Vita kati ya Urusi na Ukraine. Vita kati ya Urusi na Ukraine.  (ANSA)

Ukraine na Putin atangaza kusitisha mapigano kwa ajili ya Pasaka

Kufuatia tangazo la kiongozi huyo wa Kremlin,Rais wa Ukraine Zelensky alithibitisha nia ya Kyiv ya kuheshimu usitishaji mapigano.

Vatican News

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza kusitisha mapigano kwa saa 33 upande wa Ukraine kwa ajili ya Pasaka ya Kiorthodox. Kulingana na Kremlin, kusimamishwa kwa uhasama kutaanza kutumika kwa vikosi vya kijeshi vya Urusi kuanzia saa 9:00 Alasiri (saa za Italia) Jumamosi, Aprili 11 hadi usiku wa manane Dominika tarehe 12 Aprili 2026. Kusitishwa huku kwa muda mfupi katika mzozo huo kulibuniwa ili kuwaruhusu waamini kusherehekea sikukuu muhimu zaidi katika kalenda ya kidini. Katika kipindi hiki, jeshi la Urusi limeamriwa kusitisha shughuli katika pande zote, huku likidumisha hali ya tahadhari ili kuweza "kukabiliana na uchokozi wowote wa adui." Muundo unaoakisi, hata katika utangulizi wake, hali isiyotabirika ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Ni matumaini kwamba hayatabaki kuwa tukio la pekee

Rais wa Ukraine,  Volodymyr Zelensky, ambaye katika siku zilizopita alikuwa amependekeza makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyowekwa kwenye miundombinu ya nishati, alithibitisha nia ya Kyiv ya kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano. "Ukraine imerudia kusema utayari wake wa kuchukua hatua zinazolingana," alisema, huku pia akisisitiza hitaji la kusitisha mapigano ili yasibaki kuwa tukio la pekee. "Watu wanahitaji Pasaka isiyo na vitisho na harakati halisi kuelekea amani," aliongeza, akihimiza Moscow isiendelee na uhasama baada ya likizo. Licha ya thamani yake ya mfano, makubaliano ya kusitisha mapigano ya Pasaka hayatakuwa mchakato wa kweli wa mazungumzo. Afadhali iwe kusimamishwa kwa muda kwa shughuli za kijeshi, bila mfumo uliopangwa na dhamana ya kimataifa. Wakati huo huo, ardhini, mzozo unaendelea kudai waathiriwa.

Mashambulizi zaidi katika ardhi ya Ukraine

Mwishoni mwa usiku ya kuamkia makubaliano ya kusitisha mapigano, mashambulizi ya mizinga ya Urusi na mashambulizi ya anga yaliwaua raia wawili katika eneo la Dnipropetrovsk, kulingana na mamlaka za mitaa. Kwa vyovyote vile, umakini wa kimataifa unaonekana kurejea polepole Ulaya Mashariki. Baada ya mkwamo unaohusishwa na mvutano katika Mashariki ya Kati, ambao ulikuwa umeilenga Marekani kwenye Ghuba, kuna uwezekano wa kuanza tena kwa mazungumzo kati ya Washington, Kyiv, na Moscow. Zelensky mwenyewe, katika mahojiano na RAI, alielezea matumaini kwamba kutangazwa kwa kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran kunaweza kukuza kujitolea upya kwa Marekani kwa suala la Ukraine.

Maaskari wa Ukraine katika Mkano wa  Zaporizhzhia
Maaskari wa Ukraine katika Mkano wa Zaporizhzhia

Rais wa Ukraine alielezea, mazungumzo hayo yanapaswa kuzingatia hasa dhamana za usalama. Hata hivyo, suala nyeti linabaki wazi: mwitikio wa Marekani iwapo kutatokea uchokozi wa Urusi katika siku zijazo. Jambo linaloendelea kushikilia ambalo linaendelea kufanya njia kuelekea utulivu wa kudumu wa mzozo huo kuwa si ya uhakika.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

 

10 Aprili 2026, 14:55