Tafuta

Papa amekwenda Lesbos kukaribia ubinadamu uliojeruhiwa wa wahamiaji

Papa baada ya kufika katika kisiwa cha Lesbos amewapa kwa upya mkubatio wake.Sala,shuhuda na ishara katika ziara hii iliyosubiriwa kwa hamu.Katibu Mkuu wa Caritas Hellas akihojiwa na Mwandishi wa Vatican News amesema wanafanya kazi ili kuhakikisha maisha yenye hadhi kwa wale wote wanaofika katika fukwe zao.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Katika hatua nyingine ya Papa Francisko kwenye ziara yake ya kitume  ya 35 kimataifa amefika kwa mara nyingine tena huko Lesbos. Ametaka kukutana na wakimbizi na wahamiaji na kusali pamoja nao sala ya Malaika wa Bwana katika kituo cha kukaribisha na kurekodi wakimbizi cha Mytilene. Ni kituo chenye ulinzi na kinacho wapokea maelfu na maelfu ya watu. Baada ya safari ya ndege kwa saa moja amefika mida ya saa 3.00a kamsubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Mytilene.  Baadaye aliondoka kutoka uwanja wa ndge hapo karibu km 16 hivi na amefika kwa mara nyingine tena  katika kituo hicho mara baada ya maka mitano  mnamo 2016 ambapo akiwa pamoja na Patriaki Bartolomeo I, na Askofu Mkuu wa Atene na Ugiriki yote, Hieronymus,  walikwenda kukumbatia wale ambao walikuwa wanafafanuliwa kama  janga la kibindamu zaidi baada ya vita ya pili ya dunia; yaani ule ubinadamu uliojeruhiwa wa maelfu na maefu ya wahamiaji wanaotafuta tumaini, ambao Papa Francisko binafsi alirudia kuzungumzia juu yao wakati wa mkesha wa ziara yake ya kitume wakati wa katekesi yake Jumatano tarehe Mosi Desemba 2021.

Ziara ya Papa katika kituo cha mapokezi ya wakimbizi huko Lesbos
Ziara ya Papa katika kituo cha mapokezi ya wakimbizi huko Lesbos

Akihojiwa na Dk. Massimiliano wa Vatican News, Katibu Mkuu wa Caritas Hellas,  Anna-Maria Stella Foskolou amesimulia kuwa wakati Baba Mtakatifu alipofika huko Lesbos mnamo 2016, hali halisi ilikuwa kweli ngumu sana. Kulikuwa kumejaa hata watu kutoka Uturuki, mamia na maelfu ya wakimbizi. Wakati huo hawakuwa wamejiandaa na kwa kuwa ni nchi ndogo, walikuwa na katikati ya mgogoro wa kiuchumi. Tangu wakati huo,  Caritas Hellas, kama ilivyo hata vyama vingine  vilianza kutafuta namna ya kujibu mahitaji ya watu hao na kuunda hali halisi ya kuweza kuwapokea.

Kituo cha mapokezi ya wakimbizi huko Lesbos
Ziara ya Papa katika kituo cha mapokezi ya wakimbizi huko Lesbos
Ziara ya Papa katika kituo cha mapokezi ya wakimbizi huko Lesbos

Kwa maana hiyo Papa amerudi katika kisiwa hicho ambacho kimekuwa ishala ya wito kwa jumuiya ya kimataifa ili, tena kama alivyosema mwaka wa 2016, ulimwengu uwe  makini kwa hali hizi za hitaji la kusikitisha na la kukata tamaa na kujibu kwa njia inayostahili jumuiya  ya wanadamu. Leo hii Lesbos ina sura nyingine, kambi ya Moria, mnamo 2020, iliunguzwa na moto,na Papa Franciko amekwenda huko, lakini pia  idadi ya wahamiaji hivi sasa aimepungua kwa zaidi ya silimia 80%, kwa maana kuna watu elfu tatu, ikilinganishwa na karibu  elfu 25,000 ya wakimbizi kwa  mitano iliyopita, wakati katika nchi nzima kuna zaidi ya laki moja. Walakini, amesema dalili za hatua kali zaidi za usalama pia zinaonekana. Serikali ya Ugiriki kwa mujibu wa Bi Foskolou  amesema kwamba imejaribu kuunda vituo vya mapokezi kwa mtindo uliofungwa na kudhibitiwa ambao Caritas Hellas haikubaliani nao  kwa sababu wanaamini kuwa kuwatenga kabisa watu hawa kutokutana  na jamii  sio hadhi ya kibinadamu. Huru wa kuzunguka ndiyo unaleta matatizo, lakini pia unapaswa  kutafuta njia nyingine.

Ziara ya Papa katika kituo cha mapokezi ya wakimbizi huko Lesbos
Ziara ya Papa katika kituo cha mapokezi ya wakimbizi huko Lesbos
05 December 2021, 16:43