Tafuta

2022.09.22 Ni maelfu na maelfu ya vijana kutoka ulimwenguni kwa ajili ya toleo la Tatu la Uchumi wa Francisko huko Assisi. 2022.09.22 Ni maelfu na maelfu ya vijana kutoka ulimwenguni kwa ajili ya toleo la Tatu la Uchumi wa Francisko huko Assisi. 

Vijana wa ulimwengu huko Assisi ili kueneza uchumi wa Francisko

Katika mji wa Mtakatifu Francisko kwa siku hizi kuna nafasi kubwa ya kukabiliana na ujumuishwaji wa Uchumi wa Francisko.Septemba 22 limefunguliwa rasmi toleo la Tatu la Uchumi wa Francisko.Hili linawaona vijana wanauchumi,wajasiriamali,wanamapinduzi kutoka nchi 120.Ushuda wa Sr Rancesca Violato na Samuel Lekato.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ni karibia vijana elfu moja wanauchumi kutoka katika mchi 120 ulimwenguni waliofika kwa ajili ya kushiriki Toleo la Tatu la Economy of Francesco, yaani “Uchumi wa Francisko, tukio lililozinduliwa na Papa kwa ajili ya kutaka kueneza uchumi unaostahili na wenye thamani ya udugu.  'Uchumi wa Francisko', harakati  ya kimataifa ya wanauchumi vijana, wajasiriamali wanaojishughulisha na mchakato wa mazungumzo jumuishi, ulizaliwa baada ya barua ya Papa Francisko, iliyotumwa mnamo 2019 kwa wanauchumi vijana, wajasiriamali na ulimwenguni kote. Kutokana na wito huo umekuwa mchakato wa kufikiria kwa upya uchumi. Mikutano miwili ya kwanza ilifanyika kwa njia ya mtandaoni kutokana na janga la uviko-19.

Shuhuda mbali mbali za "Uchumi wa Francisko"
Vijana wa Uchumi wa Francisko
Vijana wa Uchumi wa Francisko

Toleo la Tatu la Uchumi wa Francisko kufunguliwa 22 Septemba 2022

Hatimaye  katika tukio la toleo la Tatu limefunguliwa asubuhi tarehe 22 Septemba 2022.  Aliyekuwa akiwapokea vijana kati ya watu wa kujitolea na Staff ya Uchumi wa Francisko, mmojawapo alikuwa ni Sr. Francesca Violato wa Shirika la Wafranciskani wa Mtakatifu Elizabeth au (Bettine huko Padua Italia) ambaye ni mmisionari nchini Equador kwa miaka 20. Katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Vatican News, walioko huko Assisi amesema: “Kuna ulimwengu ambao unamiminika Assisi. Ulimwengu wa vijana, wanaopenda uchumi. Na ilikuwa nzuri kuwaona wakifika: hakukuwa na shida ya lugha kwa sababu tabasamu, kumbatio havikukosekana. Udugu ulipumuliwa. Machoni mwangu nina sura ya vijana wanaofika kituoni: safu ndefu ya vijana wenye shauku”.

Shuhuda mbali mbali za "Uchumi wa Francisko"

Samuel Lekato:Kukutana na Papa ni kitu ambacho sitosahau maisha yangu

Na kwa upande wa Kijana mmoja Mmsai, Samuel Lekato, kutoka nchini Kenya, katika mahojiano na Mwandishi wa Vatican News kuhusu tukio linaloendelea katika jiji la Assisi amesema alivyokuja “kujumuika na vijana wengine  kutoka ulimwenguni kote  ambao ni viongozi na kila mtu”.  Samuel pia ameeleza kuhusu sifa ya utamaduni wao wa kimasai kwamba ni adabu, kwani “kama wamasai tunaamini kushikilia sana tamaduni zetu” na hivyo  kwa kuongezea yeye amesema kuwa “tamaduni nyingine sio za kupoteza, lazima kuzizingatia maana ni fahari kwetu nchini Kenya”.

Shuhuda mbali mbali za "Uchumi wa Francisko"
Vijana wa Uchumi wa Francisko
Vijana wa Uchumi wa Francisko

Katika suala la uzoefu ambao atauchota kutoka  katika Toleo hilo la Tatu la “Uchumi wa Francisko”, Samuel amesema jinsi gani “Ninatarajia kupata uongozi kwani nimekuwa kiongozi wa muda mrefu na ninaona uongozi huko ndani mwangu hivyo ni imani yangu kwamba nitaimarika katika uongozi wangu zaidi”. Hatimaye akifafanua hisia  yake ya kukutana na Baba Mtakatifu Francisko anayetarajia kuwa Assisi, Jumamosi tarehe 24 Septemba 2022, Samuel  Lekato amebainisha kwamba "ni kama fursa nzuri ambayo si kila mtu anapata kumwona na kumsalimia, kitu mbacho sitakisahau katika maisha yangu”, amehimitimisha, Samuel.

Uchumi wa Francisko Samuel Lekato

 

22 September 2022, 16:52