2026.05.14 Wanafunzi wa Kipalestina katika Chuo Kikuu cha Sapienza,Roma. 2026.05.14 Wanafunzi wa Kipalestina katika Chuo Kikuu cha Sapienza,Roma. 

Kutoka Gaza hadi Roma:Wanafunzi waanza sura mpya katika Chuo Kikuu cha Sapienza

Kundi la wanafunzi wa Kipalestina kutoka Gaza wako Roma na wanaweza kuanza kujenga upya mustakabali wao kutokana na mpango wa pamoja wa Chuo Kikuu cha Sapienza,Jimbo la Roma na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.Siku ya ziara ya Kichungaji ya Papa Leo XIV katika taasisi hiyo ya kihistoria,Mei 14 walishirikisha historia zao za vita,uhamisho na matumaini.

Na Antonella Palermo na Linda Bordoni - Vatican.

Kwa wanafunzi 72 kutoka Ukanda wa Gaza, waliofika hivi karibuni jijini Roma ili   kuendelea na masomo yao, ni sura mpya ambayo si tu inaashiria mwanzo wa safari ya kitaaluma, bali pia uwezekano wa kujenga upya mustakabali ulioingiliwa na vita. Nada Jouda na Salem Abumustafa ni miongoni mwa wanne waliojiandikisha katika Chuo Kikuu cha Sapienza cha Roma kupitia mpango wa kibinadamu na kielimu unaoendelezwa kwa pamoja na Chuo Kikuu, Jimbo la Roma na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. Matukio yao yalianza kwa kishindo: walikuwepo kumsalimia Papa Leo XIV alipotembelea katika ziara yake ya kichungaji ya Taasisi hiyo,  tarehe 14 mei 2026 kuimarisha dhamira yake ya kuwaelimisha viongozi wetu wa siku zijazo, na kuwaunda kuwa mafundi wa amani. Wakati wa hotuba yake kwa Jumuiya ya Chuo Kikuu cha  Sapienza, pia alielezea shukrani zake “kwa makubaliano ya kufungua njia ya kibinadamu ya chuo kikuu kutoka Ukanda wa Gaza.”

Makubaliano hayo, yaliyosainiwa mnamo mwezi Februari, yalilenga kuwapa vijana Wapalestina walioathiriwa na vita huko Gaza uwezekano wa kuendelea na elimu yao ya chuo kikuu nchini Italia kupitia ufadhili wa masomo, malazi na programu za ujumuishaji. Kama Papa Leo XIV alivyohimiza jumuiya ya kitaaluma kufanya vyuo vikuu kuwa “mahali pa kukutana, mazungumzo na kujenga amani,” uwepo wa wanafunzi kutoka Ukanda wa Gaza ulikuwa ushuhuda wa kugusa moyo wa hitaji la kuwekeza katika masomo na utafiti, akithibitisha - kwa maneno yake - "ndiyo kali kwa maisha! Kwa maisha yasiyo na hatia, kwa maisha ya vijana, kwa maisha ya watu wanaolilia amani na haki!"

Papa alitembelea Chuo Kikuu cha Sapienza
Papa alitembelea Chuo Kikuu cha Sapienza   (@VATICAN MEDIA)

Ufadhili wa wanafunzi kutoka Palestina

Nada, Salem na wenzao wawili huko Sapienza, wanatarajiwa kuhudhuria programu za shahada ya lugha ya Kiingereza kwa mwaka wa  masomo 2025-2026. Chuo kikuu kimetenga ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wote wa Palestina waliokubaliwa kupitia programu maalum na kitawasindikiza katika masomo yao yote na mafunzo ya kitaaluma, huduma za maelekezo, usaidizi wa huduma za afya na usaidizi wa kisaikolojia, ikiwa ni pamoja na ufikiaji wa kituo cha ushauri nasaha ya  Chuo Kikuu.

Kwa upande wake, Jimbo la Roma litawakaribisha wanafunzi hao bila malipo katika makazi ya vyuo vikuu kuanzia walipowasili Italia hadi Machi 2029, pamoja na uwezekano wa kuongeza muda wa malazi kwa mwaka mmoja zaidi huku wakikamilisha tasnifu zao. Na kupitia uchungaji wa Chuo kikuu, pia itaunga mkono ujumuishaji wao wa kijamii na ushiriki katika shughuli za nje ya chuo. Wakati huo huo, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio itatoa kozi za lugha na utamaduni wa Kiitaliano kama sehemu ya mpango wake unaojengwa kwenye korido za kibinadamu zilizoendelezwa na Sant'Egidio tangu 2016, ambazo zimeruhusu maelfu ya wakimbizi kufika salama nchini Italia.

Historia ya Nada

Akizungumza na Vatican News, Nada Jouda mwenye umri wa miaka kumi na tisa alikumbuka jinsi vita vilivyokatiza ghafla elimu yake. "Vita vilipoanza, nilikuwa na umri wa miaka 17 na katika mwaka wangu wa mwisho," alisema. "Nakumbuka kwamba mnamo Oktoba 7 nilitakiwa kufanya mtihani wa historia. Baada ya hapo, hatukuenda shule kwa karibu miaka miwili." Asili yake kutoka Rafah, Nada alielezea uhamisho wa mara kwa mara ambao familia yake ilipitia katika kipindi chote cha mgogoro. Baada ya kifo cha baba yake mwaka wa 2023, yeye, mama yake na dada zake wawili wadogo waliachwa kukabiliana na ugumu wa vita peke yao. "Tulikuwa tunapambana sana kwa sababu tulikuwa familia ndogo na hatukuwa na mtu wa kutegemea," alielezea. Mama yake, ambaye zamani alikuwa mkurugenzi wa chekechea, alipoteza kazi yake baada ya kuzuka kwa vita.

Papa alitembelea Chuo Kikuu cha Sapienza
Papa alitembelea Chuo Kikuu cha Sapienza   (@Vatican Media)

Nada alisema alikuwa akibeba vitabu vyake vya shule wakati wa kila uhamisho, akijaribu kuendelea kusoma licha ya ukosefu wa utulivu uliomzunguka. Familia yake kwanza ilitafuta kimbilio katika mahema ya muda baada ya jeshi la Israeli kuingia Rafah. "Kulikuwa na maji kidogo sana ya kunywa, na bei za chakula zilikuwa juu sana," alikumbuka. Baadaye, walihamia Khan Younis, ambapo waliishi katika nyumba iliyoharibiwa wakati wa mgogoro. "Kulikuwa na majira ya baridi kali na baridi sana. Paa lilikuwa limeanguka, na mvua iliingia ndani."

Familia ililazimika kuhama tena, hatimaye ikajificha katika jengo jingine dhaifu lenye mbao zilizofunika paa. Akiwa dada mkubwa, Nada alichukua jukumu la kubeba maji kutoka sehemu za usambazaji wa misaada hadi kwenye makazi ya familia. Pia alizungumza kwa wasiwasi kuhusu afya ya mama yake. Kwa kuwa hapo awali alikuwa na ugonjwa wa leukemia, mama yake hajaweza kupata uchunguzi wa kimatibabu kwa miaka kadhaa.

Chuo cha Sapienza

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

16 Mei 2026, 10:30