Tristan Harris:“Tishio halisi ni mbio za kutafuta AI yenye nguvu zaidi"

Katika hafla ya mkutano wa kimataifa:"Kuhifadhi Sauti na Nyuso za Binadamu,"filamu ya maandishi "The AI Doc,"ilioneshwa mjini Vatican.Katika mazungumzo na vyombo vya habari vya Vatican, mwanzilishi mwenza wa Kituo cha Teknolojia cha Ubinadamu na mmoja wa wahusika wakuu wa filamu hiyo,alionya kuhusu hatari kwa utu wa binadamu na mawazo muhimu na anamtazama Papa Leo XIV kama mtetezi anayewezekana wa mjadala wa kimataifa kuhusu AI.

Fabio Colagrande – Vatican.

Katika mjadala wa kimataifa kuhusu akili unde, unaozidi kuakisiwa na maswali ya kimaadili, kisiasa, na kianthropolojia, Vatican inatafuta kufungua nafasi ya majadiliano inayochanganya tafakari ya kitaaluma na tafakari ya kiutamaduni na simulizi. Kabla ya mkutano wa kimataifa "Custodire voce e volti umani" yaani kuhifadhi sauti na sura" uliofadhiliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano mnamo tarehe Mei 21 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, Maktaba ya Filamu ya Vatican iliandaa onyesho la faragha la makala  kuhusu:The AI Doc: Or How I Became An Apocaloptimist, yaani Hati ya Akili Unde: Au Jinsi  gani nimekuwa Mtetezi wa Matumaini ya mwisho wa dunia” iliyoongozwa na Daniel Roher na Charlie Tyrell na kutayarishwa na Daniel Kwan, ambaye tayari alishinda tuzo ya Oscar kwa film ya ‘Everything Everywhere All at Once’ yanni “Kila kitu, Kila Mahali, Yote kwa Mara Moja.

Mkutano wa Kiimataifa mnamo 21 Mei 2026 Kuhusu:Kuhifadhi sauti na Nyuso za kibinadamu
Mkutano wa Kiimataifa mnamo 21 Mei 2026 Kuhusu:Kuhifadhi sauti na Nyuso za kibinadamu

Filamu hii iliwasilishwa kama onyesho la kwanza la dunia mnamo Januari iliyopita katika Tamasha la Filamu la Sundance na baadaye pia barani Ulaya, ambayo inakusanya sauti za wahusika wakuu, wasomi na wakosoaji katika ulimwengu wa akili unde(AI). Mtengenezaji wa filamu Daniel Roher, ambaye anakaribia kuwa baba, anaanza safari ya kuelewa maana ya mapinduzi ya akili unde (AI), akiwahoji wataalamu zaidi ya 40, wakiwemo Wakurugenzi Wakuu wa OpenAI, Anthropic, na Google DeepMind. 

Filamu kuhusu AI
Filamu kuhusu AI

Makala hii inachunguza hatari za kuwepo na ahadi za ajabu za mashine ikisawazisha wasiwasi wa mwisho wa dunia na matumaini ya kuelewa ni aina gani ya ulimwengu ambao mtoto wake  atarithi. Kupitia uchunguzi huu wa kibinafsi, Roher anatafuta kujibu swali la msingi: je, ni kitendo cha wazimu au matumaini kumleta mtoto duniani katika enzi inayotawaliwa na akili unde? "Hili ndilo kosa la mwisho tunaloweza kamwe kulifanya.” Kifungu hiki kinafupisha kikamilifu mada kuu ya makala hii: kwa akili unde unde yenye akili nyingi, ubinadamu unakabiliwa na teknolojia yenye nguvu sana kiasi kwamba kosa moja katika maendeleo yake linaweza kuwa lisiloweza kurekebishwa na kusababisha kifo.

Filamu hiyo pia inamshirikisha Tristan Harris, mwanzilishi mwenza na rais wa Kituo cha Teknolojia ya Binadamu,(Center for Humane Technology,)mojawapo ya filamu zinazosikilizwa sana kimataifa kuhusu uhusiano kati ya teknolojia, utunzaji wa binadamu, na demokrasia. Katika tukio la onesho hilo mjini  Vatican, Harris alitoa mahojiano na Vatican Radio – Vatican News.

