Kitabu ‘Living Ancestors’-Sauti za Masista wa Kiafrika ni uthibitisho wa uthabiti
Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.
Ni mzaliwa wa Kenya na sasa aanatoa huduma ya umisionari nchini Marekani, Sr. Mumbi anahudumu kama Rais wa ‘Friends in Solidarity,’ maana yake Marafiki wa mshikamano, Shirika la usaidizi lisilo la faida la Kikatoliki, lenye makao yake makuu nchini Marekani na utume wa kuwawezesha watu wa Sudan Kusini. Sr huyo alisema kwamba ana shauku ya kuinua sauti za watawa wa kiafrika, ambao wamejitolea kwa Mungu kwa uamimifu katika maisha yao bila kuyumbayumba. Kazi zao mara nyingi zimekuwa kimya, mbali na kutambuliwa kwa jamii. Lakini kupitia kikundi cha ‘Watawa wa Taa’ kinachodhaminiwa na 'Mfuko wa Hilton Conrad, Sr. Mumbi ameunda jukwaa na kuwapa watawa wa Kiafrika fursa ya majadiliano na mazungumzo kwa ajili ya mafanikio ya utume wao. Hii ilikuwa incubator ya kitabu "Living Ancestors" na mahali pa kuanza uaandishi.
![]()
Sr. Mumbi Kigutha CPPS
Kuzaliwa kwa mababu walio hai
Mpango ulianza kwa swali zito: "Je, haitakuwa nzuri ikiwa tungesimulia historia za vizazi vikongwe vya kitawa barani Afrika?" Akiongozwa na Sr. Jane Wakahiu, LSOSF, mmoja wa washiriki wa kitabu hicho, Sr. Mumbi aliwaalika watawa ambao wamehudumu kwa zaidi ya miaka 30 katika maisha ya utume kutafakari kitaalimungu katika safari yao. Kitabu cha kwanza, ambacho tayari kimechapishwa, kinaelezea maisha ya watawa 15 wa wa kitawa barani Afrika yote, kutoka mashirika, tamaduni na huduma mbalimbali. Kati yao kuna waaanzilishi wa mashirika na wengine wakiwa watawa wa kwanza kwenye shirika lakini wote wameitika wito thabiti kuwa watawa. Akuzungumza na Vatican News, Sr Mumbi alisema kuwa "Watawa hawa wanaishi maisha ya kujitolea katika pembe tofauti za dunia. Historia zao si za kujipongeza, ni shuhuda takatifu za uvumilivu, imani na upendo.” Katika kitabu hiki kuna watawa ambao wamefundisha katika shule za vijijini, waliohudumia wagonjwa wakati wa machafuko ya wenyewe kwa wenyewe, walionzisha mashirika na kukuza jamii katika imani. “Historia zao si kumbukumbu tu bali ni theolojia hai,” alisema.
Historia zisizojulikana
Kanisa Barani Afrika daima limeungwa mkono na uwepo wa utulivu wa masista wa Kiafrika. Wanaendesha hospitali, shule, vituo vya watoto yatima na huduma katika parokia katika mazingira yenye changamoto nyingi. Historia zao hazijulikani zaidi ya mashirika au nchi zao. Kitabu cha ‘Living Ancestors’ kinathibitisha michango wao muhimu kwa Kanisa Katoliki ulimwenguni kote na hutoa utambuzi wa muda mrefu. Sr Mumbi anaziba pengo la vizazi kwa kuandika uzoefu wao mzuri, akiwaonyesha dada wadogo mahali ambapo mizizi yao iko na kuruhusu ulimwengu kuthamini matunda ya maisha ya kidini ya Kiafrika.
Changamoto
"Kila mafanikio yana changamoto zake," Sr. Mumbi aliakisi. "Mradi huu ulikabiliana na vizuizi vya lugha na miundombinu." Historia ya kikoloni ya Afrika ilileta migawanyiko ya lugha ambayo mara nyingi huzuia ushirikiano wa maana kati ya watawa wanaozungumza Kiingereza, Kifaransa na Kireno. "Wakati mwingine nilitegemea Programu za kutafsiri," alibainisha. "Lakini njia za mawasiliano yalipatikana." Ilikuwa ngumu kupata imani ya watawa, wengi hawakuwahi kukutana naye wala kuandika tafakari za kibinafsi hapo awali. “Nilikuwa nikiomba kitu kitakatifu,” alisisitiza. "Lakini Mungu alitoa na ikawa kazi ya Roho Mtakatifu."
![]()
Sr. Mumbi Kigutha CPPS akia anafanya kazi na watawa wa kike wa kiafrika
Maono yake
Maono yake yanaenea katika bara zima. "Nina ndoto ya kuchapisha vitabu kumi, kuakisi angalau mtawa mmoja katika kila nchi ya Afrika. Nataka hii iwe kumbukumbu ya urithi wetu wa kiroho." Pia anapanga programu za siku zijazo za “Watawa wa Taa”, zinazoangazia maisha ya kidini, uongozi na ustawi kamili, ikiwa ni pamoja na wavuti za bara juu ya afya ya akili, lishe na hali ya kiroho.
Utawa duniani
Ingawa imekita mizizi katika muktadha wa Kiafrika, Mababu Wanaoishi hubeba umuhimu wa kimataifa. "Madada wa Kiafrika ni sehemu ya udugu wa kimataifa." Sr. Mumbi alisisitiza. "Kwa kujikita katika mazingira yetu wenyewe, shida, furaha na historia zetu, tunatoa uhalisi kwa ulimwengu. Tunaimarisha Kanisa kwa kuwa vile tulivyo." Kwa wale walio nje ya Afrika, kitabu hiki kinatumika kama dirisha la mapokeo ya imani changamfu na dhabiti, ikiweka wazi huduma ya watawa wanaohudumu kwa unyenyekevu na neema. Papa Francis alisisitiza umuhimu wa kutambua mchango wa wanawake ndani ya watu wa Mungu, akilikumbusha kwamba kanisa ni mwanamke, binti, bi harusi na mama.
Kuadhimisha watakatifu walio hai kati yetu
Sr. Mumbi alihitimisha kwa kutoa wito: "Lazima tuwape watawa mataji yao wangali hai." Kitabu cha ‘Living Ancestors’ kinawaheshimu watawa wanawake walioweka misingi bora katika maisha ya kisasa ya kidini ya Kiafrika na kuhamasisha vizazi vipya kufuata nyayo zao. Utakatifu wao, anatukumbusha, haupatikana tu katika makanisa au vyeo vya utakatifu, lakini katika uthabiti wa kila siku wa wanawake wanaoinuka kufundisha, kuponya, kuomba na kutumikia.
Kitabu chake kinapatika kwa njia ya mtandao:The book is available online na wanawake watawa wa Kiafrika wanaalikwa kuchangia vitabu vijavyo na kujiunga na mazungumzo yanayoendelea ndani ya "Watawa wa Taa."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku,bonyeza hapa: Just click here