Ziara ya Kichungaji ya Kardinali Gugerotti nchini Ethiopia
Vatican News
Kardinali Claudio Gugerotti, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, alianza ziara ya kichungaji ya siku kumi nchini Ethiopia ili kukutana, kuunga mkono, na kutia moyo Kanisa Katoliki la Ethiopia, Kanisa la mji mkuu la Sheria ya Kiibada ya Alexandria. Kardinali, aliondoka Roma jioni ya tarehe 1 Juni 2026, na kuwasili Addis Ababa na siku iliyofuata, alikaribishwa na Kardinali Berhaneyesus Demerew Souraphiel, Askofu Mkuu wa Addis Ababa na mamlaka ya juu zaidi ya Kanisa Katoliki la Ethiopia, na Balozi wa Kitume wa Vatican nchini Ethiopia, Askofu Mkuu Brian Ngozi Udaigwe. Kardinali alitembelea Kanisa Kuu la Kikatoliki la Kuzaliwa kwa Bikira Maria.
Mkutano na Patriaki wa Orthodox
Kardinali tarehe 2 Juni alasiri, alimtembelea kwa heshima, Patriaki wa Kiorthodox Abune Matias na Wakatoliki wa Ethiopia, akifuatana na Balozi wa Vatican na Kardinali Souraphiel. Mada kuu ya mkutano huo ilikuwa ni wasiwasi wao wa pamoja kwa amani ya dunia na migogoro mingi inayoathiri watu mbalimbali. Wakati wa mkutano huo, Kardinali Gugerotti alimpelekea Patriaki salamu za dhati za Papa Leo XIV, akielezea shukrani kubwa ya Kanisa Katoliki kwa ushuhuda wa imani ya Kanisa la Ethiopia na kujitolea kwa kuishi pamoja kwa amani miongoni mwa jamii tofauti za kidini na kikabila.
Patriaki Abune Matias alisisitiza uhusiano bora kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Orthodox la Ethiopia la Tewahedo, uhusiano ambao unachangia kwa kiasi kikubwa kukuza utulivu, maridhiano, na amani nchini. Kisha akaomba salamu zake za kidugu zipelekwe kwa Papa Leo XIV, akimtakia aendelee kuliongoza Kanisa Katoliki kwa roho ya upendo, hekima, na kujitolea kwa kichungaji, hasa katika kukuza amani ya dunia, kwani Kanisa la Roma, katika ukubwa wake na kimo chake cha maadili, ndilo mtangulizi wa Ukristo wa kimataifa. Mwishoni mwa mkutano huo, Kardinali Gugerotti alimtakia Patriaki afya njema na huduma ndefu na yenye matunda ya kwa upatriaki na kumkabidhi, kama ishara ya heshima na urafiki wa kidugu, medali ya fedha ya mwaka wa kwanza wa Upapa wa Papa Leo XIV.
Ziara ya Msikiti wa Al-Nejashi huko Tigray
Mnano tarehe 3 Juni, Kardinali alisafiri hadi Tigray, Kaskazini mwa Ethiopia, kutembelea Upatriaki wa Adigrat. Huko Mekelle, alisimama katika Kanisa la Kuzaliwa kwa Maria na kisha, katika kijiji cha Negash, alitembelea huko akiwa pamoja na Balozi wa Vatican na Askofu wa Adigrat, Msikiti wa Al-Nejashi, mahali pa umuhimu mkubwa kwa dini ya Kiislamu na historia ya Uislamu. Msikiti huo una jina la Negus, mfalme wa ufalme wa Axum, ambaye aliwakaribisha Waislamu wa kwanza kufika katika nchi hizi, wakikimbia Arabia, akiwapa ulinzi na ruhusa ya kuishi kwa amani katika eneo lake. Baadhi ya wafuasi wa kwanza wa Muhammad wanaheshimiwa na kuzikwa hapa.
Kardinali alipokelewa na Imam wa msikiti huo, ambaye alielezea historia ya mahali hapo na umuhimu wake wa kidini na kihistoria. Katika tukio hili, maneno yaliyohusishwa na Muhammad yalikumbukwa: "Kwa kuwa mmekaribishwa kama ndugu, kamwe hampaswi kuwashambulia watu wa nchi hii." Hapo walisisitiza juu ya uhusiano mkubwa unaowaunganisha Waislamu wa kwanza hadi Abyssinia na kukumbuka thamani ya ukarimu, kuishi kwa amani, na kuheshimiana kati ya watu na dini. Katika tukio hili, uhusiano bora kati ya Askofu Mkatoliki wa Adigrat na mtu mashuhuri wa Kiislamu uliakisiwa na ishara ya kuishi kwa amani kati ya jamii hizo mbili.
Siku kuu ya Kanisa Kuu la Katoliki la Adigrat
Kardinali Gugerotti kisha alifika Adigrat ambapo alihudhuria siku kuu ya Kanisa Kuu Katoliki la jiji hilo mbele ya waamini wengi wa Kiorthodox. Kufuatia vita vya vurugu vya 2020-2022, Tigray ina makovu ya vurugu za miaka hiyo, hasa unyanyasaji mkubwa wa kijinsia, mauaji ya halaiki, uharibifu, na mgogoro wa kiuchumi na kijamii uliofuata ambao bado unaendelea, huku kukiwa na hofu kubwa ya milipuko mipya ya vurugu na matokeo ya kutengwa kwa eneo hilo.
Programu ya safari
Ziara ya kichungaji ya Kardinali Gugerotti katika Upatriaki wa Adigrat inaendelea na mnamo Juni 6, ataanza ziara yake katika Upatriaki wa Bahirdar-Dessie, mnamo Juni 9, katika Upatriaki wa Emedeber, na kisha katika Upatriaki wa Addis Ababa. Safari hiyo itakamilika mnamo Juni 12 kwa mkutano na maaskofu wote wa Baraza la Maaskofu wa Ethiopia.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here