Tafuta

Mtoto wa mwanamke mhamiaji kutoka Ghana ambaye alifika Mexico akitarajia kuvuka mpaka wa Kaskazini na kuungana tena na mumewe,ambaye tayari anaishi Marekani. Mtoto wa mwanamke mhamiaji kutoka Ghana ambaye alifika Mexico akitarajia kuvuka mpaka wa Kaskazini na kuungana tena na mumewe,ambaye tayari anaishi Marekani.  (Foto: Rocío García Villegas) #SistersProject

Wanawake wanaoponya majeraha ya wahamiaji

Vurugu,umaskini na ukosefu wa fursa vinawalazimisha maelfu ya Waamerika Kusini kuhamia Marekani na kusababisha mgogoro wa uhamiaji ambao Mtandao wa Maisha ya Watawa,wanashughulikia kwa utaalamu na huruma,kupitia Nyumba ya Mapokezi,Mafunzo na Maendeleo kwa Wanawake na Familia za Wahamiaji na Wakimbizi(CAFEMÍN).

Na Rocío García Villegas

"Katika safari ya wahamiaji nimeona miili iliyochoka, lakini zaidi ya yote mioyo iliyojeruhiwa; kuponya majeraha hayo ni kuwakumbusha kwamba maisha yao yana thamani," ndivyo Sr María Soledad Morales Ríos anaelezea utume uliotekelezwa na Mabinti wa Maria wa Bwana  wa Mtakatifu Yosefu kupitia Nyumba ya Mapokezi, Mafunzo na Maendeleo kwa Wanawake na Familia za Wahamiaji na Wakimbizi(CAFEMÍN).

Virginia García, Sr Josefina; Orlanda Carrillo Navarro, Sista wa Shirika la Mungu Mchungaji; Sr Lucia Maldonado Castañeda, wa Shirika la Mtakatifu Yosefu wa Lyon; na Sr Ernestina Diego Martínez, wa Shirika la Mungu Mchungaji, wanachama wa kikundi cha Mtandao wa Watawa wanaoshirikiana katika Mpango wa CAFEMIN.(Picha: Rocío García Villegas).

Kusindikiza wahamaiji zaidi ya 20,000 kutoka nchi 70

Kwa miaka 13, mahali hapa katika Jiji la Mexico limewasindikiza wahamiaji zaidi ya 20,000 kutoka nchi 70, na kuwa kimbilio la heshima. Kwa msukumo wa uzoefu wa Familia Takatifu ya Nazareti na tafsiri mpya ya karama yake, Shirika hutoa mwitikio thabiti kwa mateso ya wanadamu. Kwa hivyo, kwa CAFEMÍN, hakuna kisichowezekana: ingawa ina uwezo wa watu 100, imewasindikiza hadi 800 katika dharura.

Wanawake wahamiaji wasio na wanzi walioondoka nchini mwao walitembea na watoto wao, wakiwalinda kutokana na hatari nyingi.Picha: Rocío García Villegas

Misheni iliyounganishwa njiani

Wakati muhimu katika ujumuishaji wa misheni hii ulitokea mwaka wa 2012, wakati Sista María Magdalena Silva Rentería, mkurugenzi wa sasa wa CAFEMÍN, aliposhiriki katika Kituo cha Wahamiaji cha Msalaba kwenye mpaka wa Guatemala. Uzoefu huo ulisababisha msafara wa kwanza wa wahamiaji: matembezi ya siku 36, yenye watu zaidi ya 800 wanaohitaji ulinzi. "Haikuwa nadharia tena; ilikuwa kugusa maumivu, kupanga maisha, na kutetea heshima njiani," Sista Magda alikumbuka. Wakati wa safari, uwepo wake ulisaidia kuongeza uelewa wa hali ya wahamiaji, kupunguza hatari zinazowakabili makundi ya wahalifu, na kuboresha matibabu yao na mamlaka. Kwa sababu hii, chakula, maji, na maeneo ya kupumzika yalihakikishwa hadi walipofika Jiji la Mexico. Uzoefu huo uliashiria wazi jinsi CAFEMÍN leo inavyoelewa michakato yake ya malezi, udhibiti na ujenzi upya wa maisha.

Msalaba ulioongoza Msafara wa Kwanza wa Wahamiaji kwenda Mexico mnamo 2012 na kuambatana na safari zingine katika miaka iliyofuata. Nyuma inasomeka "Njia ya Msalaba 2013," mbele inasomeka "Njia ya Msalaba 2015." Picha: Rocío García Villegas.

