Lebanon,UN:Zaidi ya watu 430,000 bado wamekimbia makazi yao.Mazungumzo na Israeli mjini Roma
Vatican News
Nchini Lebanon, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano na Israeli yaliyofikiwa Juni 26, zaidi ya watu 430,000 bado hawaweza kurudi makazi yao. Umoja wa Mataifa uliripoti hilo, ukielezea kwamba raia wengi hawawezi kurudi vijijini mwao kwa sababu nyumba zao zimeharibiwa. Katika Mkoa wa kusini, makazi 50 ya pamoja yamefungwa. Nyumba nyingine 45 bado ziko wazi na zinawahifadhi takriban watu 7,000. Vituo vipya vya mapokezi vimeanzishwa katika wilaya ya Tyre ili kusaidia familia ambazo zimehamia karibu na maeneo yao ya asili lakini bado familia hizo haziwezi kurudi majumbani mwao.
Mkutano wa kidiplomasia kufanyika Roma
Wakati huo huo, katika upande wa kidiplomasia, siku ya kwanza ya kikao cha sita cha mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Israeli na Lebanon yamekamilika mjini Roma. Mazungumzo hayo, yaliyofanyika katika Ubalozi wa Marekani, ambayo natarajiwa kumalizi tarehe 15 Julai 2026. Mazungumzo hayo yanalenga utekelezaji wa makubaliano ya mfumo yaliyofikiwa Washington mnamo Juni 26, ambayo yanatoa wito wa kuondolewa kwa vikosi vya Israeli kutoka "maeneo mawili ya majaribio" kusini mwa Lebanon na kukabidhiwa udhibiti taratibu kwa Jeshi la Lebanon, sambamba na kupokonywa silaha kwa Hezbollah.
Mazungumzo hayo yanafanywa pekee katika ngazi ya kidiplomasia, bila wawakilishi wa kijeshi. Washington iliuita mkutano huo kuwa "wenye tija" na kufanyika katika mazingira chanya, ikisema kwamba pande zote mbili zimejitolea kuendelea na mazungumzo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli Gideon Sa'ar alisisitiza nia ya Israeli ya kuanzisha kujiondoa kutoka maeneo mawili ya kwanza yaliyokusudiwa katika makubaliano hayo, huku akidumisha sharti kwamba mchakato huo uendelee sambamba na kuimarishwa kwa udhibiti na Vikosi vya Jeshi la Lebanon.
Gaza, uhaba wa maji na hatari kubwa ya magonjwa ya mlipuko
Changamoto ya kila siku ni kuishi, huku kukiwa na uhaba wa maji na hatari kubwa ya magonjwa ya mlipuko. Hata hivyo, vurugu katika Ukanda wa Gaza hazionyeshi dalili yoyote ya kupungua. Kulingana na shirika la habari la Palestina Wafa, shambulio la anga la Israeli dhidi ya nyumba huko Deir al-Balah, katika Ukanda wa Gaza wa kati, liliwaua watu wanne wa familia moja, akiwemo mvulana wa miaka sita. Siku iliyotangulia, Ulinzi wa Raia wa Gaza uliripoti waathiriwa wanane, akiwemo mwanamke, katika shambulio la bomu la Israeli kwenye kituo cha polisi magharibi mwa kambi ya wakimbizi ya Jabalia. Jeshi la Israel lilisema limewapiga wanachama wanne wa Hamas ambao, kulingana na Israel, walikuwa wakipanga mashambulizi ya kigaidi, lakini hawakufafanua utambulisho wa watu wengine waliouawa katika shambulio hilo.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.