Tafuta

Mtakatifu Yohane Paulo II mwanaume wa amani na umoja, upendo, mvumilivu wa mateso. Mtakatifu Yohane Paulo II mwanaume wa amani na umoja, upendo, mvumilivu wa mateso. 

Kard.Dziwisz akumbuka miaka 45 ya Karoli Wojtyla kuchaguliwa kuwa Papa

Aliyekuwa Katibu wa Papa Yohane Paulo II,anasisitiza kuwa mawazo na matendo ya Papa wa Poland ni ya sasa.Alikuwa Yeye aliyeanzisha mchakato mgumu wa kusafisha Kanisa kutoka katika uhalifu wa unyanyasaji wa watoto.Mafundisho yake na mtindo wake wa maisha unaweza kuigwa kwa vijana , lakinilugha zinapaswa kueleweka kwa vijana.

Na Padre Paweł Rytel-Andrianik; Paweł Rozwód – Vatican.

Miaka 45 iliyopita yaani tarehe 16 Oktoba 1978, alichaguliwa Papa ambaye alikuwa ni Kardinali wa Kipoland Karol Wojtyła, na ambaye alichagulia jini la Yohane Paulo II, baada ya mtangulizi wake aliyemaliza siku 33 tatu tu za Upapa. Hata leo hii angeweza kuleta amani duniani na matumaini, kwa mujibu wa Kardinali Stanisław Dziwisz, Askofu Mstaafu wa Krakow na aliyekuwa Katibu wa Papa mtakatifu kwa miaka 26 ya Upapa wake, akizungumza na Radio Vatican. Yeye bado anazungumza na inatosha kuja mjini Vatican katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kuona watu wengi katika sala mbele ya kaburi lake. Inatosha kuingia tu katika Madhabahu ya Kipapa kwenye makanisa ya Wadowice au Kalwaria, katika maeneo yote ambayo yanabeba ishara zake. Watu wengi wanaendelea kumsikiliza , wanatafuta urafiki kiroho”, alithibitisha Kardinali Dziwisz.

Kwa Kardinali Dziwisz aliulizwa ni nini angeweza kumwambia Papa wa Kipoland kuhusu ulimwengu mamboleo. Yeye alikibu kuwa migogoro ambayo tupo tunakabiliana nayo, imewekwa kwenye mjadala wa thamani ambazo hadi sasa zilikuwa zinafafana takatifu na zisizokiukwa na ambazo zimeweka kwa kina mgawanyiko na kutoelewana kijamii, na zingemjaza uchungu moyoni mwake. “Baba Mtakatifu aliyaona na kuyapitia mabaya sana matokeo ya vita na uimla, aliteseka pamoja na wanyonge, alikuwa mtetezi na sauti ya wale walionyimwa sauti zao na, wakati wa misukosuko, alijaribu daima kuleta matumaini kwa watu. Alikuwa shahidi wa upendo wa Kristo na nguvu ya Injili, isiyobadilika licha ya kubadilika kwa ulimwengu na nadhani kwamba leo ombi lake la 'Usiogope kumfungulia Kristo mlango' lingesikika kwa nguvu mpya, yenye nguvu.” – Aliongeza kusema.

Katibu wa Mtakatifu Yohane Paulo II anabainisha kuwa kadiri inavyopita muda, ndivyo hekima ya urithi wake unang'aa na bado unaonesha wazo ambalo ni mifano mingi inayotokana naye “Inahusu hata, na pengine zaidi ya yote, masuala ambayo baadhi ya duru leo hii hujaribu kumkosoa Baba Mtakatifu, kama vile suala la ulinzi wa watoto wadogo katika Kanisa. Wengi hujaribu kunyamazisha au kupotosha ukweli kwamba ni Yohane Paulo II aliyeanza mchakato mgumu wa kulisafisha Kanisa kutokana na uhalifu, ambao waathirika wake ni watoto wasio na hatia. Mchakato huu uliendelea na warithi wake, lakini Papa wa Poland ndiye aliyekuwa wa kwanza kupinga kwa uthabiti na kwa uthabiti kupunguzwa au kunyamazishwa juu ya masuala haya chungu.” Alisisitiza.

Kardinali huyo alibainisha kuwa hata Yohane Paulo II alikuwa mtume mkuu wa Hurumaya Mungu na ambaye alializnisha misingi ya chini ya Kitaalimungu na uwepo wa mchakato wa safari ya Kanisa la Papa Francisko ambalo anaendeleza leo hii, njia ya huruma, kuinama juu ya umaskini wa ubinadamu, ambapo ndiyo dada pekee ya upendo usi ona mwisho wa Mungu”. Kardinali Dziwisz aidha alisisitizia juu ya Sinodi ya Kisinodi inayoendelea. “Nadhani si kutia chumvi kusema kwamba mizizi yake iko katika maono ya mbali ya Papa wa Poland, ambaye aliona na kuthamini nafasi ya walei katika Kanisa; alikuwa wazi kwa mazungumzo na mazingira tofauti, sio marafiki wa Ukristo kila wakati na alisikiliza kwa uangalifu kile ambacho ulimwengu ulikuwa ukiambia Kanisa.” –Alisisitiza.

Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo kuu la Krakow anaamini kwamba, mafundisho ya Yohane Paulo II na mtindo wake wa maisha bado yanaweza kuwa chanzo cha mvuto kwa vijana. "Sina shaka na hilo, zaidi ya hayo imani hii inathibitishwa na hatima ya vizazi kadhaa vya vijana, ambao John Paul II aliwavutia kwa Yesu. Mamilioni ya watu bado wanakusanyika kwenye Siku za Vijana Duniani, wakikataa nadharia juu ya kupungua kwa Kanisa na kutojali kwa vijana juu ya maswali ya imani. Katika mafundisho ya Yohane Paulo II, vijana wanaweza kupata mafundisho ya maisha yao, lakini wanaweza pia kuhamasishwa na maisha yake, hasa kwa miaka yake ya ujana, ambayo ilikuwa imejaa shauku na tabia za ujana, furaha katika kuishi, ya masilahi mengi , hamu ya maendeleo ya kiakili na kiroho, uwezo wa kufurahia urafiki, uzuri wa asili, michezo, ushairi,"  alikumbusha Kardinali

Alitaja kwamba miaka ya ujana ya Karol Wojtyła pia ilikuwa ngumu, iliyooneshwa na janga la vita, lakini licha ya hayo, aliishi kwa uzuri, akionesha kwamba inafaa kupigania maadili makuu na kuwa mwaminifu kwao. "Kwa vijana - bila kujali wapi na wakati gani wanaishi - ni mfano wa kuvutia na unaostahili kufuatwa. Shida sio kwamba Papa anaweza kuwatia moyo, lakini jinsi uzuri wa maisha yake unavyowasilishwa kwao, ni lugha gani inatumika kumzungumzia, iwe ni lugha inayogusa hisia za vijana wa leo na ikiwa inaeleweka. kwa ajili yao."

Kardinali Dziwisz katika Mkutano mkuu wa uchaguzi. Tukirudi nyumba ya tarehe 16 Oktoba 1978, Kardinali Dziwisz anakumbuka kwamba muda mfupi baada ya kuchaguliwa, Yohane Paulo wa Pili alitaka kukutana naye. “Moshi mweupe ulipotokea, moyo wangu ulitetemeka, ukizidiwa na maonyo yenye nguvu. Niliposikia jina "Carolum", lililotamkwa kutoka kwenye balcony ya Basilica ya Mtakatifu Petro, tayari nilijua kila kitu. Miaka 45 imepita tangu nyakati hizo, ambapo mambo mengi yametokea, lakini wakati huo umebakia kuchapishwa kama chapa katika moyo wangu milele. Nilikuwa na hisia kali na furaha,” alisema. Aliongeza kusema kuwa walimkuta miongoni mwa maelfu ya watu katika uwanja wa Mtakatifu Petro na kumtambulisha ndani ya jumba la kumbukumbu, katika jumba la makumbusho ambapo makadinali hao pamoja na Baba Mtakatifu walikuwa wakila. “Kadinali Jean-Marie Villot, Katibu wa Vaticana wa wakati ule, alinipeleka kwa Papa, akasimama na kunisalimia kwa ukarimu. Maneno ya kwanza niliyosikia kutoka kwa Baba Mtakatifu wakati huo yalikuwa: ‘Walinifanyia hivyo!’ Yalipunguza hisia ambazo zilikuwa zimenishinda.”

miaka 45 ya kuchaguliwa kwa Papa Yphane Paulo II 16 Oktoba 1978.
17 October 2023, 15:40