Mkusanyo wa Sadaka ya Ijumaa Kuu 2026 kwa ajili ya Nchi Takatifu
Vatican
"Ijumaa Kuu wakati tunatafakari Msulibiwa, tunaomba kukumbuka katika sala na kwa upendo wa dhati wale wanaoendelea kushuhudia Injili katika maeneo ya Ukombozi wetu. Ukaribu wetu, kaka na dada ni ishara ya dhati ya tumaini na ya amani."
Huu ndiyo wito msingi wa dhati ambao Ndugu Mdogo Francesco Ielpo,OFM, Msimamizi wa Nchi Takatifu, anawaelekea Wakristo wote Ulimwenguni kote akiwa Nchi Takatifu kwa ajili ya kuomba "kusaidia tumaini, kwa kutoa sadaka na ili kuweza kukuza amani."
Jinsi gani ya kusaidia Nchi Takatifu ?
Kanisa limeweka wazi kwa wote chombo kile cha kuweza kufanya mkusanyo wa Sadaka ya Ijumaa Kuu, siku ambayo inakumbuka Mateso ya Bwana, ambapo kwa mwaka huu itakuwa Ijumaa tarehe 3 Aprili 2026 ili kuweza kusaidia kwa dhati watu na maisha yao katika maeneo Matakatifu
Mkusanyo wa sadaka ulianzishwa kwa utashi wa Papa, Mtakatifu Paulo VI, kwa Waraka wake wa Kitume wa Nobis in Animo kunako Machi 1974, ambaye alipendekeza Maaskofu, Makleri na waamini wote ulimwenguni kote. Mkusanyao huo ulianzishwa kwa lengo la kuongeza nguvu za uhusiano kati ya Wakristi wa Ulimwenguni kote na Maeneo matakatifu na ambapo ni mkusanyo wa sadaka rasmi wa Kanisa Katoliki.
Ni nini maana ya Mkusanyo wa sadaka ya Ijumaa Kuu?
Mkusanyo wa sadaka hii, unawakilisha rasilimali msingi kwa ajili ya kusaida shughuli na maisha ambayo yanazungukia Maeneo matakatifu. Sadaka zinazokusanywa na Jumuiya za Maparokia na za Maaskofu, zinatumwa kwa Ndugu Wadogo kupitia Tume ya Kifransiskani ya Nchi Takatifu. Kwa njia hiyo, sadaka hizo zinatumiwa ili kuhifadhi maeneo matakatifu na kwa ajili ya kusaidia Jumuiya za Kikristo mahalia, ambaz mara nyingi zinafafanuliwa kama “ mawei hai” katika kanda hiyo.
Ina maana gani kutoka sadaka ya Ijumaa Kuu Takatifu?
Si kusaidia tu, lakini hata kama zipo kuna uhitaji mkubwa. Mbali na hayo haitoshi kukabiliana na dharura tu: inahitajika kupanda msyakabali na kwa hiyo kuna uwezekano tu, kwa lengo la kielimu.
Ni nini na ni kusaidia nani kwa kutoa sadaka ya Ijumaa Kuu Takatifu?
Kuna nyumba 630 za kulala wanafamilia wenye kuhitaji; shule 15 zenye wanafunzi 12,000; nafasi za kazi 1100; Nyumba za wakagonjwa na yatima 5; Taasisi za Elimu 3; na Usimamizi wa Nchi Takatifu. Maeeneo yanayowezeshwa ya Wakristo chini ya mitindo mbali mbali ya usaidizi wa sadaka zinazotolewa ni kama zifuatazo: Yerusalemu, Palestina, Israeli, Yordan, Ciyprus, Siria, Libanon, Misri, Ethiopia, Eritrea, Utuki, Iran na Iraq.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.