Tafuta

2025.05.06  Mkutano Mkuu wa XXIII UISG. 2025.05.06 Mkutano Mkuu wa XXIII UISG. 

UISG na USG waombea Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Papa mpya

Sr Patricia Murray,katibu wa Umoja wa mama wakuu wa amashirika ya kitawa aliwasilisha Ripoti ya 2022-2025,akionesha hatua kuu:malezi katika uongozi na sinodi, mtandao wa Talitha Kum dhidi ya biashara haramu wa binadamu,Mtando wa Utunzaji wa Watoto Kimataifa na mipango iliyochochewa na Laudato si.’

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuwa 'mahujaji wa matumaini', mashuhuda wa umoja na mshikamano katika ulimwengu uliojeruhiwa." Huu ni mwaliko uliotolewa na Sr Mary Barron, rais wa Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika(UISG), kwa washiriki zaidi ya 900 waliokusanyika tarehe 5 Mei 2025 mjini Roma kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa XXIII, kwenye Jumba la Hoteli ya Ergife. Mada iliyochaguliwa kuwaongoza kwa mwaka huu ni: “Maisha ya Wakfu: tumaini linalobadilika.”Katika kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa Umoja huo (UISG) na katika wakati muktadha wa kifo cha Papa Francisko, Sista Barron alikumbuka urithi wa kiroho wa Papa Francisko na umuhimu wa kukutana binafsi na Kristo, wa mamlaka kama huduma, mazingira magumu kama rasilimali, ya nguvu ya sala na thamani ya sinodi. Pamoja na Sr Patricia Murray, katibu wa Umoja huo, aliwasilisha Ripoti ya 2022-2025, akionesha hatua kuu ya : malezi katika uongozi na sinodi, mtandao wa Talitha Kum dhidi ya biashara haramu wa binadamu, Mtando wa Utunzaji wa Watoto Kimataifa, na mipango iliyochochewa na Laudato si’. Kwa upande wa Sr Mariola López Villanueva alizungumza kuhusu matumaini kama “kamba ambayo Mungu ananyoosha kwetu. Ni kifungo cha upendo, utunzaji, uaminifu, na wajibu” huku akitoa mwaliko wa “kusuka mitandao inayoponya na kuzaliwa upya.”

Sr Brambilla:maisha ni mwanga unaoangaza giza la usiku wa dunia

“Watawa waliowekwa wakfu wanaitwa kung’aa kama mwezi: si kwa nuru yake yenyewe, bali kuakisi nuru ya Kristo, katika kundi la nyota, kwa kukaa mbinguni kwa ushirika”. Haya yalisemwa na Sista Simona Brambilla, mmisionari wa Consolata,aliyekuwa Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa ambaye aliyasema katika siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Umoja huo wa Mama wakuu(Uisg) kwa mwaka 2025 unaoendelea mjini Roma, ambao unajikita katika mada ya matumaini kama mabadiliko. Katika tafakari yake, Sr Brambilla alionesha udhaifu na uchache wa maisha ya kitawa kama chanzo cha nguvu zake za kinabii, katika ulimwengu unaopendelea nguvu na mwonekano. Washiriki wa uzoefu na maswali kuhusu uongozi wa kinabii na malezi ya kweli, wakisisitiza umuhimu wa "kuunda nafasi salama za kufungua sanduku la moyo."

Vipaumbele: maisha ya kitawa,karama na kutgemeza watawawa wazee

Alasiri, tarehe 7 Mei  Sr Mary Barron aliwasilisha mpango mkakati wa Uisg wa 2025-2031, kwa kuzingatia vipaumbele vitatu: kutoa umuhimu wa maisha ya kuwekwa wakfu, kulitajirisha Kanisa kwa karama kuwa sauti ya kinabii ulimwenguni. Miongoni mwa mipango iliyotangazwa, pia kuna “Hazina ya Wazee ya Masista Wakatoliki” ili kutegemeza watawa wazee. “Watawa wazee ni hekima, ushuhuda wao ni hazina yetu sote,” alisistitiza pia Sr Elda. Pia walioshiriki katika siku hiyo tarehe 7 Mei,  ni Padre Mario Zanotti, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wakuu Mashirikia ya Kitawa ya kiume (USG), na Padre Arturo Sosa, Mkuu Shirika la Jumuiya ya Yesu na Rais wa Wakuu wa Mashirika ya kitawa  wa kiume (USG.)

Kanisa linapitia kairos iliyohuishwa na matumaini mengi

“Tunamtumaini Mungu na mapenzi yake, tukijua kwamba Roho Mtakatifu atakuwepo na ataongoza uchaguzi wa papa mpya”. Haya yaliandikwa katika barua ya Umoja wa Wakuu wa mashirikia ya kitwa ya kiume (USG), ambayo inaungana na maombi ya Kanisa zima kwa ajili ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Papa mpya: "Tunafahamu kwamba tunapitia wakati muhimu sana katika maisha ya kikanisa, kairos iliyohuishwa na matumaini mengi", inasomeka maandishi yaliyotiwa saini na Padre Mario Zanotti, katibu wa USG, "ushirika, utambuzi na wema wa Kanisa utahuisha kila mshiriki wa Mkutano:" Watawa wanahakikishia ukaribu wao kwamba: Tunasindikiza na maombi na ukaribu wetu wa kidugu zawadi ya neema ambayo Bwana atamjalia kila mteule wa makardinali”. Umoja wa Wakuu wa Mashirikia ya kike na kiume Ulimwenguni unaonesha imani katika mchakato unaoendelea: "Tuna uhakika kwamba mazungumzo na kusikilizana kutaongoza Mkutano kushinda kila hofu au kutokuwa na uhakika."Hatimaye, ukumbusho wa kipindi cha kiliturujia: "Pasaka inatuonesha umuhimu wa mpito kwa umoja wa kina zaidi na maisha ya thati zaidi ya imani. Furaha ya kumkaribisha Papa mpya na kushiriki naye safari inayofuata ya Kanisa katika historia ya wanadamu inatungoja."
 

08 Mei 2025, 10:02