Kutoka Roma hadi ulimwengu:Vitae Fest 2025 yahamasisha wito wa kimataifa wa upatanisho
Vatican News
Mfuko wa Maisha Ulimwenguni (Vitae Global Foundation) waliwakusanyisha maelfu ya vijana kwa ajili ya Tamasha la Roma Mwaka 2025(Vitae Fest Roma 2025), siku ya Jumamosi tarehe 25 Oktoba 2025, jioni ambapo sanaa, muziki, na imani viliungana kuhamasisha umoja na uponyaji wa kiroho. Tamasha hilo lililofanyika Uwanja wa Schuster, lilibadilisha moyo wa Roma kuwa nafasi ya kutafakari na kuunganisha. Tukio hilo, ambalo ni sehemu ya programu rasmi ya Jubilei 2025, lilitoa zaidi ya burudani: lilikuwa kauli ya pamoja, harakati iliyotokana na hamu ya kushinda tofauti na kujenga upya uaminifu katika ulimwengu uliogawanyika.
Wasanii wa kiitaliano na Kimataifa miongoni mwao akiwemo hata Padre Guilherme, Benji & Fede, Settembre, Aka7even, Mimi, Lowrah na W1nk0, pamoja na Mariasole Pollio kama wageni maalum, walitumbuiza kwenye jukwaa la Vitae Fest katika mazingira ya uhalisi, hisia, na umoja. Kupitia lugha ya muziki ya ulimwengu wote, sauti za Kizazi (Gen Z) kutoka kila bara zilikusanyika pamoja kutuma ujumbe kwa wanadamu kutoka Roma: upatanisho unawezekana—na sisi wenyewe, na wengine na Mungu.
Wito wa Maridhiano
Wakati wa jioni hiyo, Luis Quinelli, mwanzilishi na rais wa Mfuko wa Viate Ulimwenguni (Vitae Global Foundation,) na Mariasole Pollio, mwenyeji wa tukio hilo, waliwaalika wote kujiunga na wito huu wa maridhiano, si tu kwa kuushiriki kwenye mitandao ya kijamii bali pia kwa kuutekeleza kwa njia ya mfano. Maelfu ya watu waliinua mikono yao pamoja, wakiunda "mnyororo wa mioyo" na wale walio karibu nao, ishara hai ya madaraja ambayo tumeitwa kuyajenga. "Tulitaka kutuma ujumbe kwa viongozi wa dunia: ni wakati wa kupatana na sisi wenyewe, na wengine, na Mungu," alisisitiza Luis Quinelli, mwanzilishi na rais wa Mfuko huo wa maisha Ulimwenguni (Vitae Global Foundation.) "Tunataka Siku ya Maridhiano ya Kimataifa, siku ya kuacha kupigana, kuacha kuchukia, kuacha kugawanya. Siku ya kujenga madaraja na kurekebisha mahusiano. Tumechoka na migogoro na mgawanyiko. Kupitia mipango kama hii, tunatumai kuhamasisha kizazi kurekebisha vifungo na kuleta maridhiano katika ulimwengu ambao mara nyingi huonekana kuvunjika."
Mchanganyiko wa lugha za sanaa, muziki, na mambo ya kiroho
Tamasha la Vitae ni mpango wa kimataifa unaounganisha lugha za sanaa, muziki, na mambo ya kiroho ili kuunda uzoefu unaogusa moyo na kuhamasisha vitendo. Iliyoundwa na Mfuko huo wa Vitae Global, tamasha hilo husafiri hadi miji mikuu ya dunia, likiwashirikisha wasanii na hadhira katika dhamira ya pamoja: kutumia ubunifu kama chombo cha amani, huruma, na mabadiliko. Kufuatia mafanikio ya Vitae Fest Mexico 2025, toleo la Roma liliashiria hatua mpya, likiweka Jiji la Milele kama mahali pa kuanzia kwa mpango wa kimataifa ambapo vijana wanakuwa mawakala hai wa upatanisho katika jamii zao.
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: Just click here