Tafuta

Lugha mpya na mashuhuda wapya kwa simulizi la amani

Patriaki wa Yerusalemu ya Kilatini,Kardinali Pizzaballa alikuwa mgeni wa Vyombo vya Habari vya Vatican na kusimulia tukio la kihistoria la Nchi Takatifu kufuatia makubaliano kati ya Israel na Hamas,akisema:“wajibu kwa jumuiya zetu,ambao ni kuzisaidia kutazama zaidi,kwa matumaini na kwa utulivu,kwa mustakabali tofauti.”

Andrea Tornielli na Beatrice Guarrera - Vatican.

Matumaini ya kujenga amani ya kudumu katika Nchi Takatifu, matatizo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi, hisia za jumuiya ya maandamano ya mitaani, ambayo yameunganisha watu kwa jina la hadhi ya binadamu. Haya ni baadhi ya mambo yaliyoguswa na Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, Kardinali Pierbattista Pizzaballa, ambaye alikuwa mgeni rasmi asubuhi ya leo, Jumatano, tarehe 15 Oktoba 2025, katika studio za Radio Vatican. Kardinali huyo alizungumza juu ya mapatano dhaifu, lakini pia matumaini ya pamoja ya Waisraeli na Wapalestina kwamba hii sio "mabano," bali "kwamba tunaweza kuanza tena kuishi kwa mtazamo mpya ambao sio vita na ghasia."

Kardinali Pizzaballa akihojiwa kwenye Studio za Radio Vatican.
Kardinali Pizzaballa akihojiwa kwenye Studio za Radio Vatican.

Uko mjini Roma kupokea tuzo, ya Achille Silvestrini, ambayo leo inatolewa kwa Padre Gabriel Romanelli, Paroko wa Familia Takatifu huko Gaza. Je, hali ikoje kwa Wakristo wa jumuiya hiyo ambao wameamua kubaki katika hali hiyo ngumu?

Tunawasiliana nao kila siku. Kila mara wanaandika kwamba bado hawaamini kwamba waliweza kulala usiku kucha bila kusikia sauti ya mabomu. Kuna (drones),ndege zisizo na rubani, lakini wamezoea hiyo kwa miaka. Vinginevyo, hali bado ni mapema sana. Kumekuwa na, kama inavyojulikana, mapigano kati ya vikundi mbalimbali, lakini yote haya yalitabirika kwa sababu vita vimesitishwa-hatujui kama vimeisha-na awamu zilizofuata bado hazijaamua kabisa, hazieleweki, na ziko upande upi. Kila kitu kinahitaji kujengwa, kupangwa, na ilikuwa—na inategemewa—kutakuwa na heka heka. Bado kuna mengi ya kufanywa. Hali inabaki kuwa ya kushangaza, kwa sababu kila kitu kimeharibiwa. Kwa hivyo watu wanarudi, lakini wanarudi kwenye vifusi. Hospitali hazifanyi kazi, shule hazipo. Bado kuna suala la miili ya mateka wa Israeli waliokufa, ambayo inahitaji kupatikana. Si rahisi, hasa kwa sababu, mara nyingi sana, eneo la miili hii limepotea katika machafuko. Kutokuwa na imani kumekithiri kati ya wahusika. Hata hivyo, zaidi ya haya yote, kuna hali mpya ambayo bado ni tete, lakini tunatumaini itatengemaa.

Je, inawezekanaje katika muktadha huu wa kihistoria, katika hali hii, kujenga matumaini na udugu?

Kwanza kabisa, inachukua muda. Hatupaswi kuchanganya matumaini na suluhisho la mzozo huo, ambao haupatanishi. Mwisho wa vita sio mwanzo wa amani, na sio mwisho wa migogoro. Ni lazima tuzingatie vipengele hivi vyote. Bilashaka kuna , hatua ya kwanza. Matumaini ni, kama ninavyosema kila mara, binti wa imani. Ikiwa roho yako ina imani, inaweza pia kufikia mambo ambayo inaamini. Kwa hiyo, kwanza kabisa, ni lazima tufanyie kazi hili, na watu ambao bado wanataka kurudi kwenye mchezo na kuunda mtandao huu, ndani na nje ya Gaza, kwa sababu hatupaswi kutenganisha pande hizo mbili kwa mipaka. Ni kutengeneza udugu. Naamini tunahitaji uongozi mpya wa kisiasa, lakini pia uongozi wa kidini. Nadhani ni muhimu sana; tayari tumeanza kuwafikia. Tunahitaji nyuso mpya, takwimu mpya ambao wanaweza kusaidia kujenga upya simulizi tofauti, kulingana na kuheshimiana.

