Tafuta

2025.11.12Askofu Mkuu Paul S. Coakley wa Jiji la Oklahoma na Askofu Daniel E. Flores wa Brownsville, Texas wamechaguliwa kuwa rais na makamu wa rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Marekani. 2025.11.12Askofu Mkuu Paul S. Coakley wa Jiji la Oklahoma na Askofu Daniel E. Flores wa Brownsville, Texas wamechaguliwa kuwa rais na makamu wa rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Marekani.  (Courtesy of the USCCB)

Askofu Mkuu Coakley na Flores wachaguliwa kuwa Rais na Makamu wa Baraza la Maaskofu Marekani

Askofu Mkuu Paul Coakley ndiye rais mpya mteule wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani (USCCB)na wakati huo Askofu Daniel Flores ni Makamu wake mpya.

Vatican News

Maaskofu Katoliki nchini Marekani walimchagua Askofu Mkuu Paul S. Coakley wa Jimbo Kuu la mji wa Oklahoma kuwa  rais mpya m wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani( USCCB), tarehe 11 Novemba 2025, wakati wa  Mkutano wao Mkuu  huko Baltimore, na wakati huo huo Maaskofu pia walimchagua Askofu Daniel Flores wa Brownsville, Texas, kuhudumu kama makamu mpya wa rais. Uteuzi huo ulikuja huku Askofu Mkuu Timothy Broglio na Askofu Mkuu William Lori wakijiandaa kumalizia muda wao katika majukumu yao baada ya muhula wao wa miaka mitatu ya uongozi kuisha.

Askofu Mkuu Coakley

Askofu Mkuu Coakley mwenye umri wa miaka 70, tayari alikuwa na nafasi ya uongozi katika Baraza hilo la Maaskofu(USCCB,) akihudumu kama Katibu. Alipewa daraja la Upadre kunako  mwaka  1983, kwa jimbo la Wichita kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu wa Salina  mnamo mwaka 2004, na baadaye kuwa Askofu Mkuu wa mji wa Oklahoma mwaka 2011. Askofu Mkuu huyo ana historia ya kukuza utamaduni wa maisha, kupinga itikadi ya kijinsia, na kuwasaidia wahamiaji.

Mwaka wa 2022, Coakley aliwasifu wabunge wa Oklahoma "kwa kuunga mkono hatua za kutetea uhai" kufuatia sheria iliyopiga marufuku karibu ya utoaji mimba wote. Alisema, ili kujenga utamaduni wa uhai, mtu lazima atambue "hadhi ya asili ya kila mtu na inahitaji ulinzi unaotolewa na sheria za kutetea uhai na mabadiliko makubwa ya moyo." Coakley ameikosoa serikali ya Oklahoma kwa kuunga mkono adhabu ya kifo. Mwaka wa 2022, alisema: "Matumizi ya adhabu ya kifo yanachangia tu kuendelea kwa ukali wa jamii na kuongezeka kwa vurugu."

Askofu Flores

Askofu Flores mwenye umri wa miaka 64 aliwahi kuwa  rais wa zamani wa Kamati ya Mafundisho ya Kanisa, wa Baraza hilo ( USCCB.)  Amekuwa Askofu  tangu 2006. Alikuwa mmoja wa Maaskofu 12 waliohudumu katika Baraza la Kawaida la Sekretarieti Kuu ya Sinodi kuhusu Sinodi. Ana shahada ya udaktari katika Taalimungu na ni Profesa wa zamani wa Taalimungu. Flores atahudumu kwa muhula wa miaka mitatu kama makamu wa rais, akimrithi makamu wa rais wa zamani, Askofu Mkuu William Lori.

Mnamo mwaka 2017, Flores alisema kuunga mkono kufukuzwa kwa watu wengi ni "ushirikiano rasmi na uovu wa ndani," sawa na kumpeleka mtu kwenye kliniki ya utoaji mimba. Ameelezea wasiwasi kuhusu mgawanyiko katika Kanisa na kuhimiza "mazungumzo ya kiraia ... kutafuta yaliyo mema na kuweka kipaumbele jinsi ya kuyafikia na jinsi ya kuepuka yaliyo mabaya."

Rais na makamu mpya wa maaskfu, Marekani
12 Novemba 2025, 18:21