Vatican,AI:Majadiliano kuhusu Maadili,Vyombo vya Habari na Mustakabali wa Binadamu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mkutano wa Kimataifa kuhusu Akili Unde umefanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana Roma, kwa siku nzima tarehe 21 Mei 2026, ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu na Mfuko wa Kipapa wa Mtakatifu Yohane XXIII, katika fursa ya Siku ya LX ya Hupashanaji habari Ulimwenguni 2026. Mkutano huo uliongozwa na mada: “Kuhifadhi Sauti na Nyuso za Binadamu,” ambayo ni kauli mbiu iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Leo XIV kuongoza siku hiyo iliyoadhimishwa Dominika ya Kupaa kwa Bwana Mbingu tarehe 17 Mei 2026. Mkutano huu wa kimataifa pia umefanyika hata hivyo siku chake kabla ya kuchapishwa kwa Wosia wa kwanza wa Baba Mtakatifu tarehe 25 Mei 2025, unaoongozwa na kauli mbiu: Magnifica Humanitas, unaojikita juu ya ulinzi wa mwanadamu katika enzi ya Akili Unde na Uhalifu. Kwa hakika Mkutano huo ulifungua mjadala mkuu wa Kimataifa kuhusu moja ya maswali muhimu zaidi ya wakati wetu ya jinsi ya kuhifadhi nyuso, sauti, na mawazo ya binadamu katika enzi hizi za matumizi ya mashine.
Mwaliko wa kujenga uhusiano wa dhati,kulingana na uwajibikaji,ushirikiano na elimu
Katika ujumbe wa siku ya hupashanaji habari duniani, Baba Mtakatifu Leo XIV alitambua changamoto ya akili unde, kama suala la kibinadamu, huku akionya dhidi ya hatari kwamba kuigiza mahausiano, hisia, na hata utambulisho binafsi, unaweza kubadilisha muundo wa kuishi pamoja kwa binadamu. “Swali tunalojali si kile ambacho mashine inaweza au itaweza kufanya, bali ni kile tunachoweza na tutaweza kufanya,” Papa alikazia. Katika hilo alitoa hata “mwaliko wa kujenga uhusiano wa dhati na zana hizi, kulingana na uwajibikaji, ushirikiano, na elimu. Ikumbukwe tangu mwanzo wa upapa wake, Baba Mtakatifu Leo XIV ametambua wazi juu ya akili unde kama changamoto mpya ya kijamii, ambayo itashughulikiwa kwa kuzingatia mafundisho Jamii ya Kanisa, heshima ya kazi, na haki.
Dk.Ruffini:Kuhifadhi si kuweka kitu kwenye kabati,ni kumtunza mtu au kitu kwa upendo
Katika ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa, awali ya yote utangulizi ulitolewa na Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, kwa kuwakaribisha wageni na kuweka waziwazi wa muktadha wa ujumbe wa Papa Leo XIV na tafakari ya Kanisa kuhusu uvumbuzi wa kiteknolojia. Kwa hiyo alisema kuhusu “ulinzi wa kuhifadhi, unapowahusu watu, ni neno gumu. Haimaanishi kuweka kitu kwenye kabati, bali kumtunza mtu au kitu kwa upendo,” huku akisisitiza jinsi ambavyo malezi yanayotokana na Papa, si aina ya uhifadhi tulivu, bali ni utekelezaji hai wa uwajibikaji.
Kutofautisha kati ya ukweli na uigizaji,hesabu za takwimu
Dk. Ruffini alisisitiza hatari ya kukabidhi mawazo ya binadamu katika mifumo ya akili unde hatua kwa hatua, huku akikumbusha moja ya wasiwasi mkuu wa ujumbe wa Papa Leo XIV hasa “hatari kubwa zaidi iko katika kukubali tu wazo kwamba maarifa si yetu tena; na kwamba kitu ambacho sisi wenyewe tumekijenga kwa mashine, majukwaa, au mifumo ya otomatiki kinaweza kuaminiwa nasi kufikiri badala yetu." Dk. Ruffini aidha alielezea juu ya “mabadiliko ya sasa ya mfumo ikolojia wa habari kama changamoto inayoathiri moja kwa moja uandishi wa habari, elimu, na uraia,” akisisitiza hitaji la “kutofautisha kati ya ukweli na uigizaji, kati ya maneno ya kibinadamu na hesabu za takwimu, kati ya maarifa na otomatiki. Uchumi wa mawasiliano hauwezi na haupaswi kutenganisha hatima yake na kushiriki ukweli," kuongeza katika Hotuba yake ya kina kwamba, “ni uwazi wa vyanzo, uwajibikaji, na ubora wa habari kama vigezo muhimu vya kurejesha umuhimu wa mtu.
