Tafuta

2025.10.07 Caritas Italia huko Haiti. 2025.10.07 Caritas Italia huko Haiti. 

Haiti:"Licha ya Melissa,kipaumbele ni kujenga makazi dhabiti kwa msimu ujao"

Milio ya risasi na mapigano makali dhidi ya watu wasio na ulinzi yanaendelea kuripotiwa,kutokana na magenge yenye silaha,wizi,mashambulizi na utekaji nyara.Miongoni mwa matukio haya ya hivi karibuni ni ufyatulianaji risasi kati ya Wanajeshi wa Marekani na wanachama wa genge zenye silaha,kufuatia milio ya risasi nje ya Ubalozi wa Marekani nchini Haiti.Lakini matumaini ya maisha bora hayazimiki hata mbele ya uharibifu wa kimbunga,Melisa.

Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Matukio ya hivi karibuni yameelezewa kama "mashambulizi makali sana ya ufyatulianaji risasi" katika ubalozi mwaka huu na kinaakisi hali mbaya ya usalama nchini Haiti, ambapo magenge, kama vile yale yanayoongozwa na Jimmy "Barbecue" Chérizier, yanadhibiti karibu 90% ya mji mkuu. Kufuatia kimbunga Melissa hakikuzuia mashambulizi, wizi wa magari, unyanyasaji wa kingono, na utekaji nyara kwa ulaghai. Haya yamo katika taarifa iliyochapishwa na Shirika la Habari za kimisionari Fides tarehe 17 Novemba 2025.

Ulimwengu ulioharibiswa na vita

Katika ulimwengu huu ulioharibiwa na vita, matokeo ya kiu ya wenye nguvu zaidi ya kuwadhibiti wanyonge, kuna wale ambao wameamua kujitolea wahanga wa maisha yao ili kuleta matumaini ya maisha bora kwa watu wanaopitia hali ngumu, kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea na matukio ya hali ya hewa yenye vurugu yanayoathiri maeneo haya. Miongoni mwao ni Padre Massimo Miraglio, mmisionari wa Shirika la Camillian huko Haiti, ambaye alisimulia kwamba hatimaye aliweza kurudi kijijini kwake huko Pourcine-Pic Makaya ambapo Parokia ya Mama Yetu wa Msaada wa Daima  yeye ndiye Paroko. "Tangu katikati ya Juma  lililopita, hatimaye aliweza kurudi Parokiani,akizungumza na Fides.

Barabara na miundo mbinu iliaharibiwa na kimbunga Melissa

"Barabara bado hazipitiki, sehemu kadhaa lazima wasafari wawe makini sana kwa tahadhari kubwa baada ya Kimbunga Melissa kilichosababisha uharibifu. Ingawa Jérémie aliokolewa, eneo la Parokia halikuwa salama. Bonde lote la juu, ambapo Parokia ipo, liliharibiwa kwa siku mbili na upepo mkali sana na mvua kubwa. Wengi wamepoteza mazao yao ya maharagwe, bustani zao za matunda zimeharibiwa, na mbuzi na kuku wengi wameangamia. Nyumba nyingi, katika maeneo ya mbali zaidi, juu ya uwanda mpana ambapo Pourcine-Pic Makaya iko, zimeharibiwa.

“Majuma matatu ya kuonyesha matumaini: jani kubwa la kwanza, ishara ya kuzaliwa upya. Mimea mingi ya kahawa imeharibiwa vibaya, na kitalu kimepoteza mimea yake mizuri. Watu wamepoteza sehemu kubwa ya mavuno yao."

Uharibifu lakini pia matumaini

Katika muktadha huu wa uharibifu lakini pia wa matumaini, Padre Massimo aliakisi vipaumbele: "kusafisha baadhi ya sehemu za njia zinazoelekea kwenye uwanda wa juu na maeneo yaliyolimwa ili kuruhusu asili kupona. Shule zimerejesha masomo kama kawaida," Padre aliongeza kusema, "na zaidi ya watu 50 walipata usalama Juma lililopita katika Shule au Kanisa. Kipaumbele ni kujenga makazi dhabiti kwa msimu ujao."

21 Novemba 2025, 09:21