kardinali Parolin alisema.

Imani katika Upendo

Katibu Mkuu wa Vatican alibainisha “Njia mpya iliyozaliwa kutokana na sababu kubwa ya tumaini, imani yetu, ambayo inatoa mwongozo halisi, hasa mada ya udugu. “ Kwa kuongeza alisema. "Tunakabiliwa na ulimwengu uliogawanyika kama wetu, ambapo kuna hatari ya kuhisi kuzungukwa na wapinzani na maadui pekee, ujumbe unaotujia leo kutoka kwa Francis, ambaye anarudia ujumbe wa Yesu, ni kumpenda kila mtu, hata adui zetu. Ni kutokana na upendo huo pekee ndipo tunaweza kupata tumaini: upendo unaokuwa vitu vyote kwa watu wote na unaotafuta kujenga uhalisia wa amani."

Mtakatifu Francis, Ujumbe wa Matumaini

Akizungumzia kuhusu Mtakatifu Francis, alikumbuka kwamba maskini wa Assisi "anakumbusha umuhimu wa Kristo." Na katika wakati huu wa mkanganyiko, Kardinali alisisitiza hitaji la "kupendekeza watu, sio mawazo mengi, ambao wanaweza kuwa marejeo kwa watu.” "Hii pia inaelezea wimbi kubwa la mahujaji huko Assisi, waliofika kwa ajili ya kuona masalia ya Mtakatifu, kwa sababu "watu wanahisi hitaji la kuwa na mifano na mifano mbele yao" katika maisha yao ya kila siku. "Francis ni ujumbe wa matumaini unaoendeleza ujumbe tuliojaribu kuishi wakati wa Mwaka wa Jubilei."

KARD.PAROLIN

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

01 Aprili 2026, 19:00