Ask.Pisa kwa mapadre wapya:Maisha ya Padre ni Injili inayoishi
Na Sr Ernestina Patrick Lasway, SAC- Arusha-Tanzania.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Kipapa kwa Mwaka 2026 na Takwimu ya Mwaka ya Kikanisa (Annuarium Statisticum Ecclesiae 2024) ambayo inaelezea harakati na mabadiliko kuhusu uwepo wa waliobatizwa katika mabara matano, iliyochapishwa, ilibanisha kuwa Watawa waliofunga nadhiri ambao si Mapadre, Watawa waliofunga nadhiri na wa vyama vya kitume pia mapadre wa majimbo, wameongozeka katika baadhi ya maeneo ulimwenguni, lakini kwa baadhi ya sehemu nyingine kupungua.
Kupungua huko kuliathiri hasa bara la Amerika, Ulaya, na Oceania, huku Afrika na Asia zikirekodi ongezeko. Asilimia ya usambazaji kwa bara mwishoni mwa 2024 uliona bara la Asia na Ulaya zikiongoza (asilimia 26.7 na 26.4), zikifuatiwa kwa mbali na Amerika (asilimia 25.7), Afrika (asilimia 19.3), na Oceania (asilimia 1.9). Kwa upande wa wa mpadre kwa ujumla, ulimwengu wa wanafunzi wa Falsafa na Taalimungu unapitia mabadiliko makubwa yanayojulikana na mabadiliko yanayopungua sana. Kupungua huku, kunakoonekana katika jumla ya kimataifa, kunaathiri mabara yote isipokuwa Afrika, ambapo wanafunzi wa waseminari walipungua kutoka 34,924 hadi 35,710, ukuaji wa 2.25%. Katika bara la Asia, Ulaya, Amerika, na Oceania, lakini hasa barani Afrika, kupungua huko ni muhimu kwa kiasi cha (-8.98% barani Asia, -5.48% barani Ulaya, -1.67% barani Oceania, na -0.83% barani Amerika).
Kuongezeka kwa miito katika mashirika, upadrisho wa mapadre wa mashirika
Ni katika mtazamo huo ambapo shukrani la ongozeko la waseminari wa majimbo na pia wa mashirika, nchini Tanzania, inaendelea kuneemeka na miito ya kipadre na ya kitawa. Katika mantiki hiyo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Tanzania (TEC,) Mhasham Wolfugang Pisa na Askofu wa Jimbo la Lindi, tarehe 27 Mei 2026, wakati wa madhimisho ya Misa Takatifu ya kuwekwa daraja Takatifu la Upadre katika Parokia ya Mtakatifu Yosefu mume wa Bikira Maria, huko Patandi, Jimbo Kuu Katoliki Arusha nchini Tanzania, aliwatakata "mapadre kujitahidi kuishi kwa kuwaheshimu watu kutokana na nafasi zao mbalimbali katika jamii, kwa kutambua kuhitajiana katika familia ya Mungu na kuwabakiza katika ukweli." Mama Kanisa aliwapokea: Shemasi Straton Honest Ngowi C.S.S.p, Shemasi Edward Moshi Simkonda C.S.S.p, Shemasi Joseph Alphonce Mushi, C.S.S.p, Shemasi Justus Asingizibwe Dominick C.S..S.p, Shemasi Barnaba Joseph Kyara, C.S.S.p na Shemasi Barthlomeo Florian Paulo,SAC na kupewa daraja Takatifu ya Upadre.
Tambua nafasi yako katika Kanisa na utume wako
Askofu Pisa katika homilia yake, aliwataka mapadre wapya kutambua nafasi yao katika Kanisa na utume wao. "Mara baada ya upadrisho ni lazima Padre akubali nafasi na wadhifa anaopewa na Kanisa." Kwa kutambua nafasi yao, "mapadre wawe waadhimishaji wa sakramenti za Kanisa, hasa sakramenti ya upatanisho." Alikazia kuwa “mapadre, ninyi wenyewe muungame, na kuwafundisha watu kufanya hivyo,” kwani kwa mujibu wa mafundisho ya Mtakatifu Ignatius kuwa “Sakramenti ya upataniosho ni utambulisho wa Mkristo Mkatoliki.” Ili kuingizwa katika sakramenti ya Ekaristi, ni lazima Mkristo kupokea Ekaristi Takatifu. Mtakatifu Chrysostom alisisitiza katika mafundisho kuwa, “Padre ni muhimu sana, kuliko malaika hata malaika wakuu kwani anaweza kufanya maadhimisho ya Ekaristi Takatifu na kumwondolea Mkristo dhambi.”
Mapadre mjali hali zenu na Mahangaiko katika Utume
Familia ni Kitalu cha Miito mitakatifu
Katika mahubiri hayo Askofu Pisa aliwaomba wanafamilia kupenda na kulea vyema miito mitakatifu kwa uvumilivu na uchaji. Mama na baba wakitambua na kutimiza wajibu wao katika jamii, maisha yatakuwa na maana zaidi. “Wazazi wawalee watoto katika utakatifu wa sakramenti badala ya kuhangaikia sherehe na tafrija kumbwa badala ya maandalizi ya kiroho. Mapadre wawe walinzi wa maadili na maadhimisho ya sakramenti badala ya maisha ya nje.” Kanisa ninapaswa kufundisha kwa usahihi wala siyo kuishi na kufundisha kuendana na “hali ya watu,” alisisitiza Askofu Pisa. Mapadre waliopadrishwa wamehimizwa kuwasaidia watu na kuwafundisha ukweli katika ulimwengu wa usasa, alitamatisha.
Mapadre msitumie akili unde katika utume
Hata kwa niaba ya wakuu Shirika, alitoa neno Padre John Onna huku akiwatakia matashi mema mapadre wapya na kuwaomba wajitolee maisha yao yote kwa Mungu. Kwa upande wa wazazi Padre Onna aliwashukuru kwa kuwazaa, kuwalea na kuwaruhusu kujiunga na maisha ya upadre. Aliwataka wazazi hata hivyo “ kuwalea watoto katika imani thabiti.” Wazazi “Msiruhusu watoto kulelewa na wazazi bandia” yaani mitandao na teknolojia” alisisitiza Padre Onna. Kwa njia hiyo aliwasihi “kuonesha uso wa Kristo kwa watu wote watakaowahudumia na kamwe wasitumie akili unde katika utume.” Badala yake alisisitiza “watumie neema ya Mungu waliyo nayo kutafakari Neno la Mungu na kuliishi siku zote za maisha yao”.
Imesasishwa tarehe 29 Mei 2026 saa 12.00 jioni na Angella Rwezaula - Vatican.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.