Tafuta

Siku ya LX ya Hupashanaji habari Ulimwenguni. Siku ya LX ya Hupashanaji habari Ulimwenguni. 

Akili Unde haipaswi kuchukua nafasi ya nyuso na sauti

Katika Ujumbe wa Papa Leo XIV wa Siku ya 60 ya Hupashanaji habari Ulimwenguni,Mei 17,anatoa mwito wa“kulinda nyuso zetu na sauti zetu”katika safari iliyo mbele ili kujitayarisha kwa safari hii kupitia mafunzo ambayo ni ya kielimu badala ya kiteknolojia.Amesisitiza hayo Dk Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano yaliyochapishwa katika Shirika la Habari Katoliki,Italia(SIR).Tunachapisha maoni kamili.

Paolo Ruffini

Katika Ujumbe wake wa kwanza wa Siku ya Hupashanaji Habari Ulimwenguni Papa Leo XIV anaonya kuhusu hatari ya tasnia ya ubunifu wa binadamu kubomolewa na kubadilishwa na lebo "Inayoendeshwa na AI." Jibu ni nini? Shule ya mawazo muhimu na vyombo vya habari vyenye mamlaka. Kuna kifungu kinachoonekana kuwa cha pili, karibu kuwa kando, katika ujumbe wa kwanza wa Papa Leo XIV wa Siku ya Hupashanaji Habari Ulimwenguni.

Ni ule ambao, akizungumzia jinsi mifumo ya akili unde inavyopata udhibiti wa mawasiliano katika utengenezaji wa maandishi, muziki, na video, Papa Leo XIV anasisitiza hatari ya sehemu kubwa ya tasnia ya ubunifu wa binadamu kubomolewa na kubadilishwa na lebo "Inayoendeshwa na AI." Kwa kuwabadilisha watu na ndiyo hiyo hoja muhimu na ya kutisha, kuwa "watumiaji tulivu wa mawazo yasiyofikirika, bidhaa zisizojulikana, zisizoidhinishwa, na zisizopenda." Hapa ndipo mwito wa Papa unapotoka: kulinda nyuso zetu na sauti zetu katika safari iliyo mbele; kujitayarisha kwa safari hii kupitia mafunzo ambayo ni ya kielimu badala ya kiteknolojia. Ni kuhusu kuelewa kabla haijachelewa, kwamba tatizo si jinsi ya kuzoea mazingira mapya, bali jinsi ya kuyaunda; jinsi ya kuishi katika ulimwengu wa kidijitali bila kujazwa na mawazo yasiyofikirika.

"Ni juu yetu kutumia akili zetu na kuongoza teknolojia"

Kama Papa alivyowaambia wanafunzi walioshiriki katika Jubilei ya Elimu, "Hatuwezi kuruhusu algoriti ziandike historia yetu! Sisi ndio waandishi wa historia zetu. Ni juu yetu kutumia akili zetu kuongoza teknolojia kwa busara, bila kuruhusu teknolojia itutumie." Kwa hivyo, uelewa wa vyombo vya habari unakuwa msingi wa kwanza wa jengo la kijamii ambalo ni uraia. Bila elimu, mawasiliano yote huwa hayaeleweki, hoja zote huwa dhaifu. Sote hatuna ulinzi dhidi ya hatari ya kudanganywa na mawazo yetu wenyewe; kuathiriwa na kuenea kwa habari za kugushi; kutokuwa na uwezo wa kutofautisha ukweli na uwongo, wanadamu na mashine, upendo na hesabu.

"Uchumi wa mwasiliano hauwezi kutengenishwa na hatima&kushiriki ukweli"

Kwa sababu hiyo hasa kasi ya kiteknolojia ni ya haraka sana, elimu ndiyo dawa pekee, sio kwa bahati mbaya inayoachilia polepole, kwa hatari ya kasi bila mawazo na uwazi wa kusudi. Kwa sababu hasa mawasiliano yana hatari ya kuwa gumzo tu, aina ya janga la "mawazo yasiyofikiriwa," tunahitaji vyombo vya habari vyenye mamlaka na vya kuaminika. Papa Leo XIV alisema (katika toleo la XXXIX la Mkutano wa Kimataifa wa Akili) kwamba uchumi wa mawasiliano hauwezi na haupaswi kutenganisha hatima yake na kushiriki ukweli. Uwazi wa vyanzo, uwajibikaji, ubora, na usawa ni funguo za kurejesha jukumu la raia kama wahusika wakuu wa mfumo, na kuwashawishi kudai taarifa zinazostahili jina hilo.

“Sisi tuchukue jukumu la AI.Ni juu yetu kufikiria na kuelimisha”

Hii ndiyo sababu ni lazima tulinde nyuso na sauti. Kwa sababu ndani yake kuna ukweli wa sisi ni nani, pamoja na njia ya mawasiliano, shule ya uandishi wa habari, na kigezo cha mafunzo. Kulinda nyuso na sauti kunamaanisha kulinda uwezo wetu wa mawazo, kukataa ukaguzi mtupu wa hesabu za takwimu zinazofuta upekee wa kila mwanadamu. Inamaanisha kuturudisha kwenye njia ya uzuri na ukweli katika kukutana, mazungumzo, ugunduzi wa wengine na ulimwengu, na uandishi wa habari katika kila nyanja. Inamaanisha kuacha kufikiria Akili Unde(AI) kama kitu kingine isipokuwa sisi wenyewe na kuchukua jukumu la AI. Kuelewa kwamba ikiwa algoriti(mashine) zinahesabu na kutenda bila kufikiria, ni juu yetu kufikiria, kuelimisha, na kujifunza katika kufikiri kwa kina. Na ni juu ya vyombo vya habari vya Kikatoliki kuwa kipimo. Kukubali changamoto. Kujua jinsi ya kujifunza historia kwa kuzingatia Injili. Kuonesha kwamba aina nyingine ya mawasiliano inawezekana katika ngazi mahalia, kitaifa, na kimataifa.

“Kila mmoja apaze sauti ilikutetea wanadamu”

Kama Papa Leo XIV  anavyoandika katika ujumbe wake, ni juu ya kila mmoja wetu kupaza sauti zetu katika kuwatetea wanadamu; kuhakikisha kwamba mikakati ya makampuni haiongozwi na kuongeza faida tu, bali na kutafuta manufaa ya wote; uomba uwazi na uwajibikaji wa kijamii kuhusu kanuni za muundo zinazozingatia algoriti. Sisi ndio walinzi wa utambulisho na mabadiliko. Erich Fromm alisema kwamba kazi kuu ya mwanadamu maishani ni kujifungua, yaani, kuwa kile anachoweza kuwa. Hii hapa changamoto. Kuwa mwanadamu zaidi, si bandia zaidi. Kuwa mwangalifu zaidi, si watumiaji wa mawazo yasiyofikiriwa. Epuka kuchagua kutokuwa na uhai badala ya kuwa.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

17 Mei 2026, 11:12