Tafuta

CCEE na SECAM watakutana huko Luxembourg kujadili juu ya Uinjilishaji na Sinodi. CCEE na SECAM watakutana huko Luxembourg kujadili juu ya Uinjilishaji na Sinodi. 

Maaskofu wa Ulaya na Afrika wakutana Luxembourg:'Uinjilishaji na Sinodi:Njia za Bara'

Maaskofu wa Ulaya(CCEE )na Afrika(SECAM),watakutana huko Luxembourg kuanzia tarehe 25 hadi 28 Mei 2026 ili kujadili pamoja juu ya Uinjilishaji na Sinodi:Njia za Bara.Mara ya mwisho kwa taasisi hizi mbili kukutana ilikuwa mnamo mwaka 2004.

Vatican News

Kuanzia tarehe 25 hadi 28 Mei 2026, ujumbe wa maaskofu kutoka Shirikisho la mabaraza ya Maaskofu  wa Ulaya (CCEE) na kutoka Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar(SECAM) watakutana huko  Luxembourg kwa ajili ya Semina kuhusu: "Uinjilishaji na Sinodi: Njia za Bara." Semina hiyo itafanyika ikifuatia na ilie ya mnamo mwaka  2004 ili kutoa fursa muhimu kwa ajili ya kubadilishana taarifa na kutafakari kwa pamoja kuhusu changamoto zinazolikabili Kanisa duniani, na italenga mwaka huu 2026 kuchunguza awamu ya utekelezaji wa Sinodi na maendeleo yanayofanywa katika Makanisa mahalia pamoja na changamoto za uinjilishaji katika miktadha tofauti ya bara kwa kuzingatia Wosia wa  Baba Mtakatifu Francisko wa  Evangelii Gaudium yaani Injili ya Furaha uliochapishwa tarehe 24 Novemba 2013.

Ratiba ya tarehe 25 Mei 2026

Ratiba itaanza Jumatatu tarehe 25 Mei  2026 kwa ziara ya Tamasha la kiutamaduni la Echternach katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Willibrord. Sherehe ya uzinduzi itaongozwa na Askofu  Heiner WILMER, SCJ, wa Jimbo la  Münster na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Ujerumani.

Tarehe 26 Mei 2026

Siku ya Jumanne tarehe 26 Mei, washiriki watahudhuria Misa Takatifu katika Abasia ya Echternach, ikiongozwa na Kardinali Ladislav NEMET, SVD, Askofu Mkuu wa Belgrade na Makamu Rais wa CCEE, na kutakuwa na maandamano maarufu ya ngoma ya kiutamaduni ya Echternach (Iechternacher Sprangprëssioun), ambayo ni  ibada ya Mtakatifu Willibrord na imesajiliwa kwenye Orodha ya Wawakilishi wa Urithi wa Utamaduni Usiogusika wa Binadamu. Alasiri hiyo hiyo, shughuli zitaanza na salamu za ufunguzi na utangulizi kutoka kwa  Askofu Mkuu Gintaras GRUŠAS, wa Vilnius na Rais wa Shirikisho la Mabaraz aya Maaskofu Ulaya (CCEE,) na kwa Kardinali Fridolin AMBONGO, OFMCap., Askofu Mkuu wa Kinshasa na Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika na Madagascar(SECAM.) Hii itafuatiwa na utambulisho wa washiriki kutoka kwa vyombo viwili vya Kanisa.

Tarehe 27 Mei 2026

Jumatano tarehe 27 Me, siku  itaanza na Misa Takatifu ikiongozwa na Kardinali  Fridolin AMBONGO, OFMCap. Vikao vya kazi vitajikita na "Awamu ya Utekelezaji wa Sinodi kuhusu Sinodi." Miongoni mwa hotuba zitakazotolewa ni pamoja na ile ya Kardinali Jean-Claude HOLLERICH, SJ, Askofu Mkuu wa Luxembourg na Makamu Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (CCEE,) kuhusu Timu ya Sinodi ya wajumbe wa kitaifa wa Ulaya, na ile ya Askofu Lucio Andrice MAUNDULA, wa Jimbo la Chimoio na Mratibu wa Timu ya Sinodi ya Afrika. Hizi zitafuatiwa na mawasilisho kutoka kwa Kardinali  Ladislav NEMET, SVD, kuhusu Kikosi Kazi cha Sinodi ya Ulaya, na kutoka kwa Askofu Mkuu  Anthony MUHERIA, wa Jimbo Kuu la Nyeri na Makamu  Rais wa Shirikish la manbaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki  AMECEA, ambaye hotuba yake itajikita  kwa kazi ya sinodi katika muktadha wa Afrika na kwa desturi bora za kichungaji. Alasiriy a siku hiyo, kutakuwa na vipindi vya "Mazungumzo katika Roho" na majadiliano ya jumla.

Tarehe 28 Mei 2026

Siku ya mwisho, Alhamisi tarehe 28 Mei, itatengwa kwa ajili ya  Waraka wa “Evangelii Gaudium” na mada ya uinjilishaji katika muktadha wa Ulaya na Afrika. Wazungumzaji watakuwa Askofu  Alexandre JOLY, wa Jimbo la Troyes, na Askofu Mkuu José Manuel IMBAMBA, wa Jimbo  Kuu la Saurimo na Makamu wa Pili wa Rais wa SECAM. Semina hiyo  itahitimishwa kwa kazi ya kikundi, muhtasari wa mwisho na Maadhimisho ya Misa Takatifu ikiongozwa na Askofu  Gintaras GRUŠAS, Rais wa CCEE.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

22 Mei 2026, 14:46