13 Mei 2026:Askofu Mkuu Rudelli akiwa na Mabalozi 13 katika fursa ya tukio la utoaji wa heshima 13 Mei 2026:Askofu Mkuu Rudelli akiwa na Mabalozi 13 katika fursa ya tukio la utoaji wa heshima 

Heshima zatolewa kwa mabalozi 13 wa Kiti Kitakatifu mjini Vatican

Wanadiplomasia watunukiwa heshima baada ya miaka miwili ya huduma yao katika Kiti Kitakatifu.Ni katika hafla ya kumbukizi ya kuhitimisha mwaka mmoja tangu Papa Leo XIV alipochaguliwa kuwa katika kiti cha Mtume Petro.

Vatican News

Jumanne tarehe 12 Mei 2026 mjini Vatican katika fursa ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwa Papa Leo XIV, ilifanyika hafla ya kutoa heshima za kiutamaduni zilitolewa kwa mabalozi wa nchi mbali mbali wanaowakilisha nchi zao mjini Vatican ambao angalau wametimiza miaka miwili ya huduma yao katika Kiti Kitakatifu.

Katibu Msaidizi wa Vatican wa Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican, Askofu Mkuu Paolo Rudelli, aliwasilisha nembo na maandishi yanayolingana kwa wanadiplomasia 13 waliopokea kwa jina la: “Cavaliere” au “Dama di Gran Croce dell’Ordine Piano.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

14 Mei 2026, 09:40