Tafuta

Upepo mkali ulisababisha uharibifu mkubwa nchini Madagascar huku Kimbunga cha Kitropiki Gezani kikipiga kisiwa hicho vibaya sana. Upepo mkali ulisababisha uharibifu mkubwa nchini Madagascar huku Kimbunga cha Kitropiki Gezani kikipiga kisiwa hicho vibaya sana. 

Madagascar:Kimbunga cha kitropiki Gezani kusababisha uharibifu mkubwa

Kimbunga cha kitropiki Gezani kimeharibu Wilaya 25 katika maeneo matano ya Madagascar, na kusababisha vifo vingi,maelfu ya watu walihama makazi yao na miundombinu muhimu kuharibiwa vibaya.Huku tathmini na majibu ya dharura yakiendelea,wito wa mshikamano umeibuka kutoka kwa viongozi wa Kanisa na Mashirika ya Kimataifa ya kibinadamu.

Na Sr. Christine Masivo CPS – Vatican.

Mnamo Dominika tarehe 15 Februarri, Papa Leo XIV alionesha ukaribu wake na watu wa Madagascar wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, akiwageukia waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Alitambua mateso yaliyosababishwa na Kimbunga Fytia na Gezani, akitoa “sala kwa ajili ya waathiriwa, familia zao, na wote waliopata hasara kubwa.”

Kiwango cha Uharibufu wa kimbunga Gezani

Kiwango kamili cha uharibifu uliosababishwa na Kimbunga cha Kitropiki Gezani bado kinatathminiwa, huku timu za dharura zikiendelea kutathmini uharibifu Madagascar. Kulingana na ripoti iliyotolewa mnamo tarehe 16 Februari 2026 na Ofisi ya Kitaifa ya Usimamizi wa Hatari na Maafa (BNGRC), inabainisha kwamba Wilaya 25 katika maeneo matano ya taifa la kisiwa cha Bahari ya Hindi zimeharibiwa. Hadi wakati wa kutolewa taarifa hiyo, majengo 49,129 yalipata uharibifu, ikiwa ni pamoja na hospitali mbili na ofisi saba za serikali. Idadi ya watu ni kubwa vile vile, kwani watu 59 walikufa wakati wengine 15 bado hawajulikani walipo, na watu 804 wamejeruhiwa. Kwa jumla, watu 423,986, wanaowakilisha familia 104,706, wameathiriwa, huku nyumba 27,756 zikifurika maji. Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na IFRC Afrika, linakadiria kuwa watu 16,428, au familia 4,045, wameyakimbia makazi yao. Mji wa bandari wa Toamasina, jiji la pili kwa ukubwa nchini Madagascar, umeathiriwa zaidi. Wakazi wengi bado hawana maji ya kunywa na katika baadhi ya maeneo, umeme, na hivyo kuzidisha mgogoro wa kibinadamu.

Juhudi za Mshikamano wa Kanisa na Kimataifa

Kujibu maafa hayo, Baraza la Maaskofu wa Madagascar lilitoa barua mnamo tarehe 11Februari 2026, likiomba mshikamano na waathiriwa wa kimbunga. Barua hiyo, iliyosainiwa na Askofu Jean-Claude Rakotoarisoa, na Katibu Mkurugenzi wa Kitaifa ya Matendo ya Kitume, ya Kipapa ikiwataka waamini Wakatoliki kusaidia jamii zilizoathiriwa, hasa katika jimbo la Toamasina Mashariki mwa Madagascar. Maaskofu waliwakabidhi viongozi wa jimbo uratibu wa juhudi za misaada, wakiwasihi waamini kufuata mwongozo wao katika kutoa msaada.

Athari za Kikanda na hatari zinazoendelea

Madagascar ilikuwa tayari imekumbwa na kimbunga kingine cha kitropiki kaskazini-magharibi, ambacho kilisababisha vifo vya angalau watu saba na kuwafukuza watu zaidi ya 20,000. Ingawa Gezani haikutua moja kwa moja katika nchi jirani ya Msumbiji, ilisababisha vifo vinne na uharibifu mkubwa wa miundombinu na nyumba katika majimbo ya Inhambane na Sofala. Rais wa Msumbiji Daniel Chapo, akizungumza kando ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, alithibitisha idadi ndogo ya majeruhi nchini mwake, akiihusisha na kufuata maagizo ya usalama ya serikali. Gavana wa Mkoa Francisco Pagula pia aliripoti uharibifu wa miundombinu ya umma na mali za makazi, huku akisisitiza umuhimu wa maonyo ya mapema na uokoaji wa kuzuia katika kupunguza athari za janga hilo.

Kusini Mashariki mwa Afrika

Kusini Mashariki mwa Afrika inakabiliwa na msimu wa dhoruba za kitropiki wa kila mwaka unaoanzia Oktoba hadi Aprili, tishio linalojirudia ambalo huleta uharibifu mkubwa wa mali na upotevu wa maisha kila mwaka. Vimbunga vya hivi karibuni vimetumika kama ukumbusho mwingine dhahiri wa udhaifu wa eneo hilo na umuhimu wa maandalizi, mwitikio ulioratibiwa, na mshikamano endelevu wa Kimataifa.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

18 Februari 2026, 13:20