Tafuta

Furaha ya Kardinali Jean-Marc Aveline wa Ufaransa kuhusu ziara ya Papa leo XIV kuanzia 25-28 Septemba 2026. Furaha ya Kardinali Jean-Marc Aveline wa Ufaransa kuhusu ziara ya Papa leo XIV kuanzia 25-28 Septemba 2026.  (Vatican Media)

Kard.Aveline:Ujio wa Papa Leo XIV nchini Ufaransa ni furaha kwa Kanisa Katoliki

Kardinali Jean-Marc Aveline,Askofu Mkuu wa Marseille na Rais wa Baraza la Baraza la Maaskofu wa Ufaransa,alikabisha kwa furaha tangazo la ziara ya Kitume ya Papa Leo XIV kwenda Ufaransa mnamo tarehe 25-28 Septemba 2026.

Na Jean-Charles Putzolu – Vatican.

Askofu Mkuu wa Marseille na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Ufaransa baada ya kutangaza ziara yake ya Kitume ya Baba Mtakatifu leo XIV ya kwenda Ufaransa kuanzia Septemba 25 hadi 28,2026 alibainisha kuwa “Ni furaha kubwa" kwa Kanisa, kwa Ufaransa, kwa Wakatoliki wa Ufaransa, na kutia moyo kwa Kanisa linalojitahidi kukabiliana na changamoto nyingi, baadhi yakilenga kugeuza hali ya nyakati ngumu, mengine yakiambatana na misukumo ya upyaishaji, inayoonekana katika idadi inayoongezeka ya wakatekumeni na kuongezeka kwa shauku katika hija.” Kardinali Jean-Marc Aveline alizungumza  hayo na Vatican News kuhusu jinsi Kanisa nchini Ufaransa limeitikia tangazo hilo na kile wanachotarajia kutoka kwa ziara hii. Yafutayo ni mahojiano kamili

Askofu Mkuu, una maoni gani kuhusu tangazo la ziara hii, ambalo wewe mwenyewe ulikuwa umelitaja muda uliopita, ukisema ulitarajia itatokea?

Ninakaribisha tangazo hili kwa furaha kubwa. Tulikuwa tumelitarajia na kulisubiri, kama nilivyosema. Kuanzia wakati wa kuchaguliwa kwa Papa Leo XIV, tulijadili uwezekano wa ziara nchini Ufaransa. Niliweza kuona jinsi alivyojitolea kibinafsi kwa mpango huu. Hakukosa fursa ya kutuma ujumbe mdogo wa kutia moyo kwa mapadre au kwa matukio maalum. Ninaamini naweza kusema, baada ya kufanya kazi naye mara kadhaa kuhusu jambo hili, kwamba kuna wasiwasi na mapenzi ya kweli kwa nchi yetu kwa kile kinachowakilisha, katika historia yake, na kwa jinsi imeenea kote Kanisani na ulimwenguni kupitia watu mashuhuri wa utakatifu. Wakati huo huo, kuna changamoto zinazolikabili Kanisa nchini Ufaransa leo, ambazo zinashirikiwa na nchi zingine lakini pia zina sifa za kipekee. Nadhani hii ni habari njema si tu kwa Kanisa la Ufaransa, bali pia kwa nchi yetu.

Mnamo tarehe 28 Machi, Papa Leo XIV alikuwa Monaco. Wafaransa walifuatilia kwa karibu ziara hiyo. Mlisherehekea katika Uwanja wa Louis II. Wakatoliki nchini Ufaransa wanatarajia nini kutokana na ziara ya Papa Leo?