Kard.De Mendonça:mwanadamu anapita kiasi
Kwa upande wa Hotuba ya Kardinali, José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, aliwakaribisha washiriki wote na kukazia juu ya mada hiyo kwa tafakari pana ya kianthropolojia na kiutamaduni, huku akikumbusha moja kwa moja ujumbe wa Baba Mtakatifu Leo XIV. "Jina linalotukutanisha, kuhifadhi sauti na nyuso za wanadamu, kiukweli ni programu na ni taaluma ya imani katika ubinadamu.” Kardinali alikumbusha jinsi ambavyo utamaduni wa ukristo, uso na sauti si vipengele vya kutambua tu, bali ni maonesho ya kina ya mtu na uhusiano. Mwanadamu hawezi kamwe kupunguzwa hadi ukweli fulani, wasifu, au mashine. Mwanadamu anapita kiasi, fumbo, na mvuto kila wakati.” Kardinali Tolentino de Mendonça alionya kuhusu hatari za kuiga mahusiano bandia, kuamsha gumzo zenye hisia, na mazingira ya kidijitali yaliyojengwa karibu na wasifu wa kibinafsi, wenye uwezo wa kubadilisha sarufi ya kukutana kwa wanadamu. Lakini msisitizo wa mwisho ulikuwa juu ya uwezekano wa utambuzi chanya: Changamoto inayotusubiri si kuzuia uvumbuzi wa kidijitali, bali kuuongoza, sambamba na mwaliko wa Papa Leo XIV wa kujenga muungano muhimu na wenye uwajibikaji na teknolojia.
"AI inabadilishaje uandishi,jamii na Jumuiya?"
Baada ya hotuba yake ulifuata mjadala mpana ulioletwa mezani na watu mashuhuri kutoka katika ulimwengu wa habari, utafiti, na uvumbuzi wa kiteknolojia, ukithibitisha hamu ya Vatican ya kuhamasisha mjadala mpana na wa kimataifa kweli. Wazungumzaji maarufu katika sehemu ya kwanza iliyoongozwa na mada ya swali: “AI inabadilisha uandishi,jamii na Jumuiya? , kwa kuratibwa na Dk. Alessandro Gissoti, Naibu Mkrugenzi wa Uhariri, wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano walikuw: Mirijana Grbesa Zanzerovic Profesa wa Chuo Kikuu cha Zagreb Crotia na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam kuhusu usalama mtandaoni na uwezeshaji wa waundaji na watumiaji wa maudhui(MSI-eSEC) katika Baraza la Ulaya; Kashmir Hill wa New York Times, anayejulikana kwa uchunguzi wake kuhusu faragha, utambuzi wa uso, na ufuatiliaji wa kidijitali; Vineet Khosola, Mtendaji wa vyombo vya habari, Afisa Mkuu wa Teknolojia wa Washington Post; Eli Pariser, Mwelekezi Mwenza Mpya wa umma.
"Je, mifumo ya akili Unde(AI)inazidisha ukosefu wa usawa wa kijamii na dhuluma?"
Sehemu ya Pili kwa kuongozwa na mada: “Je, mifumo ya akili Unde (AI) inazidisha ukosefu wa usawa wa kijamii na dhuluma?kwa kuratibiwa Natasa Govekar, Mkurugenzi wa Kichungaji wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, wazunguzaji walikuwa: Joy Buolamwini, mtaalam na mwanzilishi wa maadili ya mashine na haki za kijamii, sauti inayoongoza katika kukemea upendeleo katika mifumo ya utambuzi wa uso; Paola Ricaurte Quijano, Profesa wa Idara ya Vyombo vya Habari na Utamaduni wa Kidijitali; Benjamini Rosman, mtaalamu wa kujifunza kwa mashine na sayansi ya kompyuta.
"Muungano unaowezekana"
Sehemu ya tatu ilikongozwa na mada ya “Muungano unaowezekana,” kwa kuratibiwa na Sr Nina Krapic, Naibu msemaji Mkuu wa Vyombo vya habari vya Kiti Kitakatifu vya Baraza la Kipapa la Mawasiliano, waliozungumza walikuwa: Mitchell Baker, mwanzilishi mwenza wa mradi wa Mozilla; Tristan Harris, mmoja wa wakosoaji maarufu wa uchumi wa umakini; Daniel Dzuban mhusika katika utawala wa majukwaa ya kidijitali na uthibitishaji wa uhalisi wa maudhui; na Neil Lawrence, Mtaalamu wa kina katika kujifunza mashine, Mwanasayansi mkuu wa Trent wa AI.
"Usikatae uwezo wako wa kufikiri"
Sehemu ya nne na ya mwisho iliongozwa na mada: “Usikatae uwezo wako wa kufikiri.” Mratibu alikuwa ni Askofu Paulo Tighe, Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Wazungumzaji walikuwa ni wawakilishi wa UNESCO, Divina Frau Meigs na Adeline Hulin; Justin Kings, kutoka Umoja wa Utangazaji wa Ulaya, EBU. Kwa njia hiyo uwanja huo ulikuwa mpana kuanzia vyuo vikuu vya Ulaya, Amerika, na Afrika na wazungumzaji walionesha utofauti mkubwa wa hali halisi ya mapokezi na kwa ushiriki wa wazungumzaji wanawake wengi. Kila mwisho wa sehemu mada, wazunguzamji walijibu maswali ya wasilikizaji yaliyotumwa kupitia mtandaoni, na ambapo ilirahisisha kutopoteza muda. Siku iliongozwa pia na mapumziko ambayo yaliambatana vipindi vitatu vya mapumziko kwa ajili ya chai na chakula na chai na mazungumzo na watu mbali mbali kujuana.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.