Itachukua muda mrefu kwa sababu majeraha ni ya kina, lakini hatupaswi kukata tamaa. Kwa hivyo bado kuna matumaini ya kujenga amani ya kudumu, hata ikiwa sasa hivi tunachukua hatua za kwanza tu. Kwanza kabisa, lazima tuamini ndani yake, lazima tuitake. Itachukua muda mrefu; tusijidanganye kwamba itafika hivi karibuni. Na pia lazima tukumbuke kushindwa kwa mikataba ya awali, kushindwa nyingi ambazo zimedhoofisha uaminifu kati ya wahusika. Kutakuwa na awamu kadhaa. Nadhani labda kizazi kijacho kitakuwa na uhuru ambao kizazi hiki hakina uhuru wa leo. Lakini kazi ya kizazi hiki ni kuandaa kijacho. Kwa hiyo ni lazima hatua kwa hatua tutengeneze hali zote muhimu, kwa nyuso mpya na uongozi, na zaidi ya yote, tutengeneze mazingira ambayo, kidogo kidogo, pia yanakuza utamaduni wa heshima, ambayo italeta amani.                                      

Je, ni matumaini gani thabiti ya kizazi hiki, ya watu unaokutana nao kila siku Yerusalemu na kwingineko?

Hivi sasa, tuko katika awamu mpya, ambayo bado ni tete. Tunatoka katika miaka miwili ya kutisha. Na matumaini ni kwamba huu ni mwisho wa miaka hii miwili na sio muingiliano tu, kwa hivyo hili ni tumaini la kila mtu, linaloshirikishwa na wote, Waisraeli na Wapalestina. Kulia au kushoto, au juu au chini, kwa ufupi, wote wanataka kugeuza ukurasa. Hili ndilo jambo la kwanza. Kisha, bila shaka, kuna maoni tofauti, ya kisiasa na ya kidini. Pia kuna mitazamo tofauti. Lakini pia kuna hamu kubwa miongoni mwa watu wa kawaida kuanza tena kuishi—sitasema kawaida, lakini kwa mtazamo mpya ambao si vita na vurugu.

Katika siku za hivi karibuni, tumesikia ushuhuda wa kushangaza wa hali ambayo walikuwa nayo mateka wa Hamas, na ambao sasa wameachiliwa. Na pia tumesikia historia za udhalilishaji kutoka kwa wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel. Ni nini kinachoweza kusemwa juu ya maumivu haya, ambayo kwa njia fulani hukatisha maeneo yote? Na pia kuhusu ukweli kwamba inawezekana kujenga mustakabali ambao hauanzii kutoka katika chuki?

Ni moja ya majanga ambayo tumekumbana nayo siku za hivi majuzi. Ulisema "kupunguza maumivu," lakini haikutambuliwa kwa njia hiyo. Kila mtu alijifungia katika maumivu yake mwenyewe, hivyo kila mtu aliona maumivu yake mwenyewe tu, mtazamo wake mwenyewe, maumivu ya watu wao wenyewe. Na kama wengine walivyosema, kila mtu alijawa na maumivu yake mwenyewe hivi kwamba hawakuwa na nafasi ndani yao wenyewe kwa uchungu wa wengine. Sasa kwa kuwa hali hii imekwisha, labda tunaweza kujifungua hatua kwa hatua ili kuelewa uchungu wa wengine. Kuelewa haimaanishi kuhalalisha: itachukua muda kwa haya yote, na sijui hata ikiwa itawezekana. Chuki ambayo imepandwa, si katika miaka miwili tu tangu ilipolipuka—lakini pia kabla, masimulizi ya dharau, kukataliwa, na kutengwa—inahitaji lugha mpya, maneno mapya ambayo pia yanahitaji mashuhuda wapya. Huwezi kutenganisha kinachosemwa na anayesema. Kwa hiyo, ninarudia, tunahitaji nyuso mpya, ambazo zinaweza kutusaidia kufikiri tofauti.