Wakatoliki wanatarajia ziara ya Papa, walikwenda kwa wingi huko Marseille, Corsica, na pia Monaco, kwa sababu Kanisa nchini Ufaransa linapitia hali halisi tofauti sana, lakini pia mambo mengi mazuri, kama vile idadi inayoongezeka ya vijana wanaomtambua Kristo na kuomba Kanisa ubatizo au kipaimara. Kwa sasa niko Lourdes na mahujaji 1,500 kutoka Jimbo la Marseille, na miongoni mwao wamo vijana wengi na vijana wadogo kwa wakubwa ambao wamemgundua Kristo na ambao hii ni hija yao ya kwanza. Mimi binafsi nimeshangazwa na maendeleo haya ya ajabu, ambayo yanahitaji Kanisa nchini Ufaransa kujipanga vizuri ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Pamoja na maendeleo haya mazuri, pia tunaona kuibuka tena kwa hija na umuhimu unaoongezeka wa Madhabahu ya Maria katika nchi yetu. Pia kuna masuala nyeti zaidi. Kwa mfano, katika maeneo ya vijijini, ninaona jamii zinazozeeka. Kanisa nchini Ufaransa pia linakabiliwa na hii hali halisi. Tumepitia mgogoro wa unyanyasaji na nyanyaso za kingono katika Kanisa halijaisha; bado kuna kazi nyingi ya kufanya na heshima kubwa ya kuelezea. Papa Leo XIV anafahamu sana haya yote. Kwa hivyo anakuja kutusikiliza, kututia moyo, na pia kutupatia mwelekeo wa jinsi tunaweze kuendelea na utume wetu katika ushirika na Kanisa la ulimwengu wote. Yote haya ni muhimu sana, na nadhani miezi minne si muda mrefu wa kujiandaa kwa ziara hii.

Askofu Mkuu, umetaja  magumu ambayo Kanisa la Ufaransa linafanya kazi kuyashinda. Je, unaona ziara hii kama kutia moyo kwa kazi yote ambayo imefanywa kushughulikia masuala haya magumu?

Ndiyo, naweza kuona hili katika matukio mbalimbali nilipopata fursa ya kujiandaa kwa  ziara binafsi na Papa. Ninaona kwamba tayari tumeanza kazi yetu. Tutaendelea, lakini nadhani ni muhimu pia kwamba Kanisa nchini Ufaransa litambue neema inayotolewa kupitia ziara ya Mrithi wa Petro. Tunahitaji kujiandaa; tunahitaji kutafakari tunachopitia. Lazima tuvike mioyo yetu na kumruhusu Roho Mtakatifu avike mioyo yetu, kwa sababu tunahitaji kuwa wazi kwa kile ambacho ziara hii ya kipapa itatuletea kwa maneno yake na ujumbe wake. Pia lazima tujiandae ili tuweze kumweleza waziwazi tunachopitia, ili aweze kukielewa kikamilifu na kukiweka maanani, na kisha, kupitia huduma yake na mamlaka ya kufundisha, atupe mwelekeo wa miaka ijayo.

Vatican bado haijachapisha mpango wa ziara hii. Hata hivyo, katika taarifa ya awali, Kanisa nchini Ufaransa lilisema lilitarajia Papa Leo XIV huko Paris na Lourdes

Ndiyo, ndivyo ilivyopangwa. Ni muhimu sana Papa awe Paris. Pia atakwenda makao makuu ya UNESCO, na pia anatarajiwa kutembelea Lourdes - kituo kingine muhimu. Bado kuna nafasi kidogo iliyobaki katika ratiba yake, na tutaona jinsi mambo yanavyoweza kupangwa. Ziara za awali zitafanywa hivi karibuni, na zitaturuhusu kutathmini vyema uwezekano wa matukio ya ziada. Tusisahau kwamba ziara hii ni fupi sana: kuanzia Septemba 25 hadi 28. Baadaye, Papa hakika atakuwa na fursa zingine za kuja Ufaransa, ikiwa Mungu atampa uhai na afya.

Hotuba imepangwa katika makao makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO), katika mwaka wake wa kwanza wa upapa, Papa Leo XIV amezungumzia mara kadhaa kuhusu mada hizi, akisisitiza tabia ya msingi ya elimu, kukamilishana kwa sayansi na imani, na kuwasilisha utamaduni kama daraja kuelekea udugu na amani.

