2026.05.22:Washiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari na Ujuzi wa Kidijitali wakutana na Papa Leo XIV. 2026.05.22:Washiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari na Ujuzi wa Kidijitali wakutana na Papa Leo XIV.  (@Vatican Media)

Wataalamu wa Mawasiliano duniani wajadili kuhusu:Kuhifadhi Sauti na Nyuso za Binadamu katika Enzi za Akili Unde

Wakati kijazi kinapoingia katika uhusiano wa kawaida wa kibinadamu,ubunifu,ukweli na uwajibikaji katika uandishi wa habari,kukosekana usawa na ukoloni wa kidijitali,mashine si Binadamu,haya na mengine yaliibuka kutoka kwa wazungumzaji 14 wa Kimataifa katika mkutano ulioongozwa na Kauli Mbiu ya Ujumbe wa Papa Leo XIV wa Siku ya 60 ya Hupashanaji Habari 2026:"Kuhifadhi Sauti na Nyuso za Binadamu katika Enzi za Akili Unde.”Mkutano ulifanyika Mei 21.Papa amekutana nao.

Fabio Colagrande na Angella Rwezaula – Vatican.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Leo XIV kwa ajili ya Siku ya 60 ya Hupashanaji Habari Ulimwenguni 2026  ni kichocheo kikubwa na cha thamani katika mawasiliano ya kibindamu katika Enzi za Akili Unde(AI) ambapo ulisikika tena na kudhihirika katika mawasilisho ya wazungumzaji 14 wa Kimataifa katika mkutano  ulioongozwa na Mada: "Kuhifadhi Sauti na Nyuso za Binadamu."  Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, na Mfuko wa Kipapa wa Mtakatifu Yohane XXIII, na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana tarehe 21 Mei 2026. Katika Ukumbi Mkuu wa Chuo cha Kipapa, uliwaona Waandishi wa habari, walimu, mameneja wa teknolojia, na wataalamu wa maadili ya kidijitali kutoka Ulaya, Marekani, Amerika Kusini, na Afrika wakishughulikia  swali lile lile: “Je tunawezaje kuhifadhi heshima ya mtu katika mfumo ikolojia wa habari na uhusiano unaozidi kuumbwa na mashine?

Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wamekutana na Papa Leo XIV
Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wamekutana na Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Mashine mpya kwa walinzi waapya wa Habari?

Mara baada ya Hotuba za Utangulizi kutoka kwa Wakuu wa Mabaraza ya Kipapa ya Mawasiliano na Elimu na Utamaduni, aliyefungua mjadala alikuwa ni Marijana Grbeša Zenzerović,  Profesa wa Mawasiliano ya Kisiasa katika Chuo Kikuu cha Zagreb, ambaye alielezea mfumo ikolojia wa vyombo vya habari uliobadilika sana: “vyombo vya habari vya kiutamaduni vinapoteza umuhimu wake, huku mashine zikiwa "walinzi" wapya wa habari. Ingawa televisheni ina jukumu miongoni mwa baadhi ya makundi ya watu, mitandao ya kijamii inatawala miongoni mwa vijana, na mamlaka inayohusishwa na waundaji, watu wenye ushawishi, na "wanaoshawishi waandishi wa habari" inaongezeka. Kwa mujibu wake alibainisha “hatari ni taarifa potofu nyingi zinazozidishwa na AI ya kuzalisha, inayoweza kuunda picha, video, na utambulisho wa bandia unaoaminika, na kusababisha siasa bandia za kweli.”

Bi Marijana Grbesa Zenzerovic
Bi Marijana Grbesa Zenzerovic   (@Vatican Media)

Wakati kijazishi(chatbot)kinapoinga katika uhusiano wa kawaida wa kibinadamu

Kwa upande wa Kashmir Hill, Mwandishi wa habari wa New York Times alielekeza umakini wake kwenye athari za kijazishi (Chatbot) ya gumzo kwenye maisha ya kibinafsi. Zana hizi zinaweza kuonekana kuwa za huruma na za kutuliza, hadi kufikia hatua ya kuwa watu wa siri wa mfano. Lakini muundo wake unaolenga ushiriki unaweza kuwafanya kuwa hatari, hasa unapoelekea kumfurahisha mtumiaji badala ya kumrekebisha. Hill alikumbuka kisa cha Adam Raine mwenye umri wa miaka kumi na sita, ambaye alifariki baada ya mazungumzo marefu na kijazishi(chatbot) cha gumzo, akisisitiza kwamba “hatari hiyo inamhusu mtu yeyote anayetoa hitaji la kusikiliza na kuthibitisha teknolojia hizi.”

