2024.10.11 Sierra Leone, miniere di diamanti e oro

Mapambano ya Liberia dhidi ya uchimbaji haramu

Liberia imeimarisha utekelezaji dhidi ya uchimbaji haramu na kuboresha usimamizi wa rasilimali za madini nchini.Hatua hii inaonesha wasiwasi unaoongezeka barani Afrika kuhusu hali ya kiuchumi,kimazingira na usalama ya uchimbaji usiodhibitiwa.

Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Serikali ya Liberia imezindua “Kikosi Kazi cha Kulinda Rasilimali Zetu” (PORT), ambacho kimeundwa ili kuimarisha ukaguzi, kupambana na uchimbaji haramu, na kuboresha udhibiti wa sekta ya madini nchini. Kikosi hicho cha kazi kitasimamia shughuli za uchimbaji madini, kutekeleza mahitaji ya leseni, kufuatilia malipo, na kuhakikisha kufuata kanuni za mazingira na kazi.

Uchunguzi wa serikali kuhusu uchimbaji haramu

Akizungumza katika uzinduzi huo, waziri wa madini na nishati, Matenokay Tingban, alielezea mpango huo kama mabadiliko ya kimkakati kuelekea utekelezaji unaoongozwa na Utekelezaji wa sheria, uratibu imara wa kitaasisi, na usimamizi wajibikaji wa rasilimali za madini za Liberia. Kwa mujibu Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari, (FIDES), serikali ilisema kwamba kikosi kazi hicho kimekusudiwa kupunguza uchimbaji haramu na biashara haramu za dhahabu huku kikiongeza mapato ya umma na kukuza usimamizi endelevu wa rasilimali.

Changamoto yaongezeka kikanda wa uchimbaji haramu

Uchimbaji madini haramu umeenea barani Afrika Magharibi, Bonde la Congo, Afrika Kusini na Uganda, ambapo mamlaka hivi karibuni zimeongeza juhudi za utekelezaji. Hatua ya Liberia inaonesha changamoto pana inayoathiri nchi za Afrika. Uchimbaji haramu wa dhahabu mara nyingi hutegemea vitu hatari kama vile zebaki, ambavyo huchafua mito na vyanzo vya maji, na athari yake inaenea zaidi ya sekta ya madini. Katika Wilaya ya Kanungu nchini Uganda, msongamano wa dhahabu wa hivi karibuni ulisababisha wakazi wengi kuacha kilimo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini, kuvuruga uzalishaji wa chakula na kuchangia uhaba wa chakula wa ndani na kuwalazimisha watoto kuacha shule. Hatimaye, mamlaka zilifunga eneo hilo ili kurejesha utulivu na kushughulikia matokeo yaliyoadhiri jamii mahalia.

Rasilimali za madini na usalama wa kikanda

Uchimbaji haramu pia unahusishwa na wasiwasi mpana wa usalama wa kikanda na kiuchumi. Biashara ya dhahabu na madini mengine ya kimkakati inaendeshwa na mahitaji makubwa ya kimataifa na mara nyingi huhusishwa na ufisadi, na mitandao ya uhalifu iliyopangwa. Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, udhibiti wa maeneo yenye madini mengi umeunganishwa na migogoro ya silaha. Tangu kundi la waasi la M23 lilipoteka Goma mapema mwaka 2025, maeneo kadhaa ya migodi yameripotiwa kuwa nje ya udhibiti wa serikali, huku mapato kutoka katika dhahabu na madini mengine ya kimkakati yakichangia katika mitandao haramu ya biashara. Maendeleo haya yanaonesha jinsi ushindani dhidi ya utajiri wa madini wa Afrika unavyoendelea kuathiri utulivu wa kitaifa na usalama wa kikanda.

Liberia:Uchimbaji haramu wa Madini

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

13 Julai 2026, 11:23