Tafuta

2021.05.11 Mkutano kwa waandishi wa habari wakati wa kuwakilisha Barua ya kitume ya Antiquum ministerium ya Papa Francisko kuhusu huduma ya Katekista. 2021.05.11 Mkutano kwa waandishi wa habari wakati wa kuwakilisha Barua ya kitume ya Antiquum ministerium ya Papa Francisko kuhusu huduma ya Katekista. 

Marekani: Septemba 19 Dominika ya Katekista:sema neno moja tu

Maaskofu nchini Marekani wameandaa Dominika ya Katekista Septemba 19.Tukio hili ni maajabu ya fursa kwa ajili ya kutafakari juu ya nafasi ambayo kila mtu anajikita nayo,katika muktadha wa ubatizo,kwa kurithisha imani na kuwa shuhuda wa kweli wa Injili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

“Sema neno moja tu na roho yangu itapona”: ndiyo kauli mbiu inayoongoza Dominika ya Katekista ya Baraza la Maaskofu nchini Marekani itakayo adhimisha tarehe 19 Septemba 2021, ambayo ni Dominika ya tatu ya Mwezi. Tukio hili ni maajabu ya fursa kwa ajili ya kutafakari juu ya nafasi ambayo kila mtu anajikita nayo, katika muktadha wa ubatizo, kwa kuonesha imani na kuwa shuhuda wa kweli wa Injili. Siku hii, haitazami katekista tu lakini kwa ajili ya wote ambao wanaojikita katika shughuli ya mafunzo ya imani, watu wa kila rika na katika mazingira tofauti. Kati ya wote, inatosha kufikiria walimu wakuu na walimu wa shule katoliki, kwa mujibu wa taarifa ya Baraz ala maaskofu nchini Marekani.

Katika kufafanua maana ya siku hii, maaskofu wa Marekani wamechagua picha moja iliyochorwa na El Greco, ambayo inahusu tukio moja la kiinjili ambalo Kristo aliponesha kipofu, kwa kumpaka udogongo machoni mwake. Kwa mujibu wa maelezo, ya maaskofu wanabainisha kuwa, mwaka 2020 umeweza kuonesha wazo hili juu ya dharura ya haraka ya kuponesha (kimwili, kiroho na kihemko), iwe kwa ajili yetu sisi binadamu na kwa ajili ya ulimwengu wote.  Wakati sayari ilikuwa inapambana ili kupona na UVIKO-19, kiukweli ilijitokeza bayana kwamba uponeshaji kabisa hauwezekani bila kuwa na Yesu kwa sababu ni pale ambapo anapoponesha roho zetu ndipo basi anaweza kuponesha kila kitu.

Na kauli mbiu iliyochaguliwa kwa ajili ya kuongoza Dominika, tarehe 19 Septemba 2021 ni kumbukumbu ya wazo hilo, ambalo ni kwamba, ili kuokolewa ni muhimu kufungua macho yetu kwa uponeshwaji ambao Yesu Kristo  anatupatia katika Ekaristi. Tunamwomba kwa unyenyekevu kwa kusema neno moja tu, kwa sababu tuna imani na ukweli kwamba, pamoja naye, roho zetu zitaokolewa.

Ikumbukwe kwamba, ili kuponesha umuhimu wa sura ya katekista, kuna Barua binafsi ya Papa Francisko Motu Proprio “Antiquum ministererium” yaani “Huduma kale” ya hivi karibuni ambayo, mnamo Mei 11 iliyopita, Papa Francisko alianzisha rasmi huduma ya katekista, akiifafanua kama ni dharura ya uinjilishaji katika ulimwengu mamboleo, ili ufanyike kwa njia ya kidunia, bila kuangukia katika ukikuhani kuhani.

Makatekista wanaitwa kuwa ni wataalamu na wahudumu wa jumuiya ya waamini katika kutangaza, kushuhudia na kurithisha imani katika hatua mbalimbali. Waanzie hatua ya kwanza ya kutangaza Injili, “Kerygma”, kufundisha maisha mapya katika Kristo Yesu sambamba na kuwandaa waamini kwa ajili ya kupokea Sakramenti za Kanisa na hatimaye, kuendelea na majiundo endelevu ili kila mwamini aweze kuwa tayari siku zote kumjibu kila mtu anayemuuliza habari za tumaini lililo ndani mwake; lakini kwa upole na kwa hofu, (Rej.1Pet.3:15). Makatekista wanapaswa kuwa ni mashuhuda wa imani, waalimu, watu wandani wa imani na walimu wanaofundisha kwa niaba ya Kanisa. Yote haya yanaweza kutekelezwa kwa njia ya sala, masomo na ushiriki wa moja kwa moja katika maisha ya jumuiya yanayoweza kukuza utambulisho na uwajibikaji wake wote.

18 September 2021, 16:26