Kard.Francis wa Malaysia:Utofauti wa Asia ni utajiri na sio tishio
Na Joseph Tulloch – Vatican.
Maaskofu wa Malaysia, Singapore, na Brunei wako kwenye ziara yao ya kitume (Visita ad Limina apostolorum) ambayo hufanyika kila baada ya miaka mitano, na kuwaleta pamoja wote Roma kwa ajili ya mikutano na wakuu wa mabaraza mbali mbali ya Kipapa na Papa. Miongoni mwa kundi la maaskofu hao ni Kardinali Sebastian Francis, Askofu Mkuu wa Penang huko Malaysia Magharibi. Katika mahojiano na Vatican News, alizungumzia kuhusu safari yao ya Roma, Kanisa "lenye nguvu" katika pembe ya Asia, na umuhimu wa kuona utofauti kama utajiri, badala ya tishio. Yafuayao ni mahojihano hayo yaliyohaririwa kwa ufupi kwa sababu za mtindo na uwazi.
Uko hapa, pamoja na maaskofu wengine wa Malaysia, Singapore, na Brunei, mjini Roma kwa ziara yenu: ‘Visita ad Limina apostolorum’. Je inaendeleaje?
Tunatarajiwa kutoa ripoti. Ninaona ni nzuri na ya nidhamu sana, lakini pia ni ya amani sana, kwa hivyo nimetulia sana, lakini pia niko makini. Nadhani ziara hii itaimarisha uhusiano kati yetu maaskofu wa Malaysia, Singapore, na Brunei, na hakika itaimarisha umoja wetu na Kanisa la Ulimwengu chini ya Papa Leo XIV. Nina hisi uhusianao na mshikamano mwema. Siwezi kuelezea, lakini naihisi. Hadi sasa, tumekutana na Mabaraza matatu ya Kipapa,Vatican. Tutakutana na Baraza la nne leo, na nimeshangazwa na ubora wa majadiliano. Wakati huu ilikuwa ya undani na yenye maana na umakini zaidi. Nadhani hiyo ndiyo roho ninayohisi Roma siku hizi.
Tukitoka Roma hadi sehemu unakotoka, unaweza kutuambia nini kuhusu Kanisa huko Malaysia, Singapore na Brunei?
Ni ya amani. Nchi mbili tunazowakilisha, Singapore na Brunei, zimeendelea sana, wakati Malaysia ni nchi inayoendelea. Siasa ni thabiti kabisa na Kanisa lina nguvu sana, linaendelea vizuri, na tuna watu wazima wengi wanaouliza kuhusu imani ya Kikatoliki. Wengi wao wanaomba Ubatizo wakiwa watu wazima. Hilo linatuweka kuwa makini.
Je, ni baadhi gani ya changamoto katika Kanisa kwenye hizi nchi hizi tatu?
Kanisa hili lina dini nyingi, tamaduni nyingi na hata lugha nyingi. Lakini haitoshi kuzifikiria kama changamoto! Badala yake tunapaswa kuzifikiria kama utajiri, utofauti ni utajiri, na umoja katika utofauti ni rasilimali watu. Utofauti sio tishio, na ndani ya utofauti, kuna usawa. Kwa mambo haya matatu, umoja, utofauti na usawa, ni kuhusu Utatu, na ni kuhusu sisi. Hilo ni la kusisimua sana, kiukweli, na kwa mwelekeo sahihi tunaweza kukabiliana na changamoto pamoja. Hata kama sehemu zingine za Asia bado zinaweza kupitia aina fulani ya mateso, hatupaswi kuangukia katika mtego wa kuwa na 'changamoto za walio wachache',ile ya changamoto ya mateso. Bila shaka, kuna masuala halisi, lakini tutaendelea kusimulia historia ya Yesu huko Asia.
Imesasishwa tarehe 19 Mei 2026 saa 10.10 jioni na Sr Christina Masivo.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.