Askofu Mkuu Coakley wa Marekani:Amevunjika moyo kwa maneno ya Trump kuhusu Papa
Vatican News
"Nimevunjika moyo kwamba Rais amechagua kuandika maneno ya kumdhalilisha Baba Mtakatifu. Papa Leo XIV si mpinzani wake, wala Papa si mwanasiasa. Yeye ni Mwakilishi wa Kristo anayezungumza kutoka katika ukweli wa Injili na kwa ajili ya utunzaji wa roho." Hivi ndivyo Askofu Mkuu Paul Stagg Coakley, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani, alivyosema katika taarifa akijibu chapisho la mitandao ya kijamii "Ukweli" ambapo Rais Donald Trump alimkosoa vikali Papa Leo XIV.
Taarifa ya Baraza la Maaskofu Italia CEI
Naye Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Italia(CEI), alirudia kusema katika taarifa "kuunga mkono kamili na Baba Mtakatifu Leo XIV, akielezea masikitiko yake kwa maneno aliyoandika Rais wa Marekani, Donald Trump." Akirudia kauli ya Rais wa Baraza la Maaskofu wa Marekani, alikumbuka kwamba, "Papa si mpinzani wa kisiasa, bali ni Mrithi wa Petro, aliyeitwa kutumikia Injili, ukweli, na amani. Katika wakati uliojaa migogoro na mvutano wa kimataifa, sauti yake inawakilisha wito unaohitaji utu wa binadamu, mazungumzo, na uwajibikaji. Makanisa nchini Italia yanarudia ukaribu wao, upendo, na maombi kwa ajili ya Baba Mtakatifu, huku yakitumaini heshima ya kila mtu kwa nafsi yake na huduma yake."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.