Afrika Kusini:Pombe inagharimu kidogo kuliko Mkate:inaathiri watoto na vijana!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kupandisha bei ya pombe ili kupunguza madhara yanayosababishwa na matumizi mabaya ya pombe kwenye jamii. Hili ndilo lengo la maandamano yanayofanyika tarehe 18 Februari 2026 mbele ya Bunge la Afrika Kusini mjini Cape Town. Maandamano hayo yaliandaliwa na Muungano wa Sera ya Pombe Kusini mwa Afrika-Afrika Kusini (SAAPA-SA), shirika ambalo kwa muda mrefu limezindua kampeni inayoitwa: "Gharama Halisi ya Pombe" kukemea madhara ya kijamii na kiuchumi ya matumizi mabaya ya pombe, hasa miongoni mwa vijana.
Pombe kugharimu kiasi kidogo kuliko mkate
"Maandamano haya yalilenga kusukuma ongezeko la ushuru wa pombe, kwani ni hatua iliyothibitishwa ya kupunguza matumizi mabaya ya pombe, hasa miongoni mwa watoto na vijana," alisema Nomcebo Dlamini, mkuu wa Muungano wa Sera za Pombe, Kusini mwa Afrika-Afrika Kusini(SAAPA-S.) "Pombe inayouzwa Afrika Kusini, hasa bia, inagharimu kidogo kuliko mkate katika jamii zetu nyingi, ndiyo maana inapatikana kwa urahisi," alisisitiza.
Pombe inachangia vurugu na nyanyaso za majumbani
Kulingana na Shirika la Afya Duniani, Waafrika Kusini 100 hufa kila siku kutokana na sababu zinazohusiana na pombe, au takriban vifo 37,000 kwa mwaka. Pombe pia ni mchangiaji mkuu wa vurugu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa majumbani na unyanyasaji wa kijinsia, katika nchi ambapo 36% ya wanawake hupitia ukatili wa kimwili au kingono katika maisha yao.
Wakati Sekta ya pombe ikistawi,gharam za vurugu,kiwewe na ajali huongezeka
Zaidi ya gharama za kijamii ni zile za kiuchumi: huku sekta ya pombe ikistawi, uchumi mpana kwa ujumla hunyonya gharama za vurugu, kiwewe, ajali mbaya za barabarani, na msongo wa mawazo kwenye mfumo wa huduma ya afya, huku athari ya kiuchumi ikiwa takriban randi bilioni 800 ambazo ni (zaidi ya euro bilioni 42,).
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here