Tafuta

Vijana wa Kenya Vijana wa Kenya  (AFP or licensors)

Kenya:Mahujaji wa matumaini na Mshikamano wa Watoto Wamisionari,Kakamega

Kupitia uwepo,ukarimu na ushuhuda wao wa furaha,watoto wamisionari wa Kakamega walitoa ushuhuda hai wa matumaini.Hija yao inasimama kama ukumbusho kwa Kanisa na jamii kwamba mshikamano unaweza kuanza katika umri mdogo kwamba hata mikono ndogo inaweza kusaidia kujenga madaraja ya huruma ya ushirika na utume wa pamoja.Ni Maneno ya Mkrugenzi wa PMS,Kakamega akishukuru Shirika la Utoto Mtakatifu katika hija ya matumaini na mshikamano kwa Jimbo la Lodwar.

Na Sr. Christine Masivo CPS, Vatican.

Jumuiya ya watoto 30 wa Shirika la  Kipapa la Utoto Mtakatifu   huko Kakamega nchini Kenya, ilifanya hija ya matumaini na mshikamano katika Jimbo la Lodwar, moja ya mikoa yenye maendeleo duni na eneo lenye changamoto kubwa lenye Parokia 33. Watoto hawa wakiwa pamoja na Padre wao na viongozi wao walipeleka chakula, mavazi, fedha za maombi na furaha yao kama zawadi kwa watoto hao. Kwa kuongozwa na kauli mbiu  mbiu ya kudumu ya Shirika la Kipapa la Kimisionari la Utoto Mtakatifu:  “Watoto Kuwasaidia Watoto” lililoanzishwa na Askofu Charles de Forbin-Janson, ni kanuni elekezi ambayo ilidumu sio tu katika siku nne kuu za hija hiyo, bali pia katika kipindi chote cha mwezi mzima cha matayarisho ya kusaidia watoto kufanya kazi bila kuchoka kwa wenzao huko Lodwar.

Kuimarisha utambulisho kupitia roho ya umisionari

"Ziara hii ilikuwa ishara ya nguvu ya ushirikiano na uwajibikaji wa pamoja," alisema Askofu John Mbinda wa Lodwar. "Ni dhihirisho thabiti ya kuonesha umisionari na kuimarisha roho ya ukarimu, hasa wakati ambapo rasilimali zimepungua sana. Watoto hawa wameweka mfano mzuri ambao majimbo na vikundi vinaitwa kuiga."

Mpango huo ulikaribishwa kwa moyo mkunjufu na Mkurugenzi wa mashirika ya Kipapa ya Kimisionari ( PMS )wa Jimbo la Lordwar, ambaye aliitaja ziara hiyo kuwa ni ‘baraka kubwa’ na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano na kusaidiana kati ya majimbo nchini na Afrika kwa jumla.

Umoja katika mikoa yote

Mahujaji hawa wachanga walishiriki kikamilifu na Kanisa la Lodwar kwa kuwapa rozari, nyenzo za elimu na chakula kwa watoto huko Lodwar, na kukuza vifungo vya urafiki na maelewano. Misa Takatifu iliadhimishwa katika mji wa Lodwar, ikiongozwa na Askofu wa Jimbo hilo, aliyewaleta pamoja watoto kutoka majimbo haya mawili katika sala na shukrani, wakionesha umoja wa Kanisa katika mikoa mbalimbali. Mahujaji walitembelea pia Madhabahu ya Mama Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili , ambapo watoto walikutana na familia na kusambaza zawadi walizoleta. Mikutano hii ilibadilisha matendo ya hisani kuwa nyakati za kweli  na za udugu, mazungumzo na furaha.

Matokeo ya  kukutana

Padre  Godfrey Sechero, Mkurugenzi PMS huko Kakamega na kiongozi wa kikundi hicho cha Utoto Mtakatifu  alisisitiza athari kubwa ya makabiliano kati ya watoto hao. "Tunataka watoto waelewe kwamba sisi ni watu wamoja, ingawa tunaishi katika maeneo tofauti ya kijiografia na hali ya hewa." Aliongeza kuwa uzoefu huo ulisisimua tena imani na shauku ya kimisionari katika mioyo ya vijana washiriki. Kupitia uwepo, ukarimu na ushuhuda wao wa furaha, watoto wamisionari wa Kakamega walitoa ushuhuda hai wa matumaini. Hija yao inasimama kama ukumbusho kwa Kanisa na jamii kwamba mshikamano unaweza kuanza katika umri mdogo kwamba hata mikono ndogo inaweza kusaidia kujenga madaraja ya huruma ya ushirika na utume wa pamoja.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Bonyeza hapa: Just click here

 

16 Desemba 2025, 09:27