Mkutano huu uliopangwa katika makao makuu ya UNESCO unaonesha mada muhimu kwa Kanisa zinazoingiliana. Kwa mfano, uhusiano kati ya imani na mantiki,  jambo ambalo Papa Benedikto XVI alituhimiza sana kulifanyia kazi wakati wa Ziara yake kwenda Ufaransa mwaka 2008. Kisha kuna mafundisho ya kijamii ya Kanisa Katoliki, ambayo pia yanahusu usemi halisi wa imani ya Kikristo katika maisha ya kila siku. UNESCO pia inahusu elimu. Kanisa nchini Ufaransa limeamua kujitolea miaka mitatu kufanya kazi kwenye mada ya elimu kwa sababu inagusa masuala mengi, hasa ya familia. Ni mada muhimu sana si kwa Kanisa tu bali kwa jamii ya Ufaransa kwa ujumla. Mbinu ambayo tumechukua na ambayo nilipata fursa ya kumweleza Papa ni kuchunguza hazina za Kanisa, hasa kupitia makutaniko yake mengi ya kielimu kama vile Wasalesiani wa Don Bosco na wengine, ambayo ni lazima tushiriki, na pia kupitia kile ambacho tumefanya na mawazo haya, ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo bado tunahitaji kuboresha. Tuna kazi kubwa mbele. Mpango wetu unalenga kuwaalika waekezaji wengine katika ulimwengu wa kielimu  ambao si lazima washiriki imani ya Kikristo kukaa meza moja na kujadili changamoto zinazokabili elimu leo. UNESCO, ambayo inaunganisha sayansi, utamaduni, na elimu ndani ya taasisi ya kimataifa, inawakilisha hatua muhimu sana wakati ambapo kanuni za sheria za kimataifa zinahitaji kuthibitishwa tena.

Septemba ijayo itakuwa Ziara ya Tano ya Kitume ya Papa Leo XIV Ufaransa, na tayari ni ya tatu barani Ulaya, Ulaya hii ambayo inaishi katika kipindi chenye matatizo na labda muhimu katika historia yake. Tunaona hili kupitia mgawanyiko tata wa dunia na kuongezeka kwa vita. Ni ujumbe gani tunaweza kutarajia Papa Leo XIV atoe kuhusu Ulaya?

Tutasikiliza anachotaka kuliambia bara la Ulaya. Ziara ya Papa katika nchi ni ujumbe kwa Kanisa na watu wa nchi hiyo, na pia ujumbe kwa Kanisa la ulimwengu wote na kwa wanaume na wanawake wote wenye nia njema kote ulimwenguni. Katika nchi yetu, tumekisiwa na vita barani Ulaya, lakini pia na nguvu ya ajabu ya upatanisho kama njia ya amani baada ya uharibifu mkubwa uliosababishwa na vita vilivyofuata. Uzoefu huu katika karne ya ishirini Ulaya pamoja na ukatili mbaya zaidi tunaoujua haukuzuia mchakato wa upatanisho kukua hadi kufikia hatua ambayo ikawa chanzo cha mradi wa kiuchumi na kisiasa ulioendelezwa na wanaume ambao wenyewe walikuwa Wakristo, miongoni mwa wengine ni kama vile Alcide De Gasperi, Konrad Adenauer, na Robert Schuman.

Msukumo wa Kikristo uliwezesha upatanisho kati ya watu ambao walikuwa wamepigana vita kadhaa dhidi ya kila mmoja kuwa nguvu inayoongoza ujenzi wa mradi wa kisiasa, hata kama mradi huo hauishi kulingana na hisia ya awali iliyouzalisha. Nadhani hii ni muhimu leo​​​​kwa sababu ya muktadha ambao tunajikuta, na Papa amesisitiza hili mara kwa mara. Lazima tufanye kazi kwa ajili ya amani na kujenga juu ya uzoefu huu wa Ulaya, ambao, ingawa si wa kipekee, ni muhimu sana. Lazima tuangazie umuhimu wa ushuhuda wa Ulaya na nguvu ya upatanisho kwa ajili ya ujenzi wa amani duniani.

Imesasishwa tarehe 19 Mei 2026 saa 5.15 asubuhi na Sr Christine Masivo.

ASKOFU MKUU AVELINE

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

19 Mei 2026, 11:07