Tafuta

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Barazani Ulaya CCEE linatimiza miaka 50° tangu kuanza kwake 1971-2021. Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Barazani Ulaya CCEE linatimiza miaka 50° tangu kuanza kwake 1971-2021. 

Miaka 50 ya CCEE katika huduma Ulaya:kumbu kumbu na upeo wa Wote ni Ndugu

Tangu 23-26 Septemba utafanyika Mkutano ndani ya Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya ukiongozwa na mada “CCEE,miaka 50 katika huduma ya Ulaya kumbukumbu na upeo wa Wote ni ndugu".Papa ataongoza misa katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro,Septemba 23 saa 11.00 jioni.

Na Sr. Angela rwezaula –Vatican.

Shirikisho la mabaraza ya Maaskofu Ulaya (CCEE) mwaka huu linahitimisha miaka 50, tangu kuanzishwa kwambe mnamo Machi 1971 na baadaye kuidhinishwa  na Matakatifu Paulo VI.  Ili kusheherekea tukio hili la kijubilei, kuanzia tarehe 23-25 Septemba utafafanyika Mkutano mkuu wa Mwaka ambamo marais wa Mabaraza ya maaskofu wote wa Ulaya watashiriki jijini Roma. Kwa kupendekeza kama kiungo cha muungano kati ya Mabaraza haya  ya Maaskofu wa Ulaya, na ikiwa na lengo lake kuhamasisha  na kulinda mema ya Kanisa, kwa miaka 50  ya shirikisho hili CCEE limeweza kujitoa, kulingana na sheria yake katika: kuhamasisha  zoezi la  muungano katika ushiriki kikamilifu na Papa; kukuza ushirikiano wa karibu kati ya maaskofu na Mabaraza ya Maaskofu ili kuhamasisha  na kukuza  uinjilishaji mpya; kuchangia mazungumzo ya kiekumene ya umoja wa Kikristo; kutoa ushuhuda wa kanisa katika jamii ya Ulaya ”.

Kikao cha uzinduzi wa Mkutano Mkuu huo utafunguliwa na Sherehe ya maadhimisho ya Ekaristi itakayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko, katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, tarehe 23 Septemba 2021 saa  11.00 jioni masaa ya Ulaya. Baada ya kumaliza misa watatembelea makaburi ya mapapa waliosindikiza Shirikisho la Mabaraza ya  Maaskofu  (CCEE) kwa  kuwa na muda wa maombi katika makaburi hayo, Siku itakayofuata  tarehe 24 Septemba Marais wa Mabaraza ya  Maaskofu wa Ulaya watakaribishwa huko Ikulu na  Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella.

Mada iliyochaguliwa kuongoza Mkutano Mkuu, ni “CCEE, miaka 50 katika huduma ya Ulaya kumbukumbu na upeo wa Wote ni ndugu”. Hii inataka kuwa fursa ya kuchambua hali halisi ya Ulaya, kutambua vitu gani muhimu zaidi vinavyoathiri au kusaidia Kanisa na serikali na bara lao ili kufanya kumbukumbu iliyo hai ya mizizi asili ya Kikristo katika historia yake. Na ili kupyaisha dhamira ya Kanisa katika kujenga Ulaya, kufuatia ushauri wa Baba Mtakatifu Francisko ambaye, katika ujumbe wake kwa maaskofu wa Ulaya kwenye tukio la mkutano huko Santiago ya Compostela, aliwaalika wafanye kazi kwa ajili ya ubinadamu mpya wa Ulaya, wenye uwezo wa mazungumzo, ujumuishaji na kizazi ili Ulaya iweze kukua kama familia ya watu, nchi ya amani na matumaini.

20 September 2021, 16:21