Wakati wa mahojiano na Tristan Harris kuhusu Filamu ya AI
Wakati wa mahojiano na Tristan Harris kuhusu Filamu ya AI

Kutafuta Njia ya Tatu

Alipoulizwa kuhusu maana ya "matumaini ya mwisho wa dunia (apocalottimismo ) iliyoibuliwa na kichwa cha makala hiyo, Harris alieleza kwamba hoja si kuchagua kati ya matumaini na kukata tamaa, bali ni kuhoji uwezo wa kutenda mbele ya hatari halisi. Kuhusiana na marejeo yake ni filamu ya "The Day After," yaani, “Siku moja baadaye” ambayo katika miaka ya 1980 ilisaidia kuleta hatari ya vita vya nyuklia kwa ufahamu wa pamoja. "Filamu hiyo ilianzisha katika ufahamu wa pamoja uwezekano wa matokeo ambayo hakuna mtu aliyeyataka," Harris alisema, akikumbuka jinsi hali hiyo pia ilisaidia kuandaa njia ya mazungumzo ya kwanza ya udhibiti wa silaha. Kulingana na Harris, mfano huu unatusaidia kuelewa changamoto ya akili unde: "Inaendana kikamilifu na masuala ambayo Vatican imeshughulikia kihistoria, yaani jinsi ya kutafuta njia ya tatu na kuepuka kuongezeka kwa mbio za silaha."

Vitisho vya mbio za AI zinazozalisha

Kuhusu hatari za haraka za Akili Unde(AI) zinazozalisha, Harris aliorodhesha kadhaa: kuanzia kuhamishwa kwa kazi hadi uzushi wa kina, kuanzia ulaghai hadi wizi wa mali miliki na utambulisho wa sauti. Kulingana na Harris, makampuni na serikali zinapitia ushindani huu kama changamoto ya kuwepo, ambapo uharibifu wowote wa dhamana una hatari ya kuonekana kuwa wa haki ili kuendelea mbele. "Watu katika Bonde la Silicon wanauona ushindani huu wa silaha kama suala la kuwepo. Lazima wawe wa kwanza." Alisema, ni mabadiliko haya yanayosababisha vitisho vingine vingi: ukosefu wa ajira kwa wingi, matumizi mabaya ya nyuso na sauti za binadamu, na kuyumba kwa jamii.

Nataša Govekar,Paolo Ruffini, na Tristan Harris katika chumba cha filamu -Vatican.
Nataša Govekar,Paolo Ruffini, na Tristan Harris katika chumba cha filamu -Vatican.

Madhara ya Mitandao ya Kijamii

Kisha Harris alielekeza umakini kwenye athari zinazoonekana tayari za majukwaa ya kidijitali. Kwa maoni yake, bado hakuna ufahamu kamili wa uharibifu unaosababishwa na mfumo wa kiuchumi wa mitandao ya kijamii. "Ni kama samaki anayeogelea majini na kuulizwa anafikiria nini kuhusu maji," alisema. Mfumo huo, anaelezea, umeundwa ili kuongeza umakini, marudio ya matumizi, na ushiriki, pamoja na matokeo ambayo yanajumuisha kulazimishwa, kutengwa, na kupungua kwa utambuzi. Akirejea tafiti kadhaa, Harris aliakisi ugumu ulioongezeka katika umakini na kujifunzai, na pia anaonya dhidi ya matumizi yasiyo na ukosoaji wa akili unde katika michakato ya utambuzi.

Filamu -Makala kuhusu Akili Unde
Filamu -Makala kuhusu Akili Unde

Jukumu la Papa

Hatimaye, Harris aliazingatia jukumu linalowezekana la Kanisa na Papa Leo XIV katika mjadala wa kimataifa kuhusu akili unde. "Papa Leo amekuwa kiongozi wa ajabu katika kuvutia umakini kwa kile tunachopaswa kulinda: utu wa binadamu, ubunifu wa binadamu, mawazo muhimu," alisema. Lakini, kwa maoni yake, hatua moja muhimu inabaki: kutaja waziwazi mbio za kimataifa za akili unde kama tishio la kimfumo. Marejeo hayo yalionekana wazi kwa Papa Yohane XXIII katika Waraka wake wa Pacem in Terris, uliochapishwa wakati wa kilele cha Vita Baridi, wakati Kiti Kitakatifu kilipoitaka dunia kubadilisha mantiki ya kupanda vita  kwa kasi na ile ya kufanya mazungumzo.

Harris pia alikumbuka lugha ambayo Mtaguso wa II wa Vatican baadaye ungefafanua mbio za silaha kama tishio kwa binadamu. "Ninaamini mbio za silaha za AI lazima zichukuliwe kama hatari," alisema. Kwa hivyo tumaini lake kwa Papa: "Ningependa kumuona Papa Leo akiwakusanya viongozi wa dunia hapa na kuwaambia: hamtaondoka hadi mtakapopata suluhisho," akimaanisha roho ya Reykjavik. Kwa maoni ya Harris, changamoto haiwezi kuachwa kwa ushindani wa kiuchumi au Utafiti wa vipengele vya kijiografia vinavyoathiri hatua za kisiasa pekee,  badala yake: inahusu mustakabali wa binadamu.

Mkutano kuhusu kuhifadhi sauri na sura za kibinadamu katika muktadha wa AI
Mkutano kuhusu kuhifadhi sauri na sura za kibinadamu katika muktadha wa AI

Imesasishwa  tarehe 23 Mei 2026  saa 7.10 mchana na Angella Rwezaula.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

 

23 Mei 2026, 12:14