Je, hali ikoje katika Ukingo wa Magharibi, katika Parokia za vijiji vidogo, kama vile Taybeh, Zababdeh, au Aboud? Je, ni jukumu gani la Wakristo na Wakatoliki hivi sasa, kama vile Wakatoliki wanaozungumza Kiebrania ambao wameunganishwa kikamilifu katika jamii ya Israeli?

Haya ni masuala mawili tofauti sana. Katika Ukingo wa Magharibi, hali ya jumla, si tu katika jumuiya za Parokia zetu za Kikatoliki za Kikristo, ni tete sana na inazidi kuzorota. Jamii katika vijiji vilivyotajwa inazidi kutengwa kutoka kwa kila mmoja: mamia ya vituo vya ukaguzi hudhibiti harakati za ndani, na kufanya hali kuwa ngumu zaidi. Imekuwa, kama nilivyosema mara kadhaa, aina ya "ardhi isiyo na sheria" kwa sababu kuna mashambulizi mengi na mivutano, ikiwa ni pamoja na walowezi, ambao, hata hivyo, wanabaki hivyo, maana hatuna mamlaka ya kurejea ili kukomesha hali hizi, ambazo zinaonekana, badala ya kudumu. Hii inaleta mvutano mkubwa na hata ukosefu mkubwa wa usalama ndani ya Parokia na Jumuiya zetu kwa ujumla. Hali katika Ukingo wa Magharibi bado ni tete sana, sio tu kisiasa bali pia kiuchumi. Rasilimali mbili kuu—Utalii kwenda Israeli na mahujaji—zimesitishwa kwa sasa, na hatujui zitaanza tena vipi au lini. Hii pia ina athari kubwa kwa maisha ya watu, hasa Wakristo.

Jumuiya ya Wakatoliki wanaozungumza Kiebrania inaundwa na jumuiya ndogo za watu mia kadhaa,  ambazo pia zimepokea mamia ya watoto wa wahamiaji au wafanyakazi wa kigeni nchini Israeli. Ninaamini jukumu lao ni muhimu sana ndani ya Kanisa, zaidi ya nje yake. Kwa maana fulani, wanalazimisha Jimbo letu, ambalo ni ngumu sana, kufikiria kwa upana, sio kuzingatia tu suala la Palestina, lakini kukumbuka kuwa ndani ya jamii ya Israeli pia, kuna maumivu, mitazamo, na maono tofauti ambayo lazima yazingatiwe.

Katika majuma ya hivi karibuni, tumeshuhudia uhamasishaji maarufu, maandamano kama yale ya Italia, ambapo mamilioni ya watu waliingia mitaani. Zaidi ya makundi yenye msimamo mkali na baadhi ya kauli mbiu zisizokubalika, kuna vijana wanaoingia mitaani, wakionesha nia yao ya kuondokana na mantiki ya kutojali...

Kwa hakika, kumekuwa na kupita kiasi, katika suala la vurugu na katika lugha dhidi ya Uyahudi, kwa mfano. Hili halikubaliki. Kumekuwa na maneno au kauli ambazo zinaweza hata kuhalalisha, kwa namna fulani, chuki dhidi ya Wayahudi ambayo tunaikataa kabisa na thati, hilo lazima lisemwe. Lakini hatuwezi kujumlisha, tukisema kwamba kila mtu alikuwa hivi: kulikuwa na watu wengi, sio vijana tu. Kilichonishangaza ni kwamba kulikuwa na maelfu ya watu kutoka asili na vizazi tofauti, lakini pia kutoka matabaka tofauti ya kisiasa, ambao walikuwa wameungana kwa kusema hapana  picha za vurugu walizozishuhudia. Na hii, kwa maoni yangu, ni kipengele chanya, kwa sababu haikuamsha  ufahamu wa kibinafsi tu, lakini pia wa jumuiya, kwa sababu walikuwa wameunganishwa. Hili ndilo lililounda jumuiya. Ninaamini ni kipengele muhimu, jumuiya hii inayojenga, hii kuja pamoja karibu na kitu kizuri kama utu wa binadamu na kukataliwa kwa vurugu, mistari nyekundu ambayo haipaswi kuvuka, hata katika zoezi la kujilinda. Hiki kimekuwa kipengele kizuri sana na chanya. Tunatumaini inaendelea. Naamini ni mwamko muhimu, hata kwa viongozi mbalimbali wa dini na kisiasa, kukumbuka kuwa ndani ya dhamiri ya jamii kuna jambo zuri ambalo lazima lilindwe na pengine lionekane hata nje ya mazingira haya ya vita.

