Mji wa Uchumi huko Havana, Cuba Mji wa Uchumi huko Havana, Cuba  (AFP or licensors)

Cuba:Katika fursa ya Juma Takatifu msamaha watangazwa kwa wafungwa 2,010

Serikali ya Havana imeamuru kuachiliwa kwa kundi la wafungwa,ikiiita"ishara ya kibinadamu na uhuru."Miongoni mwa wanufaika wa hatua hiyo ni wale ambao wametumikia"sehemu kubwa ya kifungo chao" na ambao "wameonesha mwenendo mzuri wakiwa gerezani."

Vatican News

Serikali ya Cuba ilitangaza kuwa imewasamehe wafungwa 2,010 kabla ya Pasaka, baada ya kuwaachilia wafungwa 14 chini ya mwezi mmoja uliopita. Havana inaita hii ni "ishara ya kibinadamu na ya uhuru" ambayo inakuja "ndani ya mfumo wa maadhimisho ya  kidini ya Juma Kuu Takatifu," kulingana na taarifa rasmi iliyosomwa kwenye televisheni ya Cuba.

Ingawa orodha ya wafungwa wanaofaidika na msamaha huu, wala kutolewa, sababu za kukamatwa kwao,  taarifa hiyo inabainisha kwamba wametumikia "sehemu kubwa ya vifungo vyao" na "wameonesha tabia njema gerezani."

Hawa ni pamoja na "vijana, wanawake, na watu zaidi ya miaka 60," pamoja na "wageni na raia wa Cuba wanaoishi nje ya nchi," hati hiyo inaendelea. Serikali ya Cuba, chini ya shinikizo kutoka Washington, ikiwa ni pamoja na kupitia kizuizi cha mafuta, ilisisitiza kwamba msamaha uliotangazwa utakuwa "wa tano" kutolewa tangu 2011. Tangu wakati huo, watu 11,000 wamefaidika na msamaha huo.

MSAMAHA CUBA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

03 Aprili 2026, 16:35