Dk.Stefano akiwa katikati na makocha wenzake huko Zanzibar,Tanzania:Maandalizi ya Toleo la 6 la Zanzibar CUP liko njiani,jiandae. Dk.Stefano akiwa katikati na makocha wenzake huko Zanzibar,Tanzania:Maandalizi ya Toleo la 6 la Zanzibar CUP liko njiani,jiandae. 

Tanzania:Dk.Conte,anatumia Kitesurfing kukuza amani,vijana na utalii,Zanzibar

Katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Vatican News,Dkt.Conte,Daktari wa watoto,anashirikisha safari na mafanikio yanayokua ya Kombe la Zanzibar,shindano la kimataifa la kitesurfing linalofanyika kila mwaka huko.Daktari aliyegeuka kuwa mtangazaji wa amani na kuishi kwa pamoja kama ndugu kupitia michezo alielezea jinsi tukio hilo linavyosaidia kukuza utalii,michezo ya vijana na umoja wa kimataifa wa Afrika Mashariki yote.

Na Angella Rwezaula na Sr.Christine Masivo, CPS – Vatican.

Akizungumza wakati wa mahojiano, Dkt. Stefano Conte alijitambulisha kwa mara nyingine tena kama Daktari wa Watoto kutoka jijini Roma nchini Italia na mwenye uhusiano mkubwa na urafiki na  Zanzibar, nchini Tanzania. Alieleza kwamba kwa miaka mingi alibobea katika upasuaji wa moyo wa watoto na pia alijitolea sehemu ya kazi yake ya ajili ya matibabu kuwasaidia mamia ya Wazanzibar  kupata matibabu ya bure.

Washindi wa Zanzibar Cup
Washindi wa Zanzibar Cup

Kuanzia matibabu hadi maendeleo ya michezo

Kazi yake ya kujitolea kibinadamu baadaye ilimtia moyo kuanzisha kwa Mchezo wa  Kombe la Zanzibar, Shindano la Kimataifa la kitesurfing lenye lengo la kuwawezesha vijana na kuunda fursa kupitia michezo. Kulingana na Dk. Conte, mashindano hayo yalianzishwa miaka mitatu iliyopita kwa ushirikiano na Serikali ya Zanzibar na tayari yamekamilisha matoleo matano yaliyofanikiwa licha ya changamoto zilizosababishwa na miaka ya janga la Uviko.

"Kuteleza kwenye kitesurfing kunakuwa moja ya michezo maarufu zaidi miongoni mwa vijana ulimwenguni kote” alisema. "Lengo ni kuisaidia Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla kukua katika mchezo huo huku pia ikitangaza utalii Kimataifa."

Washindi wa kimataifa wa Kitesurfing wa Zanzibar Cup
Washindi wa kimataifa wa Kitesurfing wa Zanzibar Cup

Tukio la michezo lenye ujumbe wa amani

Zaidi ya ushindani, Dk. Conte alisisitiza kwamba Kombe la Zanzibar lina dhamira imara ya kibinadamu na kijamii. Alielezea kwamba tukio hilo linalenga kukuza amani, udugu na umoja wakati ambapo sehemu nyingi za dunia zinakabiliwa na migogoro na ukosefu wa utulivu.

Akirejea wito wa amani uliotolewa na Papa Leo XIV, Dk. Conte alisema michezo inaweza kuwa daraja kati ya tamaduni na mataifa. "Tunataka kutuma ujumbe kwamba watu wanaweza kuishi pamoja kama kaka na dada bila vita," alisema. "Kila mtu aliye na fursa anapaswa kusaidia kusambaza ujumbe huu wa amani."

Bwana Conte pia alisisitiza juu ya “umuhimu wa kuwapa vijana fursa mbadala za michezo zaidi ya mpira wa miguu, akibainisha kuwa Kitesurfing ina uwezo wa kuvutia umakini wa Kimataifa kwa Zanzibar huku ikihamasisha ushiriki wa vijana wa ndani katika michezo ya kimataifa.”

Mashindano yanayobeba nguvu ya urafiki kidugu
Mashindano yanayobeba nguvu ya urafiki kidugu

Maandalizi ya Kombe la Sita la Zanzibar yanaendelea

Akitafakari kuhusu toleo la Tano lililofanyika mnamo tarehe 9 Februari  2026, Dkt. Conte alielezea tukio hilo kama la mafanikio licha ya hali dhaifu ya upepo. “Shindano hilo lilijumuisha kategoria mbili kuu, mbio za regata kuzunguka ufukwe na shindano la (freestyle), mtindo huru, lililohusisha kuruka na maonesho ya kiufundi.

Mashindano hayo yalivutia washiriki 42 kutoka nchi sita, wakiungwa mkono na Kundi la waamuzi wa kimataifa na kampuni 15 zinazofadhili. Dk. Conte aliisifu mchango wa Azam Sports HD kwa kutoa matangazo ya moja kwa moja kwenye Televisheni ambayo yalisaidia kupanua mwonekano wa tukio hilo ndani na nje ya nchi. Pia alitoa shukrani kwa Serikali za Zanzibar na Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono, hasa kuwatambua Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Katibu Mkuu Matar Zahor Massoud, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa kuunga mkono mpango huo.

Mashindano ya Zanzibar Cup
Mashindano ya Zanzibar Cup

Kuhusu maandalizi sasa yanalenga “Toleo la Sita la Kombe la Zanzibar lililopangwa kufanyika tarehe 23 Agosti 2026. Usajili wa washiriki wa ndani na nje ya nchi unatarajiwa kufunguliwa katika majuma yajayo, huku waandaaji wakiendelea kutafuta udhamini na ushirikiano wa vyombo vya habari. Dkt. Conte alimalizia kwa kuwaalika wanariadha, wadhamini na wafuasi kutoka ulimwenguni kote, kujiunga na tukio hilo na kuchangia katika kujenga kile alichokielezea kama “shindano la ajabu la kimataifa” linaloonesha nafasi inayokua ya Zanzibar katika utalii wa michezo duniani.”

Dkt Conte na shindano la Zanzibar
Toleo la Kiingereza na Sauti ya Dk Conte

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

12 Mei 2026, 17:16