Rais Samia  Suluhu Hassani ameapa  mbele ya jaji mkuu wa Tanzania na kuhutubia Taifa Rais Samia Suluhu Hassani ameapa mbele ya jaji mkuu wa Tanzania na kuhutubia Taifa 

Tanzania:Rais Suluhu Hassan ameapishwa muhula wa pili

Novemba 3,Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameapishwa kwa muhula wa pili huku kukiwa na ulinzi mkali, kufuatia uchaguzi uliokumbwa na maandamano yenye ghasia na kukataliwa na upinzani kuwa sio huru na wa haki.Suluhu,mwenye umri wa miaka 65,alikula kiapo chake mbele ya Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma,akiahidi "kulinda na kutetea Katiba na umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Sherehe ya kuapishwa kwake Jumatatu tarehe 3 Novemba 2025 imefanyika katika uwanja wa kijeshi katika mji mkuu wa Dodoma, Tanzania katika hafla iliyofungwa kwa umma lakini ilirushwa hewani mbashara na kituo cha serikali cha TBC. Samia alitangazwa mshindi Jumamosi kwa asilimia 98 ya kura. Alikabiliwa na upinzani mdogo huku wagombea wakuu waliokuwa wakishindana naye wakifungiwa au kuzuiwa kugombea. Mtandao ulibaki umezimwa nchi nzima wakati rais huyo alipokuwa akila kiapo, huku vikosi vya usalama vikitumwa katika miji muhimu kuimarisha usalama.

Tanzania, Novemba 3 iikuwa siku nyingine ya kukaa ndani

Katika jengo la kibinafsi linalomilikiwa na serikali huko Dodoma, mji mkuu wa nchi ya Tanzania, ambapo watu walipendelea kukaa ndani na maduka yalibaki yamefungwa, wakati  Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa rais kwa muhula wa pili katika sherehe iliyotengwa kwa wageni wali wachache tu waliochaguliwa. Hafla  hiyo ilifanyika licha ya taifa hilo kuingiwa na maandamano ya vurugu mitaani tangu Oktoba 29. Upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi, ambayo rasmi yalishuhudia Chama cha Mapinduzi, ambacho Hassan ni mwenyekiti wake, kikishinda zaidi ya asilimia 97 ya kura, na hivyo kumwacha Hassan kama mgombea pekee wa urais.

Suala la 4Rs

Kati ya mengi aliyosema, wakati wa hotuba ya Rais  Samia alisema kuwa  atafanya "kazi ya kuliunganisha taifa" hilo la Afrika Mashariki ambalo kwa kipimo chochote kile ni kwa hakika limegawika baada ya uchaguzi, na pia alisema ataendelea na "juhudi alizoanzisha za kutafuta maridhiani na mageuzi chini ya kauli mbiu '4Rs',  ambayo ni Falsafa yake inayojikita katika masuala ya Maridhiano, Ustahamilivu,Mageuzi na Kujenga upya Taifa. Na zaidi alisema Bi Samia alisema: "Niwasihi Watanzania, tuchague hekima badala ya ghadhabu, busara badala ya mihemko, upendo badala ya chuki, uvumilivu badala ya vinyongo, umoja badala ya mgawanyiko na amani badala ya vurugu."

Hata hivyo Harakati za walio wachache zimeshutumu mara kwa mara kutengwa kwa wagombea wawili wakuu katika uchaguzi bila haki na kinyume cha sheria, na hivyo kumwacha Hassan kama mgombea pekee wa urais. Na waangalizi wa kimataifa wameibua wasiwasi kuhusu uwazi wa uchaguzi huo na madhara yake ya kukumbwa na ghasia, huku mamia ya watu wakiripotiwa kuuawa na kujeruhiwa. Mamlaka imejaribu kupuuza ukubwa wa ghasia na vilevile imekuwa vigumu kupata habari kutoka nchini humo au kuthibitisha idadi ya watu waliofariki, baada ya mtandao kuzimwa  nchini kote tangu siku ya uchaguzi.

Mwendelezo wa waangalizi kuhusu upigaji kura

Vile vile waangalizi zaidi ya 80 waliofuatilia mwendelezo wa kura hiyo walifichua "kushindwa kuheshimu viwango vya kidemokrasia ambavyo vilisababisha vitisho, matukio ya udhibiti, na ukosefu wa uwazi ndai kabla na wakati wa mchakato wa kupiga kura." Ingawa mamlaka ya Tanzania bado hayajatoa idadi rasmi ya waathiriwa wa vifo hivyo, msemaji wa Umoja wa Mataifa, akinukuu ripoti za kuaminika na zilizothibitishwa, alisema kwamba kulikuwa na vifo vya watu wapatao kumi katika miji ya Dar es Salaam, Shinyanga, na Morogoro. Idadi ya upinzani inatofautiana, ikidai idadi ya vifo inaweza kufikia mamia. Na huku jeshi likiendelea kulinda mitaa na viwanja, serikali imeahirisha ufunguzi wa vyuo vikuu, uliopangwa kufanyika Jumatatu Novemba 3, huku mtandao ukiendelea kufanya kazi kwa wahusika wachache ,ukiwaacha watu wengi wametengwa. Hadi alasiri baada ya kuapishwa kwa rais ndipo mawasiliani yamerudi.

Wasiwasi na sala ya Papa Leo XIV  kwa  Tanzania

Ikumbukwe kufuatia an ghasia zilizojitokeza, tarehe 2 Novemba 2025  mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Leo XIV  pamoja na miito, nchini Sudan pia alitoa wito wa kusitisha vurugu nchini Tanzania:"tunaiombea Tanzania,ambapo,kufuatia uchaguzi wa kisiasa wa hivi karibuni,mapigano yalizuka na waathiriwa wengi.Ninawasihi kila mtu kuepuka aina zote za vurugu na kufuata njia ya mazungumzo."

Umoja wa Ulaya

Umoja wa Ulaya, kupitia Mwakilishi wake Mkuu wa Mambo ya Nje na Sera za Usalama, Kaja Kallas, "ulizihimiza mamlaka kuchukua hatua kwa kujizuia kabisa kulinda maisha ya binadamu" baada ya "kuzingatia tangazo la Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi kuhusu matokeo ya uchaguzi." Marekani pia ina wasiwasi kuhusu maandamano na mapigano mapya yanayowezekana: Idara ya Mambo ya Nje imeongeza kiwango chake cha tahadhari kuanzia 2 hadi 3 na kuwaomba raia wake kufikiria upya mipango yoyote ya usafiri na kuepuka usafiri wa siku zijazo.

Athari zinazowezekana

Mvutano unaoathiri Tanzania hivi karibuni unaweza kubadilisha mandhari ya kisiasa na usawa katika eneo hilo, ingawa kwa sasa, baadhi ya mataifa jirani yametambua uhalali wa uchaguzi. Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tshisekedi Tshilombo, na Rais wa Kenya, William Ruto, walimpongeza Rais Hassan aliyechaguliwa tena kwa "ushindi wake mkubwa wa uchaguzi." Katika chapisho kwenye akaunti yake ya X, Rais wa Uganda Yoweri Museven alisisitiza kwamba ushindi huo unaonesha "imani ambayo watu wa Tanzania wanaweka katika uongozi na maono ya Hassan."

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: cliccando qui

03 Novemba 2025, 16:41