Rais wa Nicaragua Rais wa Nicaragua  (AFP or licensors)

Nicaragua,Ortega afunga madaraka:"Uchaguzi usirudiwe tena"

Rais wa nchi ya Amerika ya Kati,huko Nicaragua katika maadhimisho ya miaka 47 ya mapinduzi ya Sandinista ya 1979, alitangaza kwamba hakutakuwa na uchaguzi tena ambao ungewaruhusu wapinzani wake kujaribu kuchukua serikali.

Vatican News

Ishara za kwanza za hili zilikuja mwaka 2025 wakati Rais Daniel Ortega alipoamua kuanzisha mfululizo wa mageuzi ya kikatiba ambayo, miongoni mwa mambo mengine, angemteua mkewe Rosario Murillo kama "rais mwenza" na kuongeza muda wake hadi miaka sita. Sasa, nia yake ya kupata madaraka yake imethibitishwa na tangazo Dominika Julai 19,2026 wakati wa  kuadhimisha miaka 47 ya mapinduzi ya Sandinista ya 1979, alibainisha kwamba hakutakuwa na uchaguzi tena ambao ungewaruhusu wapinzani wake kujaribu kunyakua madaraka.

Ukandamizaji baada ya uchaguzi wa 2021

Hatua ya Rais huyo mwenye umri wa miaka 80, ambaye ameshikilia madaraka mfululizo tangu 2007 baada ya muhula uliopita wa urais katika miaka ya 1980, ingefunga kabisa nafasi yoyote ya upinzani, ingawa hakutoa maelezo kuhusu jinsi kura hiyo itafutwa rasmi. Kauli hiyo ilitolewa kabla ya uchaguzi ujao  ambao umepangwa kufanyika mnamo Novemba 2027. Uchaguzi uliopita, uliofanyika mwaka 2021, ulipingwa sana baada ya Ortega kuwakamata wapinzani na viongozi wa biashara na kuwakandamiza wapinzani. Mashirika ya haki za binadamu yalijibu vikali. Kulingana na Juan Sebastián Chamorro, mgombea wa 2021 ambaye alibaki gerezani hadi alipoachiliwa huru nchini Marekani mwaka 2023 pamoja na wafungwa wengine zaidi ya 200 wa kisiasa, hatua hiyo inathibitisha mpango wa muda mrefu wa kuweka madaraka mikononi mwa chama cha Sandinista.

Wafungwa wa Kisiasa

Kulingana na takwimu kutoka  Mfumo wa Kutambua Wafungwa wa Kisiasa, Shirika linalofanya kazi kwa kiasi kikubwa kutoka uhamishoni na kurekodi visa vya kukamatwa kwa kisiasa nchini Nikaragua, inasemekana kuwa  watu 46 kwa sasa wanashikiliwa kwa sababu za kisiasa, ingawa baada ya operesheni ya Marekani nchini Venezuela, ambayo ilisababisha kukamatwa kwa Nicolás Maduro mwezi Januari, serikali ya Niaragua ilitangaza kuwa itawaachilia wapinzani zaidi. Tangu 2018, Nicaragua imefunga zaidi ya mashirika 5,000, mengi yakiwa ya kitawa, na kulazimisha maelfu ya watu kuondoka nchini humo. Mwanzoni mwa Julai 2026, serikali ya Ortega-Murillo ilifuta leseni za kitaaluma za idadi kubwa ya wanasheria, katika kile ambacho wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamekiita uondoaji halisi wa taaluma ya sheria.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

21 Julai 2026, 13:58