Ubunifu,Ukweli, na Uwajibikaji katika Uandishi wa Habari

Vineet Khosla, Afisa Mkuu wa Teknolojia wa Washington Post, alijikita zaidi kwenye fursa, huku akielezea jinsi akili unde  inavyojumuishwa katika michakato ya uhariri: uendeshaji otomatiki wa kazi zinazojirudia, utafiti wa hati, zana shirikishi kwa wasomaji, na maudhui ya sauti yaliyotengenezwa bandia. Lengo: kuimarisha, si kuchukua nafasi ya, kazi ya uandishi wa habari. Lakini kwa sharti moja: kudumisha ukweli kama kigezo kinachotofautisha na uaminifu wa umma kama mali muhimu.

Kwa upande wake Eli Pariser, mkurugenzi mwenza wa New_Public, alitafakari juu ya  ubora wa maisha ya kidijitali. Yeye alibainisha  kwamba majukwaa yanaahidi muunganisho lakini mara nyingi hutoa upweke, yakiwa yameundwa ili kuongeza umakini na mapato. AI inaweza pia kuwa "vimelea," inayolenga utegemezi wa mtumiaji, au "prosocial," yaani inayohusiana au inayoashiria tabia ambayo ni chanya, yenye manufaa, na inayokusudiwa kukuza kukubalika na urafiki wa ustawi wa pamoja kijamii.

Kukosekana kwa Usawa na Ukoloni wa Kidijitali

Katika jopo lililojitolea kwa kukosekana kwa usawa, Paola Ricaurte Quijano, msomi na mtaalamu wa maadili ya akili Unde  wa Mexico, alikemea asili ya "uchimbaji" wa mfumo huu wa kiteknolojia, ambao huzingatia utajiri na nguvu kwa kutumia nguvu kazi isiyoonekana, rasilimali kutoka nchi maskini, na hata data, hofu, na matamanio ya watumiaji. Mifumo ya kimashine(kialgorithimu), alisema, inahatarisha kuendeleza mantiki za kikoloni na kibaguzi, na kufuta tamaduni na lugha zilizotengwa

Upande Mbaya wa AI: Uigaji wa Huruma na Ubaguzi

Kwa upande wa Benjamin Rosman wa Afrika Kusini, na profesa katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand na mwanzilishi wa Lelapa AI, kampuni inayofanya kazi kwenye teknolojia za AI zinazozingatia miktadha na lugha za watu asilia, alitambua uwezo wa kushangaza wa mifumo ya lugha ya kuiga huruma na uwepo wa binadamu, kiasi kwamba baadhi ya vijana huitumia kama wanasaikolojia. Lakini uaminifu huu unaibua maswali mazito ya kimaadili, hasa ikiwa zana zilizoundwa ili kuongeza ushiriki zinajifunza kutumia hofu, hasira, au utambulisho wa kikabila. Hata hivyo, kwa Rosman, Kusini mwa Dunia haipaswi kuteseka na teknolojia hizi, bali kusaidia kuziunda.

Hata hivyo akifunga sehemu ya pili ya asubuhi  Joy Buolamwini, mwanzilishi wa Algorithmic Justice League, yaani (Ligi ya Haki ya Algorithmic), ambaye alilaani ubaguzi wa rangi na kijinsia uliomo katika mifumo ya utambuzi wa uso, ambao tayari unawajibika kwa makosa na kukamatwa kwa watu bila haki. Mwanaharakati na mshairi aliibua hatari ya jamii ya ufuatiliaji, ambapo akili unde hufuta utambulisho, ubunifu, na hata maisha ya binadamu, hasa kwa maendeleo ya silaha zinazojiendesha zenyewe. Wito wake wa  mwisho ulikuwa wazi: sheria za kimataifa, usimamizi wa binadamu, na haki zilizo wazi kabla ya kasi ya uvumbuzi kuzidi uwezo wa kimaadili wa kuitawala.

Joy Buolamwini akisalimiana na Papa
Joy Buolamwini akisalimiana na Papa   (@Vatican Media)

"Muungano Unaowezekana"

Jopo la kwanza la alasiri, lenye kichwa "Muungano Unaowezekana," liliongozwa na Sista Nina Krapic, Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Kiti Kitakifu. Wazungumzaji walijumuisha Mitchell Baker, mwanzilishi mwenza wa Mradi wa Mozilla na Mfuko wa Mozilla; Daniel Dzuban, rais wa mpito wa Muungano wa Uzalishaji na Uhalisi wa Maudhui (C2PA); Mkuu wa Washirika wa Kimkakati wa Uhalisi wa Maudhui katika Sony Electronics; Tristan Harris, mwanzilishi mwenza wa Kituo cha Teknolojia ya Binadamu; na Neil Lawrence, Profesa wa Kujifunza kwa Mashine katika Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza, na Mwanasayansi Mkuu katika Trent ya AI.

Mashine Si Binadamu

Lawrence alianzisha hotuba yake kwa kurudia utabiri wa mchumi na mshindi wa Tuzo ya Nobel Herbert Simon, ambao baadaye ulithibitishwa kuwa sahihi, kama haukuzidishwa, na ujio wa AI: "Utajiri wa taarifa husababisha umaskini wa umakini." Thamani hii, kwa miongo kadhaa, imekuwa ikipungua polepole na mashine, ambazo zinazidi kujihusisha kati ya watumiaji na taarifa wanazotumia. "Imechukua nguvu ya mawazo yetu, lakini si chanzo." Kile ambacho teknolojia haina ukilinganisha na wanadamu ni vipengele viwili: "uelewa wa kiutamaduni ambao tumejenga kwa vizazi vingi na udhaifu wa kibinadamu, ambao unatufanya tuwajibike kwa kila mmoja." Sio udhaifu, bali "msingi wa dhamiri." Imani ambayo, profesa alielezea, Kanisa limeiunga mkono kwa karne nyingi, ikihifadhi, kama kichwa cha mkutano kinavyosema, "sauti na nyuso za wanadamu" kupitia mabadiliko ya historia.

Bwana Neil Lawrence
Bwana Neil Lawrence   (@Vatican Media)

Muungano wa Kulinda Ukweli

Dzuban alisifu ujumbe wa Papa Leo XIV wa Siku ya Hupashanaji habari Ulimwenguni 2026, huku akiamini kuwa unatoa picha sahihi ya uhusiano kati ya ubinadamu na teknolojia mpya: Je, teknolojia hizi zitakuwa moto utakaoboresha jamii au ule utakaoiteketeza? Swali hili liliongoza uwasilishaji mzima, ambao ulijumuisha onesho la vitendo la jinsi akili unde inayozalisha inaweza kuunda picha kutoka kwa mstari wa maandishi katika sekunde chache tu. Jambo muhimu ni kwamba inaweza kutoa uwakilishi wa hali halisi zilizopo, lakini pia kuvumbua mpya, hivyo kutoa maudhui "bila sauti au nyuso za kibinadamu." Kwa hivyo, tishio la AI si la "roboti ya wauaji," bali ni mmomonyoko unaoendelea wa dhana ya ukweli halisi, unaopatikana haraka, bila gharama yoyote, na mara nyingi ni vigumu kutambua, hasa kwa watumiaji walio katika mazingira magumu zaidi.

Kuhusu uzoefu wake wa kitaaluma katika Kampuni ya Sony ya vifaa vya umeme, Dzuban alisisitiza kuwepo kwa zana kama vile programu ya Uthibitishaji wa Maudhui, inayotangazwa na C2PA, ambayo hutoa taarifa kuhusu uhalisi wa picha mtandaoni. Huu ni mfano halisi wa muungano kati ya makampuni yaliyojitolea kupitisha viwango vya pamoja.  Na katika kuhojiwa na vyombo vya habari vya Vatican kando ya Mkutano huo kuhusu suala la Kanisa na hali hii yeye altoa tumaini la mwisho kwamba "Katikati ya ugumu wa uongozi wa kitaifa katika AI, Kanisa linaweza kuchukua jukumu la msingi na kuendesha maendeleo."

Dalili Nyeusi na Ishara za Matumaini

Katika hatua hii, swali linakuwa: ni nini kinachoendesha baadhi ya matatizo yanayotokana na AI? Swali la msingi, kulingana na Harris, ambaye "tatizo lililoandaliwa vizuri ni tatizo lililotatuliwa nusu." Harris, ambaye alifanya kazi kwa miaka mingi huko Silicon Valley alionya kuhusu hatari za teknolojia mpya. "Nionyeshe motisha nami nitakuonesha matokeo," alisema, akimnukuu mwekezaji Charlie Munger, kuakisi  jinsi kampuni za AI zinavyounda "mustakabali usio wa kibinadamu," unaoendeshwa na mbio za maendeleo na uongozi wa kiteknolojia. "Tunataka AI iwe chombo," alisema mtaalamu huyo, pia akirudia maneno ya Papa Leo XIV.

Bwana Tristan Harris
Bwana Tristan Harris   (@Vatican Media)

Hata hivyo, kulingana na uchambuzi wake, hii haionekani kuwa mwelekeo unaochukuliwa na kampuni kama OpenAI na Anthropic, miongoni mwa kampuni zinazoongoza katika sekta hiyo. Motisha unaohalalisha uwekezaji wao mkubwa, kiukweli, ni mbio za kuchukua nafasi ya kazi ya binadamu.  Kama ilivyotokea tayari kwa rasilimali kama vile mafuta nchini Venezuela au madini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kile kinachoonekana kuwa baraka mwanzoni kinaweza kugeuka kuwa laana. Rasilimali, badala ya kuelekezwa kwa manufaa ya pamoja, huishia kuchochea miundombinu inayoendeshwa hasa na faida. Hatari hiyo hiyo, kulingana na tafsiri hii, inarudiwa katika uwanja wa AI, hata nchini Marekani.

Wakati mwandishi wa habari wa New York Times alipomuuliza Peter Thiel, mmoja wa wajasiriamali wenye ushawishi mkubwa katika sekta ya teknolojia, kama spishi ya binadamu itaweza kuishi teknolojia mpya, Thiel hakutoa jibu wazi. Dalili za huzuni, lakini pia ishara za matumaini: "Hakuna mtu anayetaka mustakabali wa kupinga binadamu." Kama vile Papa Yohane  XXIII, katika Waraka wa  Pacem in Terris, alivyoonya dhidi ya mbio za silaha, Ujumbe wa Leo XIV kuhusu AI unaweza pia kutusukuma kutambua kuwepo kwa kitu "kitakatifu" na cha thamani zaidi, chenye uwezo wa kuunganisha ubinadamu zaidi ya faida ya watendaji wachache.

Kufungua Teknolojia Mpya

Baker, akinukuu filamu iliyoshinda Tuzo ya Academy ya 2022, alifafanua AI kama "Kila Kitu, Kila Mahali, na  Kwa Mara Moja." Haiwezekani kutabiri kwa uhakika ambapo maendeleo yake yataongoza ubinadamu, na hivyo kuchochea enzi ya "utata mkubwa. Basi, tunawezaje kujenga miongozo kwa ajili ya mustakabali usio na uhakika kama huo? Ni kupitia kile kinachoitwa"kanuni ya hatua" na "muundo shirikishi," kufungua teknolojia mpya iwezekanavyo kwa mchango wa pamoja. Mbinu inayokumbusha falsafa ya programu huria, inayoweza kubadilishwa na kuboreshwa na mtu yeyote. Wazo hili linaenea kwa sekta nzima ya teknolojia: kila mtu anapaswa kuweza kushiriki katika faida za kiuchumi na kitamaduni zinazotokana na uvumbuzi. Mfano mkuu ni kivinjari cha Firefox, kilichotengenezwa na Mozilla. "Kwa nini ushiriki? Usalama unahakikishwaje? ni baadhi ya maswali ambayo Baker amelazimika kujibu kwa miaka mingi. Mabadiliko ya mtazamo kulingana na uwazi na ushirikiano yalionekana kuwa magumu kufikiria mwanzoni, lakini yameingizwa polepole. Kulingana na Baker, vivyo hivyo vinapaswa kutokea pia kwa mifumo ya AI.

Wazungumzaji katika Mutano wa Kimataifa
Wazungumzaji katika Mutano wa Kimataifa

Usikate Tamaa Kufikiria

Jopo la pili, Alasiri  lenye kichwa: "Usikate Tamaa Kufikiria," liliongozwa na Askofu Paul Tighe, Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Wazungumzaji walijumuisha Rayén Condeza Dall'Orso, profesa katika Kitivo cha Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Chile; makamu rais wa sehemu ya Utafiti wa Elimu ya Vyombo vya Habari (MER) ya IAMCR; na Divina Frau-Meigs, profesa mstaafu na mwanasosholojia wa vyombo vya habari katika Chuo Kikuu cha Sorbonne Nouvelle, Ufaransa. Adeline Hulin, mkuu wa kitengo cha Uandishi wa Habari na Ujuzi wa Kidijitali katika UNESCO; na Justin Kings, Mkurugenzi wa Chuo cha EBU (Umoja wa Utangazaji wa Ulaya).

AI katika Huduma ya Uandishi wa Habari

Hulin alilenga hatari zinazohusiana na matumizi ya AI, akisisitiza jinsi inavyoweza kupunguza shughuli za utambuzi, kutoa "ndoto," na kuchochea mienendo hatari ya kisaikolojia. Miongoni mwa haya ni kudhoofika kwa mawazo muhimu, ambayo husababisha, kwa mfano, kuchanganya umaarufu na mamlaka. Shughuli za UNESCO, ambazo Papa Leo XIV atazitembelea mwezi Septemba katika makao makuu yake ya Paris wakati wa Ziara yake ya kitume, zinaendana na ujumbe wa Papa wa kukabiliana na hatari hizo. Kisha Hulin akajikita katika dhana ya "ujuzi wa vyombo vya habari": Uwezo wa kuchambua na kuunda maudhui katika miundo yote ya mawasiliano. Kulingana na utafiti wa UNESCO, nchi 171 zinakuza aina hii ya elimu, ingawa kuna tofauti kubwa kati ya mabara: Imejumuishwa katika mitaala mingi ya shule za Ulaya, huku barani Afrika usambazaji wake ukibaki mdogo sana. Kwa hivyo, "mapinduzi ya kidijitali," yanapaswa kukua kwa kiwango cha kimataifa, lakini hii inahitaji "ujasiri wa kisiasa."

Shule kama "washawishi wanaoaminika"

Frau-Meigs badala yake alilenga hotuba yake kwenye "kuondoa usanifishaji" wa AI kupitia jukumu la shule. "Lazima tuache kuziona taasisi hizi kuwa za kizamani na kuanza kuziona kama washawishi wanaoaminika," alisema. Profesa pia aliakisi jinsi teknolojia mpya pia zinavyoathiri nyanja za ishara na za kiroho, kama vile imani. Alitaja, kwa mfano, uwezekano wa kuwasiliana na kijazishi(chatbot) cha gumzo vinavyomwiga Yesu, au usambazaji wa picha zilizobadilishwa za watu mashuhuri wa Kanisa, kama vile picha iliyoenea ya Papa Francisko akiwa amevaa koti jeupe linalovutia, sawa na mavazi ya chapa ya kifahari ya Balenciaga.

Mkutano wa Kimataifa
Mkutano wa Kimataifa

Ujuzi Katika Huduma kwa Jamii

Condeza Dall'Orso alitoa mfano kutoka nchi yake ya asili, Chile. Katika utamaduni wa Minga, kwenye Visiwa vya Chiloé, wakazi hushirikiana kwa manufaa ya vijiji vyao, hata kufikia hatua ya kusafirisha nyumba na majengo yaliyoharibika ili kuwasaidia wale wanaohitaji, wakiweka ujuzi na teknolojia za kisanii katika huduma kwa jamii. Kulingana na mzungumzaji, jambo kama hilo linaweza, na lazima, pia kutokea katika muktadha wa AI, na kuweka manufaa ya mtu binafsi na ya pamoja katikati. Hata hivyo, miongoni mwa changamoto kuu zinazozuia maono haya ni "mapengo" mapya yanayotokana na teknolojia za kidijitali: ukosefu wa usawa unaohatarisha kuunda wasomi wapya na mgawanyiko mkubwa wa kijamii, unaochochewa na mitazamo potofu ya ukweli na uhalisia.

Wajibu,Ushirikiano, Elimu

Kings alitoa hotuba ya mwisho, ambayo ililenga nguzo tatu: uwajibikaji, ushirikiano, na elimu. Katika hoja ya kwanza, Kings alitaja data ya EBU, ambayo kulingana na ambayo huduma za vyombo vya habari vya umma ndizo vyanzo vya habari vya kuaminika zaidi katika 91% ya nchi za Ulaya. "AI inafanya taarifa potofu kuwa ngumu zaidi kugundua," alisema. Akizungumzia thamani ya ushirikiano, kisha akakumbuka uzoefu wa Eurovision News Spotlight, mtandao wa kimataifa wa wahakiki wa ukweli waliojitolea kutambua na kuripoti habari za kugushi zinazosambaa mtandaoni. Juhudi hii pia ilihitajika na data iliyokusanywa na EBU kwa ushirikiano na BBC, ambayo iligundua kuwa 45% ya majibu yanayotokana na AI yana angalau kosa moja "kubwa". Hatimaye, Kings alisisitiza jukumu kuu la elimu. EBU inakuza kozi za mafunzo zilizowekwa kwa teknolojia mpya, kwa lengo la kukuza uelewa wa kweli wa kidijitali: utamaduni unaoweza kuwasaidia watu kuelewa, kuvinjari, na kutumia AI kwa uangalifu na kwa ufanisi na kwa uwajibikaji zaidi.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

22 Mei 2026, 16:12