2026.06.27 Mkutano Mkuu Maalum wa Makardinali,kikao cha IV na cha mwisho katika Ukumbi wa Sinodi. 2026.06.27 Mkutano Mkuu Maalum wa Makardinali,kikao cha IV na cha mwisho katika Ukumbi wa Sinodi.  (@Vatican Media)

Kikao cha mwisho cha Mkutano Mkuu kimechunguza Sinodi na ukuhani

Katika sehemu ya kwanza ya kikao cha nne cha kazi kwa Makardinali,baada ya ripoti ya katibu mkuu wa Sinodi,Makardinali walitafakari hitaji la kuwapatia mapadre taswira ya ukuhani ambao ni mzuri,mbunifu,wa kiinjili na wakati huo huo usio wa majivuno.Kiini cha majadiliano kilikuwa kizito kwa sababu ugumu wa michakato ya mashauriano unaweza kuilemea Kanisa hasa linapoitwa kutoa ushuhuda wake katika ulimwengu.

Vatican News

Kuimarisha vipimo vya kujinyima na kihistoria vya sinodi, kuwapa waamini taswira ya upadre ambao ni wa Kiinjili na usio wa kikanisa. Hizi ni baadhi ya mada zilizoibuka katika sehemu ya kwanza ya kikao cha nne cha Mkutano Mkuu Maalum wa Makardinali, kilichofanyika alasiri, Jumamosi tarehe 27 Juni 2026, kuanzia saa 10:00 jioni. Katika taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu iliripoti kwamba,  shughuli hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Sinodi, ikiongozwa na Kardinali Joseph William Tobin, Askofu Mkuu wa Newark, Marekani.

Katika Kikao cha Nne katika Ukumbi wa  Sinodi
Katika Kikao cha Nne katika Ukumbi wa Sinodi   (@Vatican Media)

"Msilitwike Kanisa mzigo"

Baada ya hotuba ya utangulizi ya Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi, Makardinali kadhaa walizungumza. Kulingana na Ofisi ya Vyombo vya Habari, Makardinali walizungumzia hatari kwamba "utata wa mashauriano unaweza kulitwike mzigo Kanisa wakati linapoitwa kutoa ushuhuda." Wakati huo huo, ilirudiwa kwamba Kanisa la kihierarkia na Watu wa Mungu wote wanashiriki, ingawa kwa njia tofauti, katika utambuzi wa kile ambacho Roho anasema kwa Kanisa.

Makardinali pia walisisitiza mchango wa jumuiya za Wakatoliki wa Mashariki, ambao uzoefu wao wa Sinodi unawakilisha mchango mkubwa katika safari inayohusisha Kanisa zima. Sehemu ya kwanza ya kikao ilimalizika saa 11:00 jioni. Baada ya mapumziko, programu hiyo ilijumuisha mazungumzo na Papa Leo XIV, huku washiriki wakiwa huru kuzungumza kwa dakika tatu.

Kikao cha mwisho cha Nne katika ukumbi wa Sinodi
Kikao cha mwisho cha Nne katika ukumbi wa Sinodi   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

27 Juni 2026, 18:30