FILE PHOTO: DRC's Kabila meets South Africa's Mbeki in Johannesburg FILE PHOTO: DRC's Kabila meets South Africa's Mbeki in Johannesburg  (SIPHIWE SIBEKO)

DR Congo: Rais wa zamani Kabila ahukumiwa kifo

Joseph Kabila alipatikana na hatia bila kuwepo kwa uhaini mkubwa.Uamuzi huo,ambao ulitoa hukumu ya kifo,ulijumuisha mashtaka ya kushirikiana na waasi wa M23.

Vatican News

Mahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) imemhukumu kifo Rais wa zamani Joseph Kabila kwa kosa la "uhaini." Kabila, mwenye umri wa miaka 54, ambaye hakuwepo katika kesi hiyo katika mji mkuu wa nchi hiyo wala kuwakilishwa, alipatikana na hatia ya kushirikiana na kundi linaloipinga serikali la M23, ambalo, kwa msaada wa Rwanda, liliteka maeneo makubwa ya mashariki mwa Congo, yenye utajiri wa maliasili na madini.

Rais huyo wa zamani hajulikani alipo

Rais huyo wa zamani aliondoka nchini mwaka 2023 na kujitokeza tena kwa muda mfupi huko Goma, mashariki mwa nchi hiyo yenye hali tete, mwezi Mei, na kusababisha machafuko mjini Kinshasa. Waangalizi wa mambo hayo wanasema hukumu hiyo ya kifo inanuiwa kuondoa uwezekano wa yeye kuunganisha upinzani ndani ya nchi, ingawaje hajulikani aliko hasa. Katika ziara yake mjini Goma mwezi Mei, Kabila alikutana na viongozi wa kidini wa eneo hilo akiwepo msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka.

Miaka 30 ya Ukatili

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, iliyoharibiwa na ghasia kwa zaidi ya miongo mitatu, iliondoa kusitisha hukumu ya kifo mwaka jana (2024), lakini hakuna hukumu ya kifo iliyotekelezwa tangu wakati huo. Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Kijeshi Lucien René Likulia alikuwa ametoa wito wa hukumu ya kifo kwa Kabila, ambaye chama chake kiliitaja kesi hiyo "kesi ya kisiasa." Likulia alimshutumu kiongozi huyo wa zamani kwa kupanga njama ya kumpindua Rais Felix Tshisekedi, na mashtaka mengine dhidi yake ni pamoja na mauaji, utesaji, na ubakaji kuhusiana na M23.

Mapambano ya Nguvu

Likulia alidai kuwa Kabila, kwa uratibu na Rwanda, alijaribu kufanya mapinduzi dhidi ya Tshisekedi, hasa kwa msaada wa Corneille Nangaa, ambaye alikuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wakati wa uchaguzi wa rais wa 2018, ambao Tshisekedi alishinda. Kabila aliongoza nchi hiyo kati ya 2001 na 2019, akichukua mamlaka kufuatia mauaji ya baba yake, Laurent-Desiré Kabila.

02 Oktoba 2025, 08:04