Maaskofu wa Pakistan watoa matumaini na wasiwasi wakati wa ziara
Vatican News
Maaskofu wa Pakistan walionesha matumaini kwa mustakabali wa Kanisa katika nchi yao huku wakiakisi changamoto kubwa zinazowakabili Wakristo, ikiwa ni pamoja na ubaguzi, shutuma za kufuru, na kulazimishwa kubadili dini. Akizungumza wakati wa ziara ya Maaskofu wa Pakistan ya ad limina Apostolorum mjini Vatican, Askofu Samson Shukardin, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Pakistani na Askofu wa Hyderabad, alisema ziara hiyo imekuwa chanzo cha kutia moyo na upya kwa Maaskofu. Ziara ya Kichungaji ‘ad limina Apostolorum’ ni hija ya mara kwa mara ambayo Maaskofu Wakatoliki hufanya katika Kiti Kitakatifu, kwa kawaida kila baada ya miaka mitano, ili kutoa taarifa kuhusu hali ya majimbo yao, kukutana na Papa na wakuu wa Mabaraza ya Kipapa, na kusali katika makaburi ya Watakatifu Petro na Paulo jijini Roma. Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana nao tarehe 15 Mei 2026 wakati wakiwa katika ziara yao ya kitume.
Tumaini jipya na ufahamu wa wakati ujao
"Tangazo hili ni muhimu sana kwetu kwa sababu kiroho na kimwili, hili limetupatia ufahamu mpya na matumaini mapya katika siku zijazo zijazo," Askofu Shukardin alisema. Alieleza kwamba ujumbe huo uliwasilisha ripoti kwa wakuu wa Mabaraza mbalimbali ya Vatican na ulipokea majibu chanya kutoka kwa Wakuu wa Curia. "Tumeshiriki ripoti zetu katika mabaraza tofauti, na tulipokea majibu chanya sana kutoka kwa wakuu tofauti, jambo ambalo ni muhimu sana kwetu," alisema.
Changamoto Kuu
Akitafakari maisha ya Kanisa nchini Pakistan, Askofu Shukardin alitaja uinjilishaji kama mojawapo ya changamoto kuu zinazokabili jamii ya Wakatoliki wa eneo hilo. Aliwaelezea waamini Wakatoliki wa Pakistan kuwa wamejitolea sana licha ya ugumu wa kiuchumi na fursa chache za kielimu. "Watu wetu bado hawajui kusoma na kuandika lakini wana imani thabiti," Askofu alisema. "Ni maskini lakini ni watu wanaofanya kazi kwa bidii, na kujituma kwa bidii kila wakati." Wakati huo huo, alilalamika kuhusu matatizo yanayowapata Wakristo wengi katika jamii ya Pakistan. "Watu wetu wengi hawapati haki sawa," alisema.
Suala la kukufuru
Askofu Shukardin pia aliakisi wasiwasi unaozunguka shutuma za kufuru na kulazimishwa kubadilisha dini, masuala ambayo yameathiri mara kwa mara makundi madogo ya kidini nchini. "Tuna tatizo kubwa kuhusu kesi za kukufuru," alisema, akiongeza kuwa "kulazimishwa kubadili dini kupo." Pia alibainisha kuwa Wakristo wakati mwingine hukabiliwa na kukataliwa na kuteswa kwa sababu ya imani na ushuhuda wao. "Wakati mwingine Kanisa letu hukataliwa, huteswa kwa sababu hatuendi mahali tuapolazimishwa," alisema, lakini licha ya matatizo haya, Askofu Shukardin alisisitiza kwamba Kanisa nchini Pakistan linaendelea kutazama mustakabali kwa matumaini. "Kanisa letu linapitia magumu, lakini tuna matumaini makubwa," alisema. "Tuna matumaini kwamba siku moja tutapata haki zetu sawa nchini Pakistan."
Imesasishwa tarehe 16 Mei 2026 saa 4.20 asubuhi na Angella Rwezaula
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.