Tafuta

2021.12.03 Papa Francisko akiwa Ugiriki alisali sala ya Kiekumene na wahamiaji katika Kanisa la Msalaba Mtakatifu. 2021.12.03 Papa Francisko akiwa Ugiriki alisali sala ya Kiekumene na wahamiaji katika Kanisa la Msalaba Mtakatifu. 

Padre Patton:Cyprus ni maabara ya ‘Wote ni ndugu’!

Msimamizi wa Nchi Takatifu Padre Francesco Patton amezungumzia uwepo wa Wafransiskani huko Cyprus huku akisisitizia uhusiano mwema wa kiekumene ambao unauisha kisiwa hicho.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya ziara ya Papa Francisko katika kisiwa cha Cyprus, kuanzia tarehe 2-4 Desemba 2021, Padre Francesco Patton, Ndugu Mdogo Mfransiskani (OFM), Msimamizi wa Nchi Takatifu ambaye alikuwa katika kisiwa hicho kumpokea Papa Francisko katika ziara yake ya kitume alipata kuzungumza kuhusiana kisiwa hicho na utume wao kama wafransikani. "Siku zote Cyprus imekuwa sehemu ya Uhifadhi wa Ardhi Takatifu", amesema Padre lakini kwa kuongeza zaidi, kwamba Cyprus ni sehemu muhimu ya historia ya wokovu. Kwa sababu ni kutoka hapo kwamba Ukristo wa zamani ulianza kuenea kwake, kwa kwa mfano kwa njia ya Mtakatifu Barnaba (ambaye ni mtakatifu msimamizi wa Cyprus), ambaye alihama kutoka kisiwa hadi Antiokia ("baadhi yao, watu wa Cyprus na Kirene, wakiwa wamefika Antiokia; walianza pia kusema na Wayunani, wakitangaza kwamba Yesu ni Bwana" (Mdo 11, 20)).

Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Cyprus
Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Cyprus

Ndiyo huyo Barnaba wa Cyprus mwenyewe aliyemtambulisha Sauli wa Tarso akiwa kiongozi wa jumuiya ya kwanza iliyochanganyika ya Wayahudi na Wagiriki huko Antiokia. Labda wachache hawajuhi kwamba kwa kipindi fulani Cyprus ilikuwa pia makao ya Usimamizi wa Nchi Takatifu. Ufalme wa Kilatini ulipoanguka mwaka wa 1291, Ndugu Wadogo wa Mtakatifu Francis wa Assisi walifukuzwa kutoka Yerusalemu, wakahamia kisiwani na kutoka hapo wakaendelea, japokuwa kwa shida sana, kutekeleza wajibu wao kama wasimamizi wa mahali patakatifu. Na leo wapo kwenye kisiwa hicho kwa jumuiya tatu ndogo lakini zenye bidii sana na parokia upande wa Ugiriki huko Nicosia, Larnaca na Limassol, na shule, Chuo cha Nchi Takatifu pia huko Nicosia. Lakini pia wana hata shughuli thabiti ya uchungaji katika upande wa Uturuki wa kisiwa hicho: kila wiki mapadre wao wanakwenda kuadhimisha misa huko Famagusta, ambayo huhudhuriwa zaidi na wanafunzi wa kigeni, hasa Waafrika na wafanyakazi wengi wahamiaji kutoka Asia, nchi ya Ulaya Mashariki na Amerika Kusini.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Cyprus
Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Cyprus

Akizungumzia juu ya wingi amesema uwepo wawakikristo walio wengi ni Waorthodox yote lakini kuna mahusiano yaliyo bora ya kiekumene, kwa maana wakati mahitaji yao ya kichungaji yanapohitajika ndugu wa kiorthodox hawasiti kuwapatia makanisa yao ua vikanisa vidogo kuruhusu kuadhimisha misa kwa wakatoliki. Na ni muhimu kuzingatia kwamba kati ya waamini wapatao ishirini na sita elfu wa ibada ya Kilatini ni elfu mbili na mia tano tu walio wenyeji; Kwa maana hiyo asilimia 90 inaundwa na wageni na wahamiaji. Cyprus si tu maabara ya uekumene bali pia ya kile kinachoweza kuwa Kanisa la kesho, yaani, Kanisa lenye uwezo wa kuunganisha watu, tamaduni na mila mbalimbali amesisitiza Padre Patoni. Cyprus pia ni nchi ya Ulaya ambayo, kwa kadiri ya ukubwa wa wakazi wake, inakaribisha idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati. Jumuiya zao tatu nchini Cyprus zimejitoa sana kusaidia wahamiaji na wakimbizi. Hasa ni suala la upendo wa kusikiliza, kwa ndugu hawa ambao wanapata mkanganyiko wa kukutana na ulimwengu tofauti sana na kule wanakotoka.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Cyprus
Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Cyprus

Padre Pattoni amesema kuhusiana na mtengano uliotokea mwaka wa 1974 kati ya eneo lililobakia kuwa sehemu ya Jamhuri ya Ugiriki na lililokaliwa na vikosi vya jeshi la Uturuki kwamba hawangiliani na hatua ya mapadre wao wanaohamia kisiwa hicho kwa uhuru. Ili kupita kutoka sehemu moja hadi nyingine, uwasilishaji wa kadi ya utambulisho ni wa kutosha. Na hii ni muhimu hasa kwa sababu inawaruhusu kusaidia sio tu jumuiya ndogo ya Wakatoliki wa eneo hilo, lakini pia uwepo mkubwa zaidi wa wanafunzi Wakristo wa Kiafrika. Katika kisiwa kizima, hata hivyo, suala la usaidizi kwa wahamiaji na wakimbizi linachukuliwa kuwa ni nyeti maalum ya wakatoalini kwa kazi yao ya utume  pia inathaminiwa katika jumuiya za Kiislam.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Cyprus
Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Cyprus

Leo, hata hivyo, shughuli za Ndugu wadogo wafransiskiani (OFM) zimejikita zaidi katika kupendelea ujumuishaji wa wahamiaji, kwa sababu njia za wakimbizi zinahusu visiwa vingine vya Ugiriki vya Aegea, kama ama vile Rodi na Kos, pia maeneo ya chini ya usimamizi wa ulinizi ambapo Ndugu wadogo hao   wanafanya yote wawezayo kutoa huduma ya kwanza kwa wanaofika.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Cyprus
Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Cyprus
04 December 2021, 15:21