Programu Mpya ya Miujiza ya Ekaristi ya Mtakatifu Carlo Acutis yazinduliwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Huku ulimwengu ukisherehekea Siku ya Wapendanao, tarehe 14 Februari 2026, Madhabahu na Kituo cha Ekaristi(Shrine & Center),vilivyowekwa kwa ajili ya Mtakatifu Carlo Acutis huko Malvern,(PA),Marekani, kilitangaza uzinduzi wa programu mpya kwa njia ya simu(new mobile app), inayojikita na kushiriki Uwepo Halisi wa Kristo katika Ekaristi. Programu hii iliyotengenezwa kwa ushirikiano na Antonia Acutis, mama yake Mtakatifu Carlo Acutis, inakusanya pamoja historia zilizoandikwa tayari kupitia inteneti za miujiza ya Ekaristi ambazo ziliandikwa na Mtakatifu Carlo mwenyewe katika Maonesho yake ya Miujiza ya Ekaristi Ulimwenguni.
"Ishi kama Carlo"
Kwa njia hiyo pamoja na "Ishi kama Carlo," safari shirikishi kupitia nyakati muhimu za maisha ya Carlo, pia kuna nafasi maalum ya Ibada ya Ekaristi mtandaoni kutoka makanisa yote ulimwenguni, ikiwaalika watumiaji katika mkutano wa kina na Uwepo Halisi wa Kristo. Ingawa Siku ya Wapendanao kwa kawaida huzingatia upendo wa kibinadamu, Programu hii, inawaalika watumiaji kutafakari kile ambacho Madhabahu hukiita "historia kuu zaidi ya upendo kuwahi kusimuliwa," uwepo wa kudumu wa Kristo katika Ekaristi. Carlo Acutis, ambaye alifariki mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 15, alitumia teknolojia kuorodhesha na kutangaza miujiza ya Ekaristi ambayo ilikuwa imechunguzwa na kuidhinishwa na Kanisa, ambayo mingi yake pia ilifanyiwa uchunguzi wa kisayansi.
Kabla ya Teknolojia ya simu na mitandao ya kijamii
Muda mrefu kabla ya ujio wa teknolojia ya simu na mitandao ya kijamii, Mtakatifu Carlo alitambua intaneti kama chombo chenye nguvu cha uinjilishaji. "Carlo alitumia teknolojia ya wakati wake kuwaleta watu karibu na Yesu katika Ekaristi," alisema Mary Bea Damico, Mkurugenzi Mtendaji wa Madhabahu ya Mtakatifu Carlo Acutis katika Nyumba ya Marejeo ya Malvern nchini Marekani."Kwa Programu hii, tunaendeleza utume huo, kwa kutumia teknolojia ya kisasa kutangaza Ekaristi kuwa ni moyo hai wa Yesu.
Program inashirikisha maisha ya Mtakatifu Carlo Acutis
Programu hii pia inashiriki safari nzuri ya maisha ya Mtakatifu Carlo, na inawaalika kila mtu kusonga mbele katika safari yao wenyewe ili kuwa watakatifu ambao waliumbwa wawe.” Antonia Acutis Mama yake Mtakatifu Carlo alielezea kuunga mkono kwake mpango huu: “Carlo alipenda kutumia teknolojia kuzungumza kuhusu Yesu na hasa kuhusu Ekaristi. Inaniletea furaha kuona kujitolea kwake kukiwa pamoja kwa njia ambayo inaweza kuwafikia vijana na familia kila mahali. Ni muhimu sana tuendelee kusambaza habari za Miujiza ya Ekaristi kote ulimwenguni( Eucharistic Miracles of the World International Exhibition.)
Programu hii itakuwa zana nzuri katika kuendeleza utume huu.” Askofu Mkuu Nelson J. Perez, D.D., wa Philadelphi ambaye anajulikana kwa kujitolea kwake na upendo wake kwa vijana alisema haya alipoona Programu hii kwa mara ya kwanza: “Hii ni nzuri sana. Kuungana na vijana, kuwahudumia vijana wetu ni kipaumbele changu cha juu. Madhabahu ya Carlo Acutis na Programu hii itasaidia mapadre wetu, walimu na wazazi tunapozungumza na watoto wetu kuhusu imani yetu ya Kikatoliki, inayounga mkono wito wetu wa kutenda, na kuishi imani yetu kila siku.”
Uhusiano wa Program na siku ya wapendao
Uzinduzi wa Programu hiyo katika Siku ya Wapendanao pia una uhusiano wa Upendo. Mtakatifu Valentine mwenyewe alikuwa Askofu kutoka Terni, katika eneo la Umbria nchini Italia, Kilomita chache tu kutoka Assisi, mahali pa kudumu pa mapumzika ya mwili wa Mtakatifu Carlo Acutis. Programu ya Muujiza wa Ekaristi ya Mtakatifu Carlo Acutis inapatikana sasa kwa vifaa vya iOS na Android na inatoa njia linalopatikana kwa watu binafsi, familia, parokia, na waelimishaji kuchunguza miujiza ya Ekaristi na kukua katika ibada na utakatifu wao wenyewe.
Kuhusu Madhabahu
Madhabahu ya Mtakatifu Carlo Acutis na Kituo cha Ekaristi katika Nyumba ya Mafungo ya Malvern, Jimbo Kuu la Philadelphia, vilifunguliwa mnamo Agosti 2022. Katika madhabahu hayo ni nyumbani kwa maonesho ya kwanza ya kudumu ya Miujiza ya Kimataifa ya Ekaristi ya Mtakatifu Carlo Acutis duniani. Madhabahu ya Malvern imekusanya pamoja miujiza zaidi ya 130 iliyoandikwa ya Mtakatifu Carlo, pamoja na Historia nzuri ya maisha ya ajabu ya Carlo - na wito wa utakatifu kwa kila mmoja wetu. Mwaka 2025, katika madhahau hayo paliandaa ziara na mawasilisho kutoka kwa zaidi ya vikundi 150 vya mafungo, shule, vikundi vya vijana, parokia na zaidi. Ikiwa katika mwaka wake wa 114, Nyumba ya Mafungo ya Malvern ni Kituo cha Mafungo cha Kikatoliki kinachomilikiwa na kuendeshwa na watu wa kawaida Walei Kiko Malvern, (PA) chenye ekari 125 zenye miti, uwanja mtakatifu umekuwa sehemu muhimu ya safari ya imani ya mamia ya maelfu ya wanaume, wanawake, vijana na familia.
Ni eneo Takatifu la Ekaristi, na umakini wa Ekaristi wa mafungo ya Malvern umetoa miito mingi ya kitawa, na uponyaji - hasa uponyaji wa moyo. Taarifa za ziada na mahojiano na vyombo vya habari kuhusu Madhabahu ya Mtakatifu Carlo Acutis, Huduma na Programu ya Simu zinaweza kupangwa kupitia Mary Bea Damico, Mkurugenzi Mtendaji, Madhabahu ya Mtakatifu Carlo Acutis na Kituo cha Mkutano wa Ekaristi katika Madhabahu ya Malvern(484) 630-4570.
Kwa maelezo zaidi au kupakua programu hiyo unaweza hapa:https://stcarloshrine.com/app
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here