Sasa, tukirudi kwenye Nchi Takatifu, unatarajia mahujaji warudi?

Tunatumaini hivyo. Nimezungumza na Mlimzi wa Nchi Takatifu kuhusu kufanya jambo pamoja, kama vile kutoa taarifa. Tusubiri majuma mawili, au matatu tuone mambo yanakwendaje. Na kisha nadhani itabidi tuanze "kupiga nyundo" kwa njia fulani, hasa yale Makanisa ambayo yamekuwa karibu sana na Nchi Takatifu kwa miaka hii miwili. Hiyo kwa kusema ni wakati wa kuonesha mshikamano sio tu kwa sala, ambayo ni muhimu sana, na pia kwa msaada, lakini pia kwa njia ya hija.

Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 30 tangu kuuawa kwa Mkuu wa Kiyahudi, mtu wa amani. Je, kuna umuhimu gani kwa uongozi mpya kujitolea kwa ajili ya amani? Je, kuna dalili zozote chanya katika mwelekeo huu?

Naamini ni moja ya vipengele muhimu. Nimesema na kurudia mara nyingi. Nitarudia hapa: tunahitaji viongozi wapya wanaozungumza lugha tofauti na ile tuliyosikia miaka ya hivi karibuni. Sio wanasiasa tu, bali hata viongozi wa kidini. Miaka 30 iliyopita, Mkuu wa Kiyahudi alisema jambo moja, na viongozi wa kidini wakasema jingine. Sasa tunahitaji kubadilika; tunahitaji kukiri hili. Na katika muktadha huu, mazungumzo ya kidini ni muhimu sana. Mazungumzo ya kidini, kwa maoni yangu, pia yanahitaji sura mpya na hayawezi kupuuza yaliyotokea, ambayo yametuumiza sisi sote. Tunahitaji kuzingatia kile kilichotokea, kile tulichosema na ambacho hatujasema, sio kuishia hapo, lakini kusonga zaidi, kwa sababu tumefahamu. Tunahitaji kusonga mbele zaidi, tukikumbuka kile kilichotokea, bila kuwa wajinga sana. Shida ni nyingi, lakini tuna wajibu kwa jamii zetu, ambayo ni hasa kuzisaidia kutazama zaidi, kwa njia chanya na tulivu, kuelekea mustakabali tofauti.

Una maoni gani kuhusu mjadala wa kimataifa kuhusu kutambuliwa kwa taifa la Palestina?

Wapalestina hawahitaji tu kusimamisha vita, kusitisha ghasia, na kupokea misaada ya kifedha na kuungwa mkono. Pia wanahitaji kutambuliwa katika hadhi yao kama watu. Sijui kama suluhisho la "watu wawili, serikali mbili" ambalo linathaminiwa sana linawezekana kwa muda mfupi. Sitaingia kwenye masuala haya. Lakini huwezi kuwaambia Wapalestina hawana haki ya kutambuliwa kama watu katika nchi yao wenyewe. Kumekuwa na matamko, ambayo mara nyingi hubakia katika kanuni, ambayo lazima yatekelezwe ndani ya muktadha wa mazungumzo kati ya pande zote, ambayo bila shaka itabidi kufikiwa kwa msaada na uungwaji mkono wa jumuiya ya kitaifa.

Je, umehisije ukaribu wa Papa wakati huu?

Tumehisi ukaribu wa Papa Leo. Tumehisi ukaribu wa Papa Francisko kwanza, na kisha pia wa Papa Leo, ambao wana tabia mbili tofauti, lakini wameelezea ukaribu wao kwa njia dhahiri sana: simu, kwa kuwasiliana mara kwa mara na Paroko wa Parokia ya Gaza, ambayo, hata hivyo, haitoi habari. Na hiyo ni sawa, hiyo pia ni muhimu, kwa sababu unapaswa kufanya kitu kwa manufaa ya jambo zima, sio kutupwa kwa waandishi wa habari. Ukaribu pia umeoneshwa kwa njia thabiti sana, kwa msaada thabiti. Sasa ishara ya mwisho tuliyopokea, siku chache zilizopita, ni shauku ya Papa kutuma maelfu ya madawa  kwenye Ukanda wa Gaza.

15 Oktoba 2025, 13:15