Makristo Watesekao wa Wakati Wetu

Sera za sasa za uhamiaji za Marekani zina ufikiaji mdogo wa madai ya wakimbizi wa Amerika Kusini, na kuwalazimisha kuvuka mipaka hadi kumi, ikiwa ni pamoja na Darién Pass, msitu  wenye zaidi ya Hekta 575 elfu kati ya Colombia na  Panama. Huko, wanakabiliwa na mito iliyojaa maji, miteremko hatari, na barabara zenye matope zinazosababisha majeraha, mkanganyiko, na, katika visa vingi, kifo. Hatari hizi zinazidishwa na uwepo wa magenge ya wahalifu na mitandao ya biashara haramu ya binadamu. Kwa sababu hii, Dada Mercedes anawaelezea wahamiaji kama Kristo anayeteseka leo: "si Kristo wa utotoni, bali yule aliyepigwa na kusulubiwa." Leticia, mhamiaji kutoka Venezuela, alisimulia jinsi alivyovuka Darién na watoto wake wawili, baba yake, na watu wengine kumi na mmoja. "Tulishiriki chakula, uchovu, na hofu."

Hatari haikuisha walipoondoka katika eneo hilo. "Niligundua kuwa Darién haikuwa msitu pekee; Mexico pia ingekuwapo, lakini wakati huu imetengenezwa kwa zege," Leticia alisema. Njaa, utekaji nyara, unyang'anyi, na vitisho viliashiria kupita kwake nchini. "Kuna nyakati ambapo nilifikiri hatungetoka hai. Watoto wangu waliona vurugu ambazo hakuna mtoto anayepaswa kuona." Kulingana na timu ya Usaidizi wa Kisaikolojia ya CAFEMÍN, 90% ya wanawake wanaowasaidia wamepitia vurugu wakati wa safari yao. Historia kama za Leticia hurudiwa kila siku katika Cafemin na katika hosteli nyingi kote Mexico.

CAFEMIN katika eneo la Ujumuishaji wa Mitaa, huendeleza programu za mafunzo, sifa, na vyeti kwa idadi ya watu, na kuwawezesha kupata njia ya kujikimu. Hili ni kundi la wanawake katika karakana ya kushona; hutengeneza mifuko iliyotengenezwa kwa mikono. Kulingana na takwimu kutoka Kitengo cha Sera ya Uhamiaji, Usajili, na Utambulisho wa Watu (UpMRIP), kati ya Januari na Agosti 2024, watu 925,085 walisajiliwa kama wahamiaji wasio wa kawaida nchini Mexico, wakiwemo zaidi ya wasichana, wavulana, na vijana 108,444,000.

Vijana wahamiaji wanashughulikia oda ya Chakula cha Mchana cha Boksi katika duka la mikate kama sehemu ya mpango wa Mtandao wa Waajiri. Picha:Rocío García Villegas

Nafasi ya kupona na kuanza upya

"Hapa niliweza kusimama, kufikiria, na kufanya maamuzi kwa ajili ya mustakabali wa watoto wangu. Niligundua tena furaha na amani yangu; sikuwa nimecheka kwa miaka mingi," Leticia alishiriki. Kwake yeye na maelfu ya wengine, CAFEMÍN ni mahali salama, ambapo mfumo wake wa kitaasisi umeongozwa na ujumbe Papa Francisko kwa ajili ya Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi 2018, alipopendekeza jibu lililoelezwa katika vitenzi vinne: kukaribisha, kulinda, kukuza, na kuunganisha. Kanuni hizi hutafsiriwa katika utunzaji wa kimwili, kisaikolojia, kiroho, na kisheria, pamoja na michakato ya ujumuishaji wa kijamii inayolenga kujenga upya mpango wa maisha wa kila mtu.

Uongozi wa SSisita huyo umeunda mtandao wa Makanisa na taaluma mbalimbali, ambao umegusa maumivu lakini pia umeshuhudia maisha yakizaliwa upya. Safari ya mhamiaji haiishii Cafemin. Hapa, safari ya kusindikiza inaanza, lakini ndoto ya kuwapatia mabinti na wana mustakabali wa heshima, amani, na fursa inaendelea. Isaiah, mvulana mhamiaji wa Venezuela mwenye umri wa miaka 11, anafupisha kwa maneno rahisi yanayodumisha matumaini: "Sikujua kama ningefika hapa... lakini nilifanya hivyo."

23 Februari 